Mganga Mkuu wa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera Dkt. Peter Mkenda
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera Dkt. Peter Mkenda

Na Lydia Lugakila - Bukoba

Wananchi katika Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera wametakiwa 

kutokutunza taka katika kaya zao na maeneo mbali mbali 

ya biashara kwani kwa kufanya hivyo ni hatari kwa afya zao

 huku watakaobainika kuchukuliwa hatua za kisheria.

Kauli hiyo imetolewa na Mganga Mkuu wa Manispaa ya 

Bukoba Mkoani Kagera Dkt. Peter Mkenda wakati 

Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake 

waliotaka kujua masuala mbali mbali yahusuyo afya 

ndani ya Manispaa hiyo.

Mkenda amesema Manispaa hiyo imeweka utaratibu mzuri

 wa ukusanyaji wa taka katika mitaa ambapo magari yanapaswa 

kuzoa taka licha ya wananchi kutokutoa taka hizo kwa wakati.