Home » » Biharamulo kujenga madaraja matatu

Biharamulo kujenga madaraja matatu

HALMASHAURI ya wilaya Biharamulo mkoani Kagera imekusudia kujenga madaraja kwenye mito mitatu katika kata ya Rusahunga ambayo imekuwa kero kubwa hasa kwenye kipindi cha mvua ambapo baadhi ya watoto wa shule hushindwa kuhudhuria masomo yao pindi mito hiyo inapojaa maji.

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Nassib Mmbagga amesema hayo jana kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani cha kujadili taarifa ya robo mwaka ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Akijibu swali la diwani wa kata ya Rusahunga, Amoni Mizengo aliyetaka kupata ufafanuzi wa mkakati wa halmashuri wa kujenga madaraja kwenye mito hiyo,Mmbagga amesema utekelezaji wa miradi hiyo utaaanza ndani ya siku 14 zijazo.

 Amefafanua kuwa Ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kabla ya kipindi cha mvua kubwa kuanza mkurugenzi huyo amewaagiza wataalamu wa idara ya ujenzi kufika katika maeneo ya mito hiyo kwa muda wa siku 14 ili ujenzi huo ukamilike kama ulivyokusudiwa.

Mito inayodaiwa kuwa tishio kwa wakazi wa kata hiyo ambayo inakusudiwa kujengwa ni Nyamagala kwenda Nyarusenge,Nyakasenga kwenda shule ya msingi ya kijiji hicho na Nyambare kwenda Mwasu.

Awali Akizungumzia hali hiyo Diwani wa kata hiyo Mizengo(Chadema)amesema tatizo hilo hujitokeza kila mwaka kwenye kipindi cha masika kutokana na maeneo hayo kukosa madaraja baada ya barabara kukatika.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa