KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI AWAOMBA WANANCHI WANAOISHI MIPAKANI KUTOA TAARIFA ZA WAHAMIAJI HARAMU KWENYE VYOMBO VYA DOLA


Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala wa kwanza kutoka kushoto akikagua vichochoro vinavyotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini katika kijiji cha Mugulika Kata ya Bwerenyange wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera. Kamishna Jenerali yuko mkoa wa Kagera kujionea shughuli zinazotekelezwa na Idara yake mkoani humo.
Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala wa kwanza kutoka kushoto akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Karagwe mkoa wa Kagera Godfrey Mheluka watatu kutoka kulia katika kijiji cha Muguluka Kata ya Bwerenyange wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera.Kamishna Jenerali huyo amefanya ziara katika Vipenyo vinavyotumiwa na wahamiaji haramu kutoka nchini nyingine kuingia Tanzania.
Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala wa nne kutoka kulia akiwa katika Mkutano wa Hadhara na baadhi ya Wananchi (hawapo pichani) wa Kijiji cha Muguluka Kata ya Bwerenyange wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera.Kamishna Jenerali huyo amefanya ziara katika Vipenyo vinavyotumiwa na wahamiaji haramu kutoka nchini nyingine kuingia Tanzania.
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Muguluka Kata ya Bwerenyange wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala katika Mkutano wa Hadhara baina ya wanakijiji hao na Ujumbe huo wa Idara ya Uhamiaji kutoka Makao Makuu ambapo katika Mkutano huo Dk. Makakala alitoa wito kwa wanakijiji hao kutowahifadhi wahamiaji haramu kwenye makazi yao sambamba na kuwataka kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola pale wanapogundua kuna mgeni asiyeeleweka na wanamtilia mashaka kwenye makazi yao.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

VPL: KAGERA SUGAR 1 vs 1 RUVU SHOOTING, VENANCE LUDOVIC AOKOA JAHAZI KAITABA


Kipindi cha pili Kagera Sugar waliliandama mara kwa mara Lango la Timu ya Ruvu Shooting na huku Ruvu wakiwa pungufu 10 uwanjani.
Patashika kwenye lango la Timu ya Ruvu Shooting.
Kikosi cha Timu ya Kagera Sugar kilichoanza leo dhidi ya Timu ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba leo hii kwenye Mchezo  wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara.
Kikosi cha Timu ya Ruvu Shooting kilichoanza leo dhidi ya Timu ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba leo hii kwenye Mchezo wa pili wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara.


Na Faustine Ruta, Bukoba.

Timu ya soka ya Kagera sugar imelazimisha sare ya kufungana bao 1 kwa 1 na timu ya soka ya Ruvu shooting katika mzunguko wa Ligi kuu Vodacom Tanzania bara ikiwa ni mzunguko wa kwanza tangu ligi imeanza mwezi uliopita mchezo ambao umepigwa katika uwanja wa nyumbani wa Kaitaba Bukoba Mjini.

Ligi kuu Vodacom Tanzania bara timu ya kagera sugar kwa mara ya kwanza katika mzunguko huo ulioanza August 26 kagera sugar ilifungwa na Mbao Fc ya Jijini Mwanza bao 1 kwa 0 huku Ruvu shooting  ikifungua Dimba vibaya kwa kupigwa na timu ya Simba Sc bao 7 kwa 0 ambapo timu zote mpaka sasa  zina Alama sawa ya  moja moja.

Katika mchezo huo ulichezeshwa na mwamuzi Shomari Lawi ulianza kwa saa kumi za jioni huku wachezaji wa kagera sugar wakianza mchezo huo wakiwa wamepoa na timu ya ruvu shutingi wakianza kwa mashambulizi makali dhidi ya Kagera Sugar

Ruvu shooting walikuwa wa kwanza kwa kufungua lango la timu ya kagera sugar kwa kujipatia goli la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wa timu hiyo Ishara Juma dakika 16.

Licha ya timu ya Ruvu shooting kuwa wa kwanza kupata bao 1 kipindi cha kwanza pia ilikuwa ya kwanza mchezaji wake namba 13 George Wawa kupewa kadi nyekundu muda mfupi baada ya kumfanyia rafu mbaya Mchezaji wa Kagera Sugar V. Ludovick aliyeingia kipindi cha pili cha mchezo huo. 


Dakika ya 75 kagera sugar wamepata fursa ya kusawazisha kupitia kwa mchezaji huyo huyo  Venance Ludovick na mtanange kumalizika kwa kwa sare ya bao 1-1.

RATIBA MPYA LIGI KUU YA VODACOM

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


Kikosi kazi, kilichopewa kazi maalumu ya kupitia upya Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), kimemaliza majukumu yake na sasa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawatangaza ratiba mpya.

Kwa mujibu wa ratiba mpya, baada ya michezo ya Agosti 26 na 27, Ligi Kuu ya Vodacom kwa sasa itaendelea Septemba 9 na 10 kama ambavyo inajionyesha kwenye kiambatanisho.

KAGERA YETU INAWATAKIA EID NJEMA


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa