MADIWANI WA HALMASHAURI ZA KYERWA NA BIHARAMULO WAANZA MAFUNZO YA YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA PS3 MKOANI KAGERA

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, Deusdedith Kinawiro akifuyngua mafunzo ya siku nne ya Madiwani kutoka Hlamashauri mbii za Kyerwa na Biharamuo juu ya namna ya utekelezaji wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za umma (PS3) chini ya ufadhili wa Serikali ya Marekali kupitia shirika ake la misaada la Kimataifa (USAID) ikishirikiana na serikali kuu.

Mradi huo ulizinduliwa Julai 12 mwaka huu ambapo Halmashauri hizo mbii ndio zitatekeeza mradi huo mkoani Kagera kwa awamu ya kwanza.

Kinawiro alisema anatarajio kuona mafunzo haya elekezi yanatumika kama ilivyokusudiwa, na waheshimiwa madiwani wanapata uelewa na maarifa kuhusu uendeshaji wa Serikali za Mitaa, pamoja na wajibu na majukumu yao katika kusimamia uendeshaji wa Mamlaka hizi.




Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Kanali (Mstaafu), Shabaan Lissu akiwa na Mkuu wa Wiaya ya Biharamulo, Saada Malunde wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ya madiwani yaliyofanyika mjini Bukoba leo.
 Mwenyekiti wa Hlamashauri ya Kyerwa, Kashunju Runyogote (kushoto) akiwa na madiwani wenzake wa Kyerwa wakifuatilia hotuba ya ufunguzi.
 Baadhi ya Madiwani na Watendaji wa Hamashauri za Kyerwa na Biharamuo mkoani Kagera wakifuatilia ufunguzi huo.
 Kiongozi wa timu ya Uzinduzi ya PS3 Mkoani Kagera na Mtaalam wa Fedha wa Mradi huo wa PS3, Abdul Kitula akizungumza juu ya mafunzi hayo kwa madiwani.

Kitua aliwataka watendaji hao kushiriki kikamilifu katika mafunzo hayo ambayo ndio utekelezaji wa mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za  Umma ambao nchini unatekelezwa katika mikoa 13 na kuzinufaisha Halamashauri 93. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

HALMASHAURI ZA WILAYA KYERWA NA BIHARAMULO ZAANZA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UIMARISHAJI MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA.

Mwakilishi wa Shirika la Misaada la Kimataifa la Makani (USAID), Moses Busiga akizungumza wakati wa kikao cha kwanza cha maofisa watendaji wa Halmashauri mbili za Wilaya ya Kyerwa na Biharamulo mkoani Kagera kilichofanyika leo ikiwa ni kuanza kwa utekelezaji wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za umma (PS3) Mkoani Kagera. Source:Father Kidevu Blog
 Kiongozi wa timu ya Uzinduzi wa Mradi wa PS3 Mkoani Kagera, Abdul Kitula akizungumza

Washiriki wakisikiliza kwa makini mada
Washiririki walikaa katika makundi na kuainisha wadau mbalimbali wa maendeleo walioko katika halmashauri zao na namna ambavyo wanashirikiana katika kuimarisha mifumo ya sekta za umma.
Wataalam wa masuala ya Utawala nao walishiriki kuhakikisha mambo yanaenda vizuri.
 Afisa Mipango wa Halamashauri ya Wilaya ya Kyerwa, Johansen Karugaba akiwasilisha taarifa ya Wilaya yake.
 Dk Rest Lasway wa mradi wa PS3 akitoa mapendekezo yake.
 Afisa Maenendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Sebastian Kitiku akitoa mapendekezo.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, Kashunju Runyogote akitoa maoni yake.
  Afisa Mipango wa Halamashauri ya Wilaya ya Biharamulo, Andambike Kyomo akiwasilisha taarifa ya kundi lake.
 Mmoja wa washiriki akichangia maoni
Mtaalam wa masuala ya Rasilimali watu kutoka Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), Remmy Moshi akiwasilisha mada.
 Afisa Elimu wa Halamashauri ya Wilaya ya Kyerwa akifafanua jambo.
 Ofisa wa PS3, Desderi Wenger akizungumza wakati wa uwasilishaji wa taarifa za vikundi.
 Mratibu wa Mradi wa PS3 kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Berha Swai akizungumza.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, Kashunju Runyogote akitoa neno la shukrani.

KYERWA NA BIHARAMULO KUANZA UTEKELEZAJI AWAMU YA KWANZA YA MRADI WA PS3 MKOANI KAGERA

Kiongozi wa Timu ya Uzinduzi wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) mkoani Kagera, Abdul Kitula (kulia) akimkabidhi bahasha iliyo na majina ya Halmashauri mbili zilizopitishwa kuanza utekelezaji wa mradi wa PS3, Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Amantius Casmiri Msole mjini Bukoba leo. Halmashauri Mbili za Wilaya ya Kyerwa na Biharamulo ndizo zimechaguliwa kuanza utekelezaji wa mradi huo.Source:Father Kidevu Blog
 Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Amantius Casmiri Msole akionesha bahasha hiyo iliyo na majina.
Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Amantius Casmiri Msoleakizisoma Haklamashauri zilizo chaguliwa ambazo ni   Wilaya ya Kyerwa na Biharamuloambazo zimeonekana kuwa na uhitaji mkubwa wa kuimarisha mifumo yake kulinganisha na Halmashauri zingine sita za Karagwe, Muleba, Misenyi, Ngara, Bukoba Mji na Bukoba ambazo zitaingia awamu ya pili.
 Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Col (Mstaafu) Shaban Shaban Ilangu Lissu ambaye Wilaya yake imechaguliwa kuanza awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi wa PS3.
 Ofisa kutoka PS3 Soud Abubakar akiwasilisha sifa na vigezo vilivyo tumika kuzipata Halamashauri mbili za awali zilivyo patikana ili ziweze kuanza utekelezaji wa mradi.
 Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Kigoma wakifuatilia uwasilishaji wa taarifa kutoka Wilaya mbalimbali.
 Washiriki wakifuatilia uwasilishajki huo.
Mwakilishi wa Halmashauri ya Mji wa Bukoba, ambaye ni Mchumi Msaidizi, Rahel Mbuta akiwasilisha kazi za makundi ambazo ziliainisha Changamato na maeneo ya uboreshaji. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa