Home » » ANASWA AKIIBA MAHINDI, ALAZIMISHWA KULA MABICHI!

ANASWA AKIIBA MAHINDI, ALAZIMISHWA KULA MABICHI!

Akilazimishwa kula maindi hayo.
Akila maindi hayo ili kuepuka kichapo.


HAMIDA HASSAN
Jamaa ambaye jina halikuweza kupatikana mara moja, amejikuta akionja joto ya jiwe baada ya kudaiwa kukutwa akiiba kwenye shamba la mahindi hivyo kulazimishwa kula mahindi mabichi.Tukio hilo la aina yake lilijiri hivi karibuni kwenye Kata ya Miembeni, Bukoba mkoani Kagera na kuibua gumzo kubwa.

Kwa mujibu wa shuhuda wetu, baada ya kumnasa kijana huyo akiiba mahindi aliyoyajaza kwenye gunia, wamiliki wa shamba hilo walimuamuru kukaa chini na kuyala yakiwa mabichi hadi yaishe, kitendo ambacho jamaa huyo alikubaliana nacho.

lielezwa kwamba, katika hali ya kushangaza, kijana huyo hakukataa wala kuonesha kutetereka kwani alianza kuyala hadi alipoamriwa kuacha na kuambiwa aondoke.Katika habari hiyo iliyoripotiwa na Mtandao wa Harakati, kijana huyo alionekana kuwa na matatizo ya kutosikia vizuri wala kuongea kwa maana ya kuwa ni ‘bubu’.

Hata hivyo, kijana huyo hakujulikana alitokea wapi kwani mbali na madai ya wizi na ububu pia hakuonekana mwenye ufahamu mzuri kutokana na mavazi aliyokuwa amevaa. GPL

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa