Home »
» Waziri mkuu apokea misaada ya waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera
Waziri mkuu apokea misaada ya waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera
|
Waziri Mkuu wa
Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea msaada wa mablanketi kutoka kwa
Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida ukiwa ni msaada kwa ajili ya waathirika
wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.Kulia ni Mwakilishi Mkuu wa Shirika la JICA nchini
Toshio Nagase.
|
|
Waziri Mkuu wa
Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea
hundi ya shilingi milioni 6.7m kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi Taasisi ya
wakaguzi wa ndani wa Serikali na kampuni Binafsi Bw.Richard Magongo leo Jijini
Dar es Salaam ukiwa ni msaada kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi
Mkoani Kagera.
|
|
Waziri Mkuu wa
Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea pesa taslimu shilingi milioni 2
kutoka kwa Mwenyekiti wa Magereji Tegeta Bw.Lenard Mwanjela ukiwa ni msaada kwa
ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.
|
|
Waziri Mkuu wa
Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea mfano wa hundi ya shilingi
milioni 325 kutoka kwa wawakilishi wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya ACACIA ikiwa ni kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.
|
|
Waziri Mkuu wa
Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 41.5 kutoka kwa Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Utangazaji
Tanzania(TBC) Bw.Ayoub Ryoba ikiwa ni kutokana na harambee iliyofanywa na Shirika
la Utangazaji Tanzania(TBC) kwa ajili ya
kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
|
|
Waziri Mkuu wa
Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa
akipokea moja ya misaada kutoka kwa Katibu wa Jumuiya ya wafanyabiashara
wa kariakoo Bw.Abdallah Mwinyi ambao wametoa vifaa vyenye thamani ya milioni 60
ikiwa ni kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.
|
Picha na Daudi Manongi
0 comments:
Post a Comment