Mradi wa Umeme Vijijini (REA III) kufika Vijiji vyote nchini


Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kwikuba kuhusiana na Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akipokelewa na Mwenyekiti wa kijiji cha Kwikuba, Kamunyiro Kwibega.

Baadhi ya wananchi wakiagana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) mara baada ya kumaliza kuzungumza nao
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).
Serikali imesema vijiji vyote ambavyo havikufikishiwa huduma ya nishati ya umeme vitapata huduma hiyo kupitia Mradi mkubwa wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III).

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo katika ziara yake katika kijiji cha Kwikuba, Mkoani Mara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili (REA II) ambao unamalizika.

Katika maeneo mbalimbali aliyotembelea Waziri Muhongo alielezwa kuwa vijiji vya ndani havina umeme kwani umeme umeishia kwenye vijiji vilivyopo katika barabara kubwa na kwenye senta za biashara.

Waziri Muhongo alisema Serikali inatambua vijiji ambavyo havikufikishiwa huduma husika na hivyo aliwaasa wananchi katika vijiji hivyo kuwa na subira kwani lengo la Serikali ni kuhakikisha ndani ya miaka 10 vijiji vyote nchini view vimefikiwa na umeme.

Alisema Mradi huo wa REA III umetengewa zaidi ya trilioni moja ambayo ni mara tatu zaidi ya iliyotengwa kwa Mradi wa REA II ambao unamalizika kwa kuunganisha baadhi ya vijiji.

Aliongeza kuwa sasa hivi Serikali ipo katika utaratibu wa kuwapata Wakandarasi mahiri ambao watakabidhiwa jukumu la kutekeleza mradi huo ambao alisema ni mkubwa na wa kihistoria nchini.

Aidha akizungumzia mradi huo wa REA III, Meneja wa Kanda ya Ziwa wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Amos Maganga alisema mbali na kuunganisha vijiji vyote, lakini pia mradi huo umelenga kuhakikisha unamaliza mapungufu yaliyojitokeza katika REA II.

Alisema katika utekelezaji wa mradi wa REA II kuna mapungufu yaliyojitokeza kwa sababu mbalimbali ikiwemo kutokuwa na wigo mpana na hivyo kusababisha baadhi ya vijiji kurukwa na vingine kutofikiwa kabisa na vilevile uhaba wa baadhi ya vifaa katika maeneo mbalimbali.

Aliwaasa wananchi ambao vijiji vyao havijafikishiwa huduma ya nishati ya umeme kuwa na subira kwani mradi mkubwa wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) hautaacha kijiji.

KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TAIFA SHAKA AFANYA ZIARA WILAYANI NGARA MKOA WA KAGERA NA KUZINDUA MIRADI MBALIMBALI YA UMOJA HUO

  Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC)akizungumza na
Wajumbe wa Baraza la UVCCM pamoja na Wajumbe wa Sekretariet ya CCM Wilayani
Ngara Katika  Kikao Cha Ndani Kilicho Fanyika katika Ukumbi wa Engubenako
Wilayani Ngara.
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akiwasili katika
Kijiji Cha BENACO Wilayani Ngara, Shaka yupo  kwa ziara ya kuimarisha uhai
wa chama, kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya
CCM 2015_2020
 Mwenyekiti wa uvccm Mkoa wa Kagera Bw. Yahya Kateme akizungumza
kumkaribisha Ndg: Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka
Kuzungumza na Wajumbe wa Baraza la UVCCM pamoja na Wajumbe wa Sekretariet
ya CCM Wilayani Ngara
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC)akizungumza na
Wajumbe wa Baraza la UVCCM pamoja na Wajumbe wa Sekretariet ya CCM Wilayani
Ngara Katika  Kikao Cha Ndani Kilicho Fanyika katika Ukumbi wa Engubenako
Wilayani Ngara
 :Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizindua Mradi wa
kikundi cha Vijana wajasiliamali cha Ufugaji wa Nyuki na Shamba la Upandaji
wa Miti katika kijiji cha Nyaruku Wilayani Ngara.
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akikagua Mradi
wa Usambazaji wa Umeme Vijijini katika kijiji cha Nyankenda ikiwa ni
Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2015_2020
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akikagua
Ukamilishaji wa Agizo la  Utengenezaji wa Madawati  katika Shule ya Msingi
Rulenge Jinsi lilivyo Kamilika kama alivyotoa agizo Mhe:Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akimkabidhi
mmoja kati ya Wazee 25 waliopokea Vyeti Vya Matibabu ya bure kwa wazee
katika kijiji cha kijiji cha Mumiramila Wilayani Ngara.
 Mwandishi wa Gazeti la Uhuru Bw.Antari Sangali pamoja na wazee wakijiji
cha Mumilamila Wilayani Ngara wakimsikiliza kwa makini Kaimu Katibu Mkuu
UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC)alipo kua akigawa Vyeti kwaajili ya
Matibabu ya Bure kwa wazee.
:Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC) alipo zindua
Mradi wa Shamba la Uvccm wilayani Ngara kwa ajili ya Shughuli Mbali mbali
za kilimo kwa Vijana Wilayani humo ikiwa ni Utekelezaji wa agizo lake
alilotoa kwa Makatibu wote kuandaa miradi Mbali mbali ili kukwamua Vijana
kiuchumi kama kauli Mbiu yake isemayo'' SIASA NA UCHUMI''(picha na woinde Shizza.

RAIS DKT MAGUFULI AMUAPISHA KATIBU TAWALA WA MKOA WA KAGERA (RAS) KAMISHNA DIWANI ATHUMANI LEO IKULU DAR ES SALAAM

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishna Diwani Athumani kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera (RAS) Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 22, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na  Kamishna Diwani Athumani pamoja na viongozi waandamizi wa serikali na vyombo vya ulinzi na usalama umma   baada ya Kamishna Diwani kuapishwa  kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera (RAs) Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 22, 2016.

PICHA NA IKULU

OFISI YA WAZIRI MKUU YAPOKEA MIFUKO 1000 YA SERUJI KWA AJILI YA WAATHIRIKA WA MAAFA KAGERA.

 Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jenerali Mbazi Msuya (kulia) akitoa neno la shukrani kwa Meneja Mkuu wa Kampuni ya Amsons-Camel Bw. Salim A.Salim baada ya kukabidhi msaada wa Mifuko 1000 ya Seruji kwa ajili ya waathirika wa Tetemeko la Ardhi la Kagera Novemba 09, 2016 katika Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es Salaam.
 Meneja Mkuu wa Kampuni ya Camel Bw. Salim A. Salim (kushoto) akitoa maelezo ya msaada wa mifuko 1000 ya Seruji kwa Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jenerali Mbazi Msuya (kulia) walipofika katika Ofisi yake Dar es Salaam Novemba 09, 2016.
 Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jenerali Mbazi Msuya (katikati) akipeana mkono wa shukrani na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Camel Bw. Salim A. Salim wakati wa kuwasilisha msaada wao wa mifuko 1000 ya Seruji kwa waathirika wa maafa Kagera, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Amsons-Camal Bw. Ghalib H. Ghalib.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria katika zoezi la makabidhiano ya mifuko 1000 ya seruji kwa ajili ya waathirika wa maafa mkoani Kagera kutoka Kampuni ya CAMEL katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SERIKALI YAANZA MCHAKATO WA UJENZI WA RELI YA KATI KWA KIWANGO CHA KIMATAIFA (STANDARD GAUGE)


Na Frank Shija, MAELEZO
Serikali ya Awamu ya Tano ndani ya mwaka mmoja imeanza mipango ya kuboresha usafiri wa reli ya Kati kwa kuijenga kwa kiwango cha kimataifa yaani Standard Gauge. Usafiri huu utaongeza fursa za kiuchumi kwani mazao ya chakula na biashara toka mikoa ya Kigoma, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Tabora na Singida kuelekea Dar es Salaam yatasafirishwa kwa haraka.

Reli hii itarahisisha pia usafiri wa abiria wa mikoa ya Kanda ya Ziwa, Kati na Magharibi. Usafiri wa treni kwa kiwango kikubwa huwa ni wa uhakika na wa gharama nafuu. Hivyo ujenzi wa reli kwa Standard Gauge uteleta ukombozi mkubwa wa kiuchumi kwa watu wa maeneo hayo na Taifa kwa ujumla.

Kwa kipindi kirefu huduma ya usafiri wa treni kupitia Reli ya Kati (Central Line Railway) imekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa mkoa wa Kigoma na maeneo ya Kanda ya ziwa na nchi za jirani zikiwemo Burundi, Rwanda, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Historia inaonesha kuwa Reli ya Kati kama inavyojulikana sasa ilijengwa kati ya mwaka 1905 hadi 1914 wakati huo ikiitwa Reli ya Tanganyika kwa kuwa ilikuwa ikielekea Mkoani Kigoma ambako Ziwa Tanganyika linapatikana.

Kutokana na umuhimu wake katika kukuza uchumi kupitia usafirishaji bidhaa na huduma mbalimbali ndani na nje ya Tanzania, Katika mwaka wa fedha 2016/2017 Serikali imeamua kuja na mpango kabambe wa kuifanyia maboresho miundombinu ya  reli hiyo ili iweze kwenda na wakati na kasi ya ukuaji wa uchumi.

Mpango huo unahusisha ujenzi wa mtandao wa Reli mpya ya Kati katika Viwango vya Kimataifa (Standard Gauge 80’) ili kuendana na kasi ya ongezeko la mizigo.

Msemaji wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Bw. William Budoya anaeleza kuwa gharama iliyokaidiriwa kutumika kukamilisha mradi huo ni Dola za Kimarekani Bilioni 7.6 ambazo ni sawa na shilingi za Kitanzania Trilioni 16.

Fedha hizo zitatumika kugharamia ujenzi wa Kilomita 2,561 za reli kwa kiwango cha Kimataifa . Ili kufanikisha mradi huo Serikali imepata ufadhili kutoka Benki ya Exim ya China ambayo imekubali kutoa mkopo wenye masharti nafuu.

Aidha, katika kuhakikisha kuwa ujenzi huo unafanikiwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anakutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Exim ya China Bw. Liu Liang Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yao Rais wa benki hiyo anamuhakikishia Rais Dkt. John Magufuli kuwa Benki hiyo iko tayari kutoa kiasi hicho cha fedha ili kufanikisha ujenzi wa kilometa 2,190 za reli. Pia anamuhakikishia Rais kuwa Benki hiyo itashirikiana na Tanzania katika kubadilishana uzoefu na utaalamu katika ujenzi na uendeshaji wa reli hiyo.
Akiuzungumzia ujenzi wa Reli hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli anabainisha kuwa kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kuinua uchumi wa Tanzania na nchi jirani zisizopakana na bahari zikiwemo Uganda, Rwanda, Burundi, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Anasema reli hiyo mpya itakua tofauti na inayotumika sasa kutokana na uwezo  wake wa kuhimili usafirishaji wa mizigo mingi kwa kuwa inajengwa kwa kiwango cha Kimataifa "Standard Gauge railway " na itaanzia Dar es Salaam Mpaka Kigoma, kupitia Tabora, Mwanza,Isaka hadi Rusumo; Kaliua -Mpanda -Karema na Uvinza -Musongati nchini Burundi.

Katika ufafanuzi alioutoa hivi karibuni kuhusu ujenzi wa reli hiyo wakati wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi mjini Dodoma hivi karibuni, Rais John Pombe Magufuli alisema tayari mchakato wa ujenzi wa reli hiyo umeanza kwa kutangaza zabuni ili kumpata mkandarasi atakaye jenga Reli hiyo.

Anasema sambamba na kazi hiyo Serikali itakarabati matawi ya reli ya kati sehemu ya Kaliua-Mpanda ili kuboresha ufanisi wake, kwa kutenga Sh. bilioni 5.5 za ajili ya usanifu.

Aidha, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano uliowasilishwa bungeni Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango ,Dk. Philip Mpango unaeleza kuwa Serikali imejipanga kufanya usanifu na ujenzi wa madaraja 16 kati ya 28 yaliyochakaa kati ya Dar es Salaam na Tabora.

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Servaciaus Likwelile akizungumza mara baada ya utiaji saini wa makubaliano wa ujenzi wa reli hiyo kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Naibu Meneja Mikopo Nafuu wa Benki ya Exim ya China Bw. Zhu Ying anasema kuwa Dola za Kimarekani bilioni 7.6 ambazo ni sawa na Shilingi Trilioni 16 zitatumika kutekeleza mradi huo.
 
Dkt. Likwelile anasema hatua hiyo inawezesha kuanza kwa kazi ya upembuzi yakinifu, usanifu na uundwaji wa timu za pamoja kuanza kuainisha mahitaji halisi ya ujenzi wa mradi huo.
 
Anasema mradi huu umekuja wakati muafaka kutokana na kwamba reli iliyopo sasa ambayo ni ya Kiwango cha "meter gauge” haina uwezo mkubwa katika ubebaji wake wa mizigo, hata baada ya kufanyiwa ukarabati.
Kwa mwaka ni tani Milioni 5 za mizigo ndizo zinaweza kupitishwa na reli ya sasa, ambazo haziwezi kukabili mahitaji ya mizigo ya Kanda hii ambayo itafikia tani Milioni 30 ifikapo mwaka 2025.

Kutokana na uhitaji huo wa kukabiliana na uongezaji wa mizigo kwa kujenga uwezo wa kuihudumia kwa kuwa na reli ambayo pamoja na kuwa na uwezo wa kubeba mizigo hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba abiria wengi zaidi na kwa starehe lakini pia kwa kasi ya spidi ya wastani wa kilometa 100 kwa saa hivyo kuwezesha abiria kufika haraka zaidi sehemu wanazokwenda.

Pia wakati wa ujenzi wa reli hiyo watanzania takribani 300,000 watapata ajira kutokana na kushiriki katika ujenzi wa reli hiyo.
Mwisho.

PLATINUM CREDIT TANZANIA YACHANGIA MAAFA YA KAGERA




Afisa masoko Platinum Credit Tanzania, Gideon Lufunyo (kushoto) akikabidhi msaada wa mifuko 300 ya saruji ambayo ni sawa na tani 15 kwa Mkuu wa mkoa Kagera, Salum Kijuu ikiwa ni msaada wa taasisi hiyo kwa waathirika wa tetemekonla Ardhi mkoani humo.
Kampuni ya Platnum Credit Tanzania Leo imekabidhi msaada wa mifuko 300 ya sumenti kwa mkuu wa mkoa wa Bukoba Salum Kajuu kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibuni.

                   
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Jana ofisa masomo wa kampuni hiyo Gideon Lufunyo alisema  tetemeko hilo limeleta madhara mkubwa ambayo yamewagusa n kwamba nia yao ni kuona shule kinaendelea na ratiba ya kawaida ili watoto wasikose elimu.

STAMICO YACHANGIA MILIONI 20 MAAFA YA TETEMEKO LA ARDHI KAGERA

01
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza na wawakilishi wa Taasisi mashirika mbalimbali (Hawapo pichani) zilizochangia wanananchi wa Bukoba Mkoani Kagera waliopatwa na maafa ya tetemeko la ArdhiSeptemba 10 mwaka huu ambapo Waziri Mkuu amepokea fedha taslimu sh. milioni 25.62 pamoja na nguo zenye thamani ya sh. milioni mbili kutoka kwa wadau mbalimbali, Huku Shirika la Madini la STAMICO likichangia jumla ya shilingi milioni 20 katika fedha hizo.
Fedha hizo jumla ya shilingi milioni 20 zilizotolewa na STAMICO ni michango ya pamoja iliyotolewa na kampuni tanzu za KTCL, SAMIGOLD na STAMICO yenyewe.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika hafla fupi iliyofanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es salaam leo.
(PICHA NA JOHN BUKUKU WA FULLSHANGWE-MAGOGONI DAR ES SALAAM)
1
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini nchini STAMICO Bi.Zena Kongoi akizungumza kabla ya kukabidhi msaada wao wa shilingi milioni 20 kwa Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa kulia kwake ni Mahende Michael Peter Mwanasheria Mkuu wa STAMIGOLD na waliosimama nyuma kutoka kushoto ni Raymond Rwehumbiza Mratibu wa mradi Ununuzi wa Madini ya bati KTCL uliopo Kyerwa Mkoa wa Kagera, Alex Rutagwelela Kaimu Mkurugenzi wa Uchorongaji STAMICO , Beatrice Musa Lupi Mhasibu Mkuu STAMICO na Koleta Njelekela Meneja Masoko na Uhusiano kwa Umma STAMICO.
2
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini nchini STAMICO Bi.Zena Kongoi akimuonyesha Waziri Mkuu Vocha ya malipo yaliyofanywa kwenye akaunti ya kuchangia wahanga wa Tetemeko la Ardhi Kagera kabla ya kukabidhi rasmi kwa waziri mkuu kutoka kushoto ni Mahende Michael Peter Mwanasheria na Mkuu wa Kitengo cha Sheria STAMICO na Koleta Njelekela Meneja Masoko na Uhusiano kwa Umma STAMICO.
3
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini nchini STAMICO Bi.Zena Kongoi akikabidhi vocha hiyo kwa Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa kutoka kushoto ni Raymond Rwehumbiza Mratibu wa Ununuzi wa Madini ya KTCL Kyerwa Mkoa wa Kagera, Mahende Michael Peter Mwanasheria na Mkuu wa Kitengo cha Sheria STAMICO na Koleta Njelekela Meneja Masoko na Uhusiano kwa Umma STAMICO.
4
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akipiga picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO Bi. Zena Kongoi na ujumbe wake alioongozana nao kutoka shirika hilo.
5 7
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Kassim Majaliwa aki akizungumza jambo na Bi. Koleta Njelekela Meneja Masoko na Uhusiano kwa Umma STAMICO mara baada ya makabidhiano hayo.
8
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kassim Majaliwa na wageni mbalimbali waliofika ofisini kwake kutoa msaada kwa ajili ya wahanga wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera wakimkubuka Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikiwa ni maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo chake miaka 17 iliyopita.

Waziri mkuu apokea misaada ya waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera


Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea msaada wa mablanketi kutoka kwa Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida ukiwa ni msaada kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.Kulia  ni Mwakilishi Mkuu wa Shirika la JICA nchini Toshio Nagase.


Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea  hundi ya shilingi milioni 6.7m kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi Taasisi ya wakaguzi wa ndani wa Serikali na kampuni Binafsi Bw.Richard Magongo leo Jijini Dar es Salaam ukiwa ni msaada kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.


Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea pesa taslimu shilingi milioni 2 kutoka kwa Mwenyekiti wa Magereji Tegeta Bw.Lenard Mwanjela ukiwa ni msaada kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.


Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 325 kutoka kwa wawakilishi wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya ACACIA  ikiwa ni kwa ajili ya  waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.


Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea hundi  ya shilingi milioni 41.5 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa  Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) Bw.Ayoub Ryoba ikiwa ni kutokana na harambee iliyofanywa na Shirika la Utangazaji  Tanzania(TBC) kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.


Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa  akipokea moja ya misaada kutoka kwa Katibu wa Jumuiya ya wafanyabiashara wa kariakoo Bw.Abdallah Mwinyi ambao wametoa vifaa vyenye thamani ya milioni 60 ikiwa ni kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.
Picha na Daudi Manongi
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa