Biharamulo kujenga madaraja matatu

HALMASHAURI ya wilaya Biharamulo mkoani Kagera imekusudia kujenga madaraja kwenye mito mitatu katika kata ya Rusahunga ambayo imekuwa kero kubwa hasa kwenye kipindi cha mvua ambapo baadhi ya watoto wa shule hushindwa kuhudhuria masomo yao pindi mito hiyo inapojaa maji.

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Nassib Mmbagga amesema hayo jana kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani cha kujadili taarifa ya robo mwaka ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Akijibu swali la diwani wa kata ya Rusahunga, Amoni Mizengo aliyetaka kupata ufafanuzi wa mkakati wa halmashuri wa kujenga madaraja kwenye mito hiyo,Mmbagga amesema utekelezaji wa miradi hiyo utaaanza ndani ya siku 14 zijazo.

 Amefafanua kuwa Ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kabla ya kipindi cha mvua kubwa kuanza mkurugenzi huyo amewaagiza wataalamu wa idara ya ujenzi kufika katika maeneo ya mito hiyo kwa muda wa siku 14 ili ujenzi huo ukamilike kama ulivyokusudiwa.

Mito inayodaiwa kuwa tishio kwa wakazi wa kata hiyo ambayo inakusudiwa kujengwa ni Nyamagala kwenda Nyarusenge,Nyakasenga kwenda shule ya msingi ya kijiji hicho na Nyambare kwenda Mwasu.

Awali Akizungumzia hali hiyo Diwani wa kata hiyo Mizengo(Chadema)amesema tatizo hilo hujitokeza kila mwaka kwenye kipindi cha masika kutokana na maeneo hayo kukosa madaraja baada ya barabara kukatika.

Madiwani wailalamikiwa barabara iliyozinduliwa na Rais Kikwete

BARABARA iliyozinduliwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete katika Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera imelalamikiwa na madiwani wa halmashauri hiyo kufuatia baadhi ya barabara zinazoingia katika taasisi za huduma za jamii kuharibiwa na kampuni ya Chico inayotengeneza barabara hiyo kwa kiwango cha Lami.
Madiwani Wamesema hayo katika kikao kilichofanyika leo(Jumanne) kufuatia barabara hizo kuharibiwa na hali ambayo imesbabisha wananchi wa maeneo hayo kulazimika kutembea umbali mrefu kwenda kwenye huduma za kijamii badala ya kutumia vyombo vya usafiri yakiwemo magari,na pikipiki.

Mmoja wa madiwani hao Diwani wa kata ya Rusahunga,Amon Mizengo akichangia hoja hiyo kwenye baraza la madiwani la kujadili taarifa za robo mwaka amesema hali hiyo imesababisha magari yanayopeleka huduma za kijamii kushindwa kuingia na mbaya zaidi kunapotokea mgonjwa inakuwa vigumu kumwahisha kwenye huduma ya matibabu.

Taasisi zilizoadhirika na uharibifu wa barabara hizo ni makao makuu ya tarafa,kata na kijiji cha Rusahunga ambako kuna Zahanati shule ya msingi Nyambale,Shule ya sekondari Rusahunga,tatizo ambalo limekuwepo tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Hoja hiyo ilikuja kufuatia majibu yaliyotolewa na mkurungezi wa halmashauri hiyo,Nassib Mmbagga kwamba ukarabati wa barabara hizo umeanza kutekelezwa ambapo kampuni ya Chico imeanza kuzingatia agizo la madiwani lililowahi kufikishwa pia kwenye kikao cha bodi ya barabara Taroad mkoani hapa.

Julai 26 mwaka huu rais Kikwete alizindua barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 154 inayotekelezwa na Kampuni ya Chico ambapo ambapo toka ujenzi huo uanze baadhi ya barabara zinazoelekea sehemu zingine ziriharibiwa hali ambayo imeleta usumbufu mkubwa kwa wananchi.

Serikali yaahidi kukamilisha mradi wa umeme Chato

SERIKALI kupitia wizara ya Nishati na Madini imeahidi kumaliza kero ya mgao wa umeme inayowakabili wakazi wa wilaya ya Chato mkoani Geita hali ambayo imechangia kuzorota kwa uzalishaji mali katika maeneo hayo.

Kauli hiyo ya serikali imetolewa na waziri wa Nishati na Madini Prof,Sospeter Muhongo baada ya kuahidi kufunga mashine mpya ya kufua umeme kwenye wilaya hiyo ili kuepuka adha ya mgao wa umeme unaotokana na mashine zilizoko wilaya jirani ya Biharamulo.

Prof Muhongo amesema hayo jana(JUMATATU) kwenye mkutano wa hadhara muda mfupi baada ya ombi lililotolewa na Mbunge wa jimbo la Chato,Dk John Magufuli kutokana na adha kubwa ya kukatika kwa umeme mara kwa mara hali inayodaiwa kukwamisha ukuaji wa uchumi.

Amesema serikali imekubali kutoa mashine moja kubwa itakayozalisha umeme katika wilaya hiyo na kwamba itafungwa katika wilaya hiyo badala ya kuendelea kutumia mshine zilizoko wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera.

Amesema mashine zinazotumika kufua umeme katika wilaya ya Biharamulo na Chato ni chakavu ambazo wakati zinafungwa zilikuwa tayari zimeshatumika sehemu nyingine hapa nchini.

WIVU NI NOMA: MWANAUME AKATWA ULIMI NA MKEWE-NGARA

Bw.Anord Nyabenda akionesha Ulimi wake namna ulivyokatwa kwa meno na mkewe. Imeelezwa kuwa chanzo ni wivu wa kimapenzi kati yake na mkewe. Hadi sasa mwanamke hajafika Hospitalini alikolazwa kwa matibabu ili kujulia hali mwenzake.

RAIS KIKWETE AKIWA WILAYANI MULEBA


Wananchi wa Muleba wakimshangilia Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili wilayani humo akiwa katika ziara yake ya siku sita Mkoani Kagera
Rais Kikwete akivikwa skafu na skauti baada ya kuwasili Muleba
Vikundi vya ngoma vikitumbuiza wageni
PICHA NA IKULU

ZIARA YA RAIS JAKAYA KIKWETE IKIWA INAENDELEA MKOANI KAGERA.



Rais Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Kagoma-Lusahunga katika wilayani BiharamuloRais Jakaya Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Kagoma-Lusahunga katika wilayani Biharamulo. 
Rais Kikwete akipiga picha ya kumbukumbu na wananchi wa Ngara baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo Jumamosi Julai 27, 2013Rais Kikwete akipiga picha ya kumbukumbu na wananchi wa Ngara baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo  Rais Kikwete akishiriki kupiga ngoma na kikundi cha utamaduni cha Ngara wakati wa uzinduzi wa kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo wilayani NgaraRais Kikwete akishiriki kupiga ngoma na kikundi cha utamaduni cha Ngara wakati wa uzinduzi wa kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo wilayani Ngara 



Rais Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya Kyerwa (1)Rais Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya KyerwaRais Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya Kyerwa (2)Rais Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya Kyerwa.Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete aliposimama kwa muda kuwasslimia wilayani Karagwe akielekea Rusumo kuzindua kivuko cha Ruvuvu (1)Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete aliposimama kwa muda kuwasslimia wilayani Karagwe akielekea Rusumo kuzindua kivuko cha Ruvuvu Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete aliposimama kwa muda kuwasslimia wilayani Karagwe akielekea Rusumo kuzindua kivuko cha Ruvuvu (2)Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete aliposimama kwa muda kuwasslimia wilayani Karagwe akielekea Rusumo kuzindua kivuko cha Ruvuvu Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete baada ya kuzindua  kivuko cha MV Ruvuvu  Jumamosi Julai 27, 2013 (1)Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu jana Jumamosi Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete baada ya kuzindua  kivuko cha MV Ruvuvu  Jumamosi Julai 27, 2013 (2)Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu  Kivuko cha zamani kilichokuwa kikitumiwa na wananchi wa Ngara kuvuka mto RusumoKivuko cha zamani kilichokuwa kikitumiwa na wananchi wa Ngara kuvuka mto Rusumo Kivuko kipya cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo kilichozinduliwa na Rais Kikwete Jumamosi Julai 27, 2013Kivuko kipya cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo kilichozinduliwa na Rais Kikwete Rais Kikwete akihutubia umati NgaraRais Kikwete akiongea na wananchi katika sherehe ya kuzindua mradi wa umeme vijijini katika kijiji cha Nyaishozi, Wilaya ya Karagwe Rais Jakaya Kikwete yuko mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi ya siku nane.Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa (2)Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa (3)Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya KyerwaUmati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa (4)Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa .
(PICHA NA IKULU).

RAIS KIKWETE AFUNGUA JENGO LA MAHAKAMA KUU KANDA YA BUKOBA


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua pazia kuzindua rasmi jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba leo Julai 25, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba leo Julai 25, 2013. Aliyeshika utepe ni Jaji Mkuu, Othman Chande
 Rais Kikwete akiwa katika moja ya vyumba vya mahakama hiyo
 Rais Kikwete akifuatana na Jaji Mkuu wakati akikagua jengo la mahakama hiyo
 Jaji Mkuu Othman Chande akimpa maelezo Rais Kikwete wakati wakiwa kwenye jengo la mahakama hiyo.
 Rais Jakaya Kikwete na Jaji Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wa mahakama waliohudhuria uzinduzi wa jengo hilo la mahakama. 
Picha na Ikulu

RAIS DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE AONGOZA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA KATIKA KAMBI YA KABOYA BUKOBA MKOANI KAGERA LEO.


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka ngao/sime katika mnara wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa katika kambi ya jeshi ya Kaboya, Bukoba, mkoani Kagera leo Julai 25, 2013.
 Viongozi wa dini wakisoma dua kwenye maadhimisho hayo. Pembeni ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Mohamed Ali Shein, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Jaji Mkuu Mheshimiwa Chande Othman na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Othman Makungu.
 Rais Jakaya Kikwete akitembelea makaburi ya mashujaa waliopoteza maisha wakati wa vita na Nduli Iddi Amini wa Uganda.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Wazee ambao ni sehemu ya mashujaa wetu walio hai waliohudhuria maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa katika kambi ya jeshi ya Kaboya, Bukoba, mkoani Kagera leo Julai 25, 2013.
Katika maadhimisho haya alikuwepo pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Mohamed Ali Shein, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Jaji Mkuu Mheshimiwa Chande Othman na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Othman Makungu

PICHA NA IKULU.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUTURU NA WAKAZI WA KAGERA WILAYA YA MISENYI JANA.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Kagera, baada ya kufuturu nao futari ya pamoja aliyoiandaa katika Kiwanda cha Kagera Sugar, jana Julai 24, 2013. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, Kanali Mstaafu, Issa Njiku (kushoto) ni Mmiliki wa Kiwanda cha Kagera Sugar, Nassor Seif.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Kagera Sugar, Hashim Ranner, baada ya kumalizika kwa hafla ya Futari ya pamoja na wananchi wa Mkoa wa kagera iliyofanyika katika Kiwanda cha Kagera Sugar Wilaya ya Misenyi jana Julai, 24, 2013. Katikati ni Mmiliki wa Kiwanda hicho, Nassor Seif.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkk. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya wananchi alioshiriki nao Futari ya pamoja katika Kiwanda cha Kagera Sugar Wilaya ya Misenyi Mkoa wa Kagera, baada ya kumalizika kwa hafla hiyo jana Julai 24, 2013

 Baadhi ya wananchi waumini wa dini ya Kiislamu waliohudhuria hafla ya futari ya pamoja, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akizungumza nao jana Julai, 24, 2013. 
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

UNIC YAHAMASISHA VIJANA WILAYANI KARAGWE KUJIUNGA KATIKA VILABU VYA UMOJA WA MATAIFA


IMG_0620
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akizungumza na Mkuu wa Shule ya Sekondari Ndama ya Wilayani Karagwe Mwl. Emmanuel Muganyizi kuhusiana na umuhimu wa wanfunzi wa shule yake kuanzisha Vilabu vya Umoja wa Mataifa na faida zake.
IMG_0638
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akizungumza na walimu wa shule ya Sekondari Ndama na kuwapa hamasa ya kuwa walezi wazuri wa vilabu hivyo vitavyoanzishwa shuleni hapo ikiwa ni kama somo la ziada kwa wanafunzi wao ili wasipate muda wa kushiriki matendo ya ajabu na yasiyo na maadili.
IMG_0644
Usia Nkhoma Ledama akiongozwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Ndama ya wilayani Karagwe kuelekea madarasani kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo.
IMG_0672
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akizungumza na vijana wa shule za sekondari Ndama wilayani Karagwe mkoani Kagera, kuwaelezea umuhimu wa kujiunga na vilabu vya Umoja wa Mataifa (UN Club) vinavyoanzishwa mashuleni kwa kuwa kwanza vitawasaidia kujitambua.

Amewaambia kwa vijana kama wao ambao tayari wameanzisha na kuendesha vilabu hivyo mashuleni kujiunga kwa wingi zaidi na kutawawezesha kujifunza shughuli za umoja wa mataifa duniani, kuhusishwa na mashirika mengine ya kimataifa, kushiriki katika mafunzo mbalimbali, warsha na mikutano ndani na nje ya nchi kama vile National Model UN, the Eastern Africa Model UN, the Africa Regional Model UN na mengineyo, ikiwemo kupata nafasi ya kuisaidia jamii zao kupitia program mbalimbali.

Bi. Usia pia amewafafanulia vijana kuwa katika klabu hizo wataweza kuwa na mtandao na vijana wengine kitaifa na kimataifa, kupata nafasi ya kufanya kazi za kujitolea.
IMG_0666
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Ndama wakimsikiliza kwa makini Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) Usia Nkhoma Ledama (hayupo pichani).
IMG_0677
Usia Nkhoma Ledama katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ndama pamoja na Mkurugenzi wa Radio Jamii FADECO ya wilayani Karagwe Bw, Joseph Sekiku (kushoto).
IMG_0567
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akijitambulisha kwa baadhi ya walimu wa Shule ya Sekondari Kayanga ya Wilayani Karagwe Mkoani Kagera. Kushoto mwenye suti ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Johnbosco Paul.
IMG_0580
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akikagua Maktaba ya Shule ya Sekondari Kayanga. Kulia ni Mwl. Mkuu wa Shule ya Kayanga Johnbosco Paul.
IMG_0704
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akizungumza na wazazi wa watoto wanaosoma katika shule ya sekondari ya Kayanga amewaelezea kuwa pindi watoto wao wanapojiunga na klabu za Umoja wa mataifa zilizopo mashuleni watapata elimu na uzoefu utakaotengeza thamani ya CV zao na kuzipa uzito zaidi na pia watapata ufahamu wa mambo mengi utakao wasaidia wasijiunge na vikundi visivyofaa wala kushiriki matendo ya ajabu na yasiyo na maadili.

Amewaambia wazazi hao ndani ya klabu hizo hutokea kupata tarajali, uzoefu wa kazi, na kwamba kwa kupitia klabu hizo vijana wote shule zilizopo mikoa yote ya Tanzania watakuwa na nafasi ya kuwa karibu na taratibu na kanuni za Umoja wa Mataifa.
IMG_0603
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Kayanga ya Wilayani Karagwe mkoani Kagera wakiwa mapumzikoni kuelekea kupata uji.

Picha na maelezo kwa hisani ya fullshangweblog.com

YUNA NA UNESCO YAKUSANYA MAONI YA WANANCHI WA KARAGWE KUHUSU UTEKELEZAJI WA MRADI WA AMANI NA DEMOKRASIA KWA KUSHIRIKIANA NA REDIO ZA KIJAMII (FADECO).


IMG_0073
Mshauri wa Radio Jamii kutoka UNESCO Rose Haji Mwalimu akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Dary Lwegasira alipomtembelea ofisini kwake mjini Kayanga mkoani Kagera kutambulisha mradi wa Amani na Demokrasia wenye lengo la kuhamasisha ushiriki wa jamii miongoni mwa vijana, wanawake na walemavu katika maendeleo na kudumisha amani nchini Tanzania. Mradi huo utakuwa unaratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na UNDP.
IMG_0085
Mweka hazina wa Shirikisho la Vijana la Umoja wa Mataifa (YUNA) Tanzania Bara na Visiwani Bw. Omary Hassan akifafanua jambo kuhusiana na mradi wa Amani kwa Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Dary Lwegasira (wa tatu kulia) namna utakavyoendeshwa kwa wakazi wa Wilaya yake. Kushoto ni Mkurugenzi wa Radio jamii FADECO ya Wilaya ya Karagwe Joseph Sekiku na wa pili kulia ni Mshauri wa Radio Jamii kutoka UNESCO Rose Haji Mwalimu.
IMG_0221
Picha juu na chini ni Bw. Omary Hassan akikusanya maoni ya vijana wa Chuo cha Ufundi Stadi (KDVTC) kilichopo kitongoji cha Kayanza wilayani Karagwe mkoa wa Kagera.
IMG_0182 IMG_0208
Mweka hazina wa Shirikisho la Vijana la Umoja wa Mataifa (YUNA) Tanzania Bara na Visiwani Bw. Omary Hassan na Mkurugenzi wa Radio jamii FADECO ya Wilaya ya Karagwe Joseph Sekiku (fulana ya Blue) kwenye picha ya pamoja na walimu na wanafunzi wa Chuo cha ufundi stadi (KDVTC) mara baada ya kumaliza zoezi la ukusanyaji maoni kwa wananchi wa Karagwe.
IMG_0254
Mweka hazina wa Shirikisho la Vijana la Umoja wa Mataifa (YUNA) Tanzania Bara na Visiwani Omary Hassan akizungumza na uongozi wa Perfect Education of Tourism and Institutions (PETI) kuhusiana na ukusanyaji maoni ya Utekelezaji wa Mradi wa Amani na Demokrasia Wilayani Karagwe. Kushoto ni Mkuu wa taasisi ya PETI Devotha Brassio na Makamu Mkuu wa taasisi hiyo Fravian Gedion.
IMG_0271
Bw. Omary Hassan akizungumza na wanafunzi wa Perfect Education of Tourism and Institutions (PETI) kuhusiana na utekelezaji wa mradi wa Amani ambapo vijana nao wanahusika katika kujenga Amani ya nchi kwa sababu wao ndio taifa la leo.
IMG_0295
Bw. Omary Hassan katika picha ya pamoja na uongozi wa taasisi ya PETI na baadhi ya wanafunzi wa taasisi hiyo.
IMG_0324
Mweka hazina wa Shirikisho la Vijana la Umoja wa Mataifa (YUNA) Tanzania Bara na Visiwani Bw. Omary Hassan akikusanya maoni kwa wananchi wa wilaya ya Karagwe kufanya tathmini ya utekelezaji wa mradi wa Amani na Demokrasia.
IMG_0378
Kina mama nao walihusika katika kuchangia maoni ambapo wengi wao wameomba mradi huo utakapoanza kuwepo na kipindi maalum katika radio jamii ya wilaya ya Karagwe cha kuwaelimisha waume zao kuhusu swala la unywaji Pombe kupita kiasi ambao unapelekea uvunjifu wa amani katika nyumba zao.
--
Mashirika ya UNDP na UNESCO yameanzisha mradi wa pamoja wenye lengo la kuhamasisha ushiriki wa jamii miongoni mwa vijana, wanawake na walemavu katika maendeleo na kudumisha amani nchini Tanzania.
Kama inavyojulikana haiwezekani kuwa na maendeleo bila kuwa na amani, na haiwezekani kuwa na amani bila kuwa na maendeleo.
Kwa sababu hiyo Jumuiya ya Kimataifa inatambua kuwa moja ya mikakati msingi ya kujenga amani ni kuwa na msingi thabiti wa uchumi jamii.Pia kuwezesha raia wote kuhusisha katika kutoa maamuzi ni kuweka msimamo katika maendeleo endelevu.
 
PICHA ZOTE NA 
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa