Home » » ‘KAGERA INA WALEMAVU 150,000’

‘KAGERA INA WALEMAVU 150,000’

ASAS ya kiraia ya Karagwe Community Based Rehabilitation Program (KCBRT), imesema kuwa, mkoa wa Kagera una jumla ya walemavu 150,000, wanaokabiliwa na changamoto mblimbali.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Mtendaji wa asasi hiyo, Agrey Mashanda wakati akisoma risala ya ujenzi wa kituo cha utengemavu kinachotarajiwa kujengwa katika eneo la Nyakanongo Kata ya Ndama kwa kufadhiliwa na shirika la Uholanzi la Lilian Foundation.
Mashanda alisema kuwa idadi hiyo ni sawa na asilimia 5.8 ya watu wote katika mkoa wa Kagera ambapo katika wilaya ya Karagwe, shirika linahudumia zaidi ya walemavu 10,000 katika kaya 31tangu mwaka 2004 hadi 2014.
Alisema kuwa, shirika hilo la Uholanzi limetoa kiasi cha sh. milioni 460, ambapo ujenzi kwa awamu ya kwanza utakamilika kwa kipindi cha miezi tisa kuanzia sasa kabla ya kuanza wa awamu ya pili na ya tatu.
Kwa mjibu wa katibu huyo, jengo hilo ambalo litahusika na shughuli za walemavu litakuwa na ukumbi wa mikutano, nyumba mbili za utumishi, matanki ya maji, vyumba vya walemavu kwa ajili ya mazoezi, jengo la taaluma, chumba cha upasuaji na mazoezi ya viungo.
Aliongeza kuwa ujenzi kwa awamu ya kwanza utagharimu sh.bilioni 150 na kwa awamu ya pili zitatumika sh. million 506 wakati awamu ya tatu itagharimu sh. million 367.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa