VYAMA vya
ushirika vya kuweka na kukopa katika Halmashauri ya wilaya ya Biharamulo mkoani
Kagera vyadaiwa kushindwa kujiendesha inavyotakiwa kutokana na kukosa wahasibu
waliosomea taaluma hiyo.
Ofisa ushirika wa Halmashauri ya wilaya ya
Biharamaulo,Mary Kahesi alisema hali hiyo imesababisha vyama hivyo kushindwa
kurejesha mikopo ya wanachama na hivyo kukabiliwa na uhaba wa fedha za
kuendesha mafunzo kwa wanachama wake.
Kahesi,amesema hayo baada ya kutakiwa na kaimu
mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bw.Zabron Njanga kutoa maelezo kuhusiana na
kuwepo kwa baadhi ya vyama vya ushirika vya vijana kushindwa kurejesha mikopo
yake kwa wakati na kupoteza mwelekeo wa mpango wa kuanzishwa kwake.
Hatua hiyo ya mkurugenzi ilikuja kufuatia baadhi
ya madiwani kwenye kikao chao cha baraza kilichofanyika jana(J'tano)kutaka
kupewa mpango mkakati wa kuboresha vyama hivyo hasa kwa upande wa makundi ya
vijana na akina mama.
Diwani wa kata ya Bisibo Bw.Joseph
Kayamba(chadema),alisema pamoja na kuwepo kwa vijana wengi kujiunga kwenye
vyama vya ushirika baadhi yao wanakosa mikopo na hivyo vyama hivyo
kusambaratika kutokana na kutokuwa na elimu ya ujasiriamali.
Katika taarifa ya utendaji wa kazi na
uwajibikaji wa halmashauri hiyo katika kipindi cha kaunzia julai 2012 hadi juni
2013 iliyowasilishwa na ofisa uchumi,Abdalah Mvungi kwenye kikao hicho
kuonyesha uhaba wa fedha na wananchi kukosa ubunifu wa kuunganisha shughuli zao
ili kuunda vyama vya ushirika.
0 comments:
Post a Comment