Home » » WANANCHI WAONYWA KUTOWAKARIMU WAGENI WASIOWAJUA

WANANCHI WAONYWA KUTOWAKARIMU WAGENI WASIOWAJUA


Kamanda wa polisi mkoa wa Geita, Joseph Konyo
Makamanda wa Polisi wa Kigoma, Kagera na Geita, wamewataka wananchi kutowakarimu wageni wasiowajua kwani wengi wao ni wahalifu wanaotumia silaha za moto.
Kutokana na hofu ya kuwapo kwa wageni wengi katika mikoa hiyo, makamanda hao wameamua kuzindua mpango endelevu wa kuangamiza mtandao wa uhalifu wa kutumia silaha unaotishia maisha ya wananchi wengi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita, Joseph Konyo, alisema wananchi lazima wachukue tahadhari baada ya Januri 19 mwaka huu katika kitongoji cha Mhama kijiji cha Ilyamchele wilayani Bukombe, Geita, kuwakarimu majambazi kwa kuwapa chakula na vinywaji wakiamini ni wasamaria wema, lakini baadaye wakafanya uhalifu na uporaji kwa kutumia silaha za moto.
Konyo alisema alisema wagani hao ambao wengi wao huvuka mipaka toka nchi za jirani, jeshi la polisi la mikoa hiyo mitatu imeamua kuzindua mkakati kabambe wa kuuteketeza mtandao huo.
Naye kamanda wa polisi mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe, alizindua mkakati huo Januari 20 katika kijiji cha Nyakanazi wilayani Biharamulo mkoa wa Kagera.
Majambazi hao ambao baada ya kufanya uharamia wa uporaji, walisakwa na polisi na kuishia kupora mchele kilo 60 na baiskeli tatu ambazo walitumia kubebea mchele huo wa uporaji.
Aidha, alisema majambazi hao baada ya kufanya uporaji waliondoka katika kijiji hicho na kuteketekeza kwa moto kwa kuwatisha wanakijiji na polisi ili wasiwafuatilie.
Hata hivyo, ilielezwa mtandao huo wa ujambazi wa kutumia silaha umeshamiri katika miji ya Lunzewe, Namonge, Kasanda  na Mabamba iliyopo mikoa ya Geita, Kagera na Kigoma, baada ya kufanya uhalifu huvuka mipaka na kukimbilia nchi jirani.
Mwaka jana watu wanaosadikiwa majambazi, walivamia kituo kikuu cha polisi wilaya ya Bukombe mkoani Geita ,kuua polisi wawili na  kupora silaha mbalimbali lakini  na ushirikiano na wananchi uliwezesha  polisi kuwakamata watuhumiwa pamoja na silaha zilizoibwa.
CHANZO: NIPASHE 
KUELEKEA UCHAGUZI 2015: JE UNAPENDA NANI AWE KIONGOZI WAKO? JAZA FOMU HII FUPI HAPA

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa