Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya watu 11 ajali ya Kagera


11 WAFARIKI KATIKA AJALI KAGERA


Na Ripota wa Globu ya Jamii Kagera.

WATU 11 wamefariki Dunia na wengine sita kujeruhiwa kutokana na ajali ya gari aina ya hiace kugongana na malori matatu iliyotokea mnamo majira ya saa tano usiku wa kuamkia leo,katika kijiji cha Mubigera kata ya Nyantakara wilaya ya biharamulo mkoani kagera ,wakati wakisafiri kutoka wilaya ya kibondo kuelekea kahama mkoani Shinyanga.

Mganga mkuu wa hospitali teule ya Biharamulo Dr Grasmus Sebuyoya amethibitisha kupokea miili ya watu hao wakiwa maiti na majeruhi sita na kwamba kati ya majeruhi hao wawili hali zao ni mbaya na waliofariki wa jinsia ya kiume ni saba na jinsia ya kike ni watatu

Dr Sebuyoya amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Juma Samo (25) Joseph Otieno (30), Oscar Leonard Sebastian (27), Baseke Mashinga Nyabashiki (31), Mahalulo Charles (25) na majeruhi wa sita hajafahamika kwa kuwa hajajitambua na kwamba maiti waliofia eneo la tukio ni Tisa na wawili wamefariki baada ya kufikishwa hospitalini hapo.

Awali Mwenyekiti wa kijiji cha Mubigera Bw Mapunda Kayuki amesema ajali hiyo imetokea jana majira ya Saa 11 jioni ambapo hiece ilitaka kukwepana na roli kwenye barabara ya biharamulo kwenda kahama kwenye kijiji hicho na kugongana ambapo dereva wa hiece na tingo wake ni miongoni mwa waliofariki

Bw Kayuki amesema hiece hiyo yenye  namba za usajili T.542 DKE ilikuwa ikitokea kibondo kwenda kahama ambapo maroli yaliyohusika kwenye ajali hiyo ni T.860CGS, T.103 DUJ na T.147 DUJ magari  yako chini ya usalama wa jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Agustino Olomi amesema hajakamilisha taarifa kamili ya tukio hilo ikiwa ni pamoja na kutambua majina ya waliopoteza maisha mpaka ajiridhishe na taarifa,  zitatolewa kwa umma bila kutia mashaka ili ndugu wa marehemu waweze kujua na kufuatilia kwa uhakika

WAZIRI MPINA AKAMATA KILO 65,600 ZA SAMAKI ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI MIA TATU

Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina (katikati )akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Bi Mwanaidi Mlolwa akitoa maelezo baada ya kushuhudia shehena ya samaki wachanga aina ya Sangara kilo 65600 mjini Bukoba waliokamatwa katika kisiwa cha Lubili wilayani Muleba leo.Mwenye koti ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustapha Kijuu.
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina (aliyenyanyua mikono ) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustapha Kijuu (mwenye koti) leo, nje ya ghala la kuhifadhia samaki katika ofisi ya Uvuvi mjini Bukoba mara baada ya kushuhudia shehena ya samaki wachanga aina ya Sangara kilo 65600 waliokamatwa katika kisiwa cha Lubili wilayani Muleba.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustapha Kijuu (aliyesimama) akisoma taarifa ya mkoa kuhusu sekta ya mifugo na Uvuvi kwa Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina (alikaa kulia kwake) leo, mara baada ya kufanya ziara ya ghafla leo ili kushuhudia shehena ya samaki wachanga aina ya Sangara kilo 65600 waliokamatwa katika kisiwa cha Lubili wilayani Muleba. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi nchini, Mwanaidi Mlolwa.
Sehemu ya shehena ya samaki wachanga waliokaushwa kwa chumvi aina ya Sangara kilo 65600 waliokamatwa katika kisiwa cha Lubili wilayani Muleba, wakiwa wamehifadhiwa katika ghala kwenye ofisi ya Uvuvi jijini Bukoba. Samaki hao walikaatwa kufuatia raia mwema kutoa taarifa kwa Waziri Luhaga Mpina hivi karibuni.

Mwandishi Maalum,Bukoba
…………………………………………………………………………………………………………………
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina amekamata kilo 65600 za samaki wachanga aina ya Sangara waliokaushwa kwa chumvi wenye thamani ya shilingi milioni mia tatu katika Kisiwa cha Lubili wilayani Muleba kwenye Mkoa wa Kagera baada ya wamiliki wa samaki hao kukimbia.

Akizungumza leo na Waandishi wa Habari katika Ofisi ya Kitengo cha Doria na Udhibiti wa Uvuvi wa mpakani katika Mkoa wa Kagera, Mpina amesema tukio la kukamatwa kwa samaki hao lilifanikiwa baada ya yeye kupata taarifa kutoka kwa raia mwema ambapo aliagiza mamlaka za Wilaya ya Muleba kufuatilia kwa karibu hatimaye kuwakuta samaki hao wakiwa wameanikwa chini katika kisiwa hicho.

Waziri Mpina alisema Sheria ya Uvuvi namba 22 ya Mwaka 2003 na Kanuni zake za mwaka 2009 kifungu cha 90(1) inataka samaki
wanaovuliwa waandaliwe katika mazingira yanayokidhi vigezo vya usalama  kwa mlaji na kwamba ni kosa kisheria kuwavua au kuchakata samaki aina ya Sangara walio chini ya sentimeta 50 kwa kuwa ni wachanga na sentimita 25kwa Samaki aina ya Sato. Pia sentimita 85 kwa Sangara kwa kuwa ni wazazi wanaotakiwa kundelea kuzaa.

Aidha Waziri aliongeza kwamba Sheria hiyo imetoa mamlaka kwa watendaji wa Serikali kutaifisha mali zote zilitumika katika uvuvi haramu kupitia kifungu cha 37(a) (ii) na (iii) pamoja na Sheria ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu namba 29 ya mwaka 1994.

Waziri Mpina ameagiza watendaji kufuata taratibu zote za kisheria ili samaki hao wauzwe kwa njia ya mnada na mapato hayo yaingie Serikalini mara moja.Aidha aliwaonya wafanyabiashara na wavuvi kuachana na uvuvi haramu kwa kuwa ni kuhujumu raslimali za taifa ambazo zingetumika kwa kizazi cha sasa na baadaye.

“Mfanyabiashara yoyote wa samaki na mazao yake anayetaka kufilisika na kutafuta matatizo katika maisha yake aendelee na biashara ya uvuvi haramu”alisisitiza Mpina

Kufuatia tukio hili, Waziri Mpina amewapa wiki mbili wafanyabiashara na wasafirishaji wote wa samaki na mazao yake waliopewa
leseni ya ya kufanya biashara hiyo kwa mwaka 2018 kuleta cheti cha uthibitisho cha ulipaji kodi ambapo amesema kama watashindwa
kufanya hivyo hawataruhusiwa kufanya biashara hiyo.

Alisema kuanzia sasa wafanyabiashara wote wote wataruhusiwa kupata leseni hiyo baada ya kuwasilisha cheti cha uthibitisho wa ulipaji kodi, cheti cha usajili wa kampuni na mahesabu ya kibiashara yaliyohakikiwa ili kuepuka utaratibu wa sasa ambao unatoa mwanya kwa mawakala wa ndani na nje ya nchi kujiingiza katika biashara hiyo kinyemela na kuikosesha Serikali mapato kwa kukwepa kulipa kodi
mbalimbali.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustapha Kijuu alisema Serikali itahakikisha kwamba uvuvi haramu unakuwa historia katika Mkoa wa Kagera na kuwataka wananchi kuwafichua wavuvi haramu ili vyombo vya Serikali viwakamate na kuwafikisha katika mikondo ya sheria.

Alisema sekta ya uvuvi inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuinua hali ya uchumi kwenye mkoa wake na taifa kwa ujumla kama wadau wote watashiriki kikamilifu katika vita dhidi ya uvuvi haramu ambapo alisema jumla ya wananchi 26,272 wameajiriwa kutokana na shughuli za uvuvi katika mkoa huo.

Alisema mkoa utaendelea na kupambana na uvuvi haramu ambapo kwa mwaka 2016/17 jumla ya doria 65 zilifanyika na kuwezesha kukamatwa kwa makokoro ya Sangara 422, nyavu ndogo za dagaa 57,nyavu za timba 3,231, nyavu za makila 14,141, ndoano 711, katuli 16,mitumbwi 133 samaki wachanga kilo 5,621 na watuhumiwa 86.

Hata hivyo Mkuu huyo alisema katika kuongeza uzalishaji wa samaki jumla ya mabwawa 584 yamechimbwa kwa mwaka 2016/2017 kutoka mabwawa 181 mwaka 2005/2006 sawa na ongezeko la mabwawa 403.

Kwa upande mwingine Mkuu wa Mkoa alisema hivi karibuni Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ngara ilikamata gari lenye namba za uasajili T 614 CLQ aina ya Mitsubishi Canter likiwa limepakia samaki kilo 2,000 aina ya Sangara na kilo 530 wa aina ya Sato kwenye mpaka wa Murusagamba wilayani Ngara.

Alisema Afisa wa Kitengo cha Doria na Udhibiti wa Uvuvi wa mpakani katika Mkoa wa Kagera bwana Ayoub Ngoma na dereva wa gari hilo Ayoub Sanga walishikiliwa na polisi kwa hatua za kisheria kwa tuhuma za kushiriki
katika utoroshaji wa samaki wenye kilo 2530 kwenda nchini Burundi zenye thamani ya shilingi 20,850,000/= ambapo Ngoma ameshasimamishwa kazi kupisha uchunguzi.

Pia Mshauri wa Uvuvi wa Mkuu wa Mkoa, Efrazi Mkama na maafisa Uvuvi wa Halmashauri ya Muleba Wilfred Tibendelana na Maengo Nchimani na Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba vijijini Renus Ruhuzi wanaendelea kuripoti katika kituo cha polisi Bukoba kwa mahojiano ya kisheria juu ya utoroshwaji wa samaki hao.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Mwanaidi Mlolwa alisema Serikali ina mkono mrefu na kwamba hakuna mtu atakayebaki salama iwapo atajihusisha na uvuvi haramu.

Aidha alisema maafisa uvuvi wanawajibu wa kuhifadhi na kutunza takwimu mbalimbali za sekta ya uvuvi ili kutoa picha halisi ya jinsi sekta inavyochangia katika uchumi wa nchi kwa ujumla.

“Kimsingi sekta ya uvuvi ina mchango mkubwa katika uchumi wa
nchi yetu lakini tatizo kubwa ni ukosefu wa takwimu sahihi

KATIBU MKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI (MIFUGO) DK MARIA MASHINGO AWATAKA WAFUGAJI KUHAKIKISHA IFIKAPO JANUARI 31 MIFUGO YOTE NCHINI IWE IMEPIGWA CHAPA


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Maria Mashingo akipiga chapa ng’ombe katika Kijiji cha Igalula Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi leo alipokwenda kuhamasisha zoezi la upigaji na kuwataka wafugaji kuhakikisha mifugo yote inapigwa chapa ifikapo Januari 31 mwaka huu.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo) Dk. Maria Mashingo akiwaonesha wafugaji sehemu sahihi ambayo ng’ombe anatakiwa kupigwa chapa ili kuepuka kuiraribu ngozi baada ya kushiriki zoezi la upigaji chapa katika Kijiji cha Igalula wilayani Tanganyika mkoani Katavi leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Maria Mashingo akipiga chapa ng’ombe katika Kijiji cha Igalula Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi mapema leo alipokwenda kuhamasisha zoezi la upigaji na kuwataka wafugaji kuhakikisha mifugo yote inapigwa chapa ifikapo Januari 31 mwaka huu.



Na Kumbuka Ndatta, WMUV

KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dk. Maria Mashingo amewataka wafugaji kuhakikisha wamekamilisha zoezi la upigaji chapa mifugo yao kabla ya muda ulioongezwa na Serikali wa hadi Januari 31 mwaka huu kwani baada muda huo kupita haijulikani Serikali itaamua nini kuhusu mifugo itakayokuwa haijapigwa chapa.

Akizungumza wakati akishiriki zoezi la upigaji chapa mifugo katika Kijiji cha Igalula Kata ya Mpanda ndogo Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, Dk. Mashingo alisema zoezi hilo la upigaji chapa linatekelezwa kwa mujibu wa Sheria ya utambuzi ,usajili na ufuatiliaji wa mifugo Na. 12 ya Mwaka 2010 .

Dk. Mashingo alisema upigaji chapa umelenga kudhibiti magonjwa ya mifugo,wizi wa mifugo, uimarishaji usalama wa afya na mazao ya mifugo sambamba na kudhibiti usafirishaji na uhamaji wa mifugo kiholela na kuimarisha biashara ya mifugo na mazao yake kitaifa na kimataifa.

"Wafugaji hakikisheni mifugo yenu yote inapigwa chapa kwani baada ya Januari 31 mwaka huu hatujui Serikali itaamua nini kwa mifugo itakayokuwa haijapigwa chapa "alisema.

Dk. Mashingo alisema pamoja nia njema ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuwatetea wafugaji wanaofanyiwa vitendo vya uonevu na mamlaka nyingine za Serikali pia aliwahimiza kutii sheria za nchi kwa kutoingiza mifugo yao kwenye maeneo yasiyoruhusiwa kwa mujibu wa sheria.

Pia aliwakumbusha wafugaji kutambua kuwa rasilimali ya mifugo waliyonayo ina thamani kubwa na kwamba wao pia ni sehemu ya wawekezaji hivyo ni vyema wakatengeza miundombinu bora kwa ajili ya mifugo yao kuliko kuisubiri Serikali pekee kujenga miundombinu hiyo.

“Wafugaji ni wawekezaji muhimu sana katika nchi yetu kwani kama wasingekuwepo nchi ingelazimika kuagiza mazao ya mifugo kutoka nje ya nchi na tungelazmika kutumia sh. trioni 17 kwa mwaka”alisema Dk. Mashingo.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Cresencia Joseph amemweleza Dk. Mashingo kuwa mkoa huo unajumla ya ng'ombe 570,758 ambapo kati ya hao 423,767 wameshapigwa chapa.
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa