WANANCHI WAONYWA KUTOWAKARIMU WAGENI WASIOWAJUA


Kamanda wa polisi mkoa wa Geita, Joseph Konyo
Makamanda wa Polisi wa Kigoma, Kagera na Geita, wamewataka wananchi kutowakarimu wageni wasiowajua kwani wengi wao ni wahalifu wanaotumia silaha za moto.
Kutokana na hofu ya kuwapo kwa wageni wengi katika mikoa hiyo, makamanda hao wameamua kuzindua mpango endelevu wa kuangamiza mtandao wa uhalifu wa kutumia silaha unaotishia maisha ya wananchi wengi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita, Joseph Konyo, alisema wananchi lazima wachukue tahadhari baada ya Januri 19 mwaka huu katika kitongoji cha Mhama kijiji cha Ilyamchele wilayani Bukombe, Geita, kuwakarimu majambazi kwa kuwapa chakula na vinywaji wakiamini ni wasamaria wema, lakini baadaye wakafanya uhalifu na uporaji kwa kutumia silaha za moto.
Konyo alisema alisema wagani hao ambao wengi wao huvuka mipaka toka nchi za jirani, jeshi la polisi la mikoa hiyo mitatu imeamua kuzindua mkakati kabambe wa kuuteketeza mtandao huo.
Naye kamanda wa polisi mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe, alizindua mkakati huo Januari 20 katika kijiji cha Nyakanazi wilayani Biharamulo mkoa wa Kagera.
Majambazi hao ambao baada ya kufanya uharamia wa uporaji, walisakwa na polisi na kuishia kupora mchele kilo 60 na baiskeli tatu ambazo walitumia kubebea mchele huo wa uporaji.
Aidha, alisema majambazi hao baada ya kufanya uporaji waliondoka katika kijiji hicho na kuteketekeza kwa moto kwa kuwatisha wanakijiji na polisi ili wasiwafuatilie.
Hata hivyo, ilielezwa mtandao huo wa ujambazi wa kutumia silaha umeshamiri katika miji ya Lunzewe, Namonge, Kasanda  na Mabamba iliyopo mikoa ya Geita, Kagera na Kigoma, baada ya kufanya uhalifu huvuka mipaka na kukimbilia nchi jirani.
Mwaka jana watu wanaosadikiwa majambazi, walivamia kituo kikuu cha polisi wilaya ya Bukombe mkoani Geita ,kuua polisi wawili na  kupora silaha mbalimbali lakini  na ushirikiano na wananchi uliwezesha  polisi kuwakamata watuhumiwa pamoja na silaha zilizoibwa.
CHANZO: NIPASHE 
KUELEKEA UCHAGUZI 2015: JE UNAPENDA NANI AWE KIONGOZI WAKO? JAZA FOMU HII FUPI HAPA

JAJI MUTUNGI AVIONYA VYAMA VYA SIASA VINAVYOENDEKEZA MIGOGORO

Hivi Karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la Migogoro ndani ya vyama vya Siasa. Jambo hili linaleta Taswira mbaya kwa jamii, hasa kipindi hiki ukielekea katika uchaguzi Mkuu wa nchi.

Athari za migogoro hii ni nyingi, ikiwemo chama cha kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa, kupoteza mvuto kwa jamii na wanachama wake, ukosefu wa amani na utulivu ndani ya chama na kupoteza sifa za usajili.
Hivi sasa mfumo wa demokrasi ya vyama vingi vya siasa una takribani miaka 23 tangu urejee tena mwaka 1992. Hivyo jamii inategemea kuwa mwanasiasa na vyama vya siasa kuonyesha ukomavu na busara katika kuokuongoza na kushiriki shughuli za chama.
Mojawapo ya ukomavu na ustarabu huo ni kuweka mifumo, kuongoza na kushiriki shughuli za chama katika namna ambayo itaepusha migogoro. 
Mojawapo ya Mambo ya kuzingatia ni chama kudhibiti tofauti za wanachama na baina ya viongozi kwa njia ya kidemokasia na utawala bora katika kuongoza na kushiriki shughuli za chama na kuheshimu na kufuata sheria, katiba na kanuni za chama.
Hivyo natumia nafasi hii kama ninavyotambulika na jamii kuwa ni mlezi wa vyama vya siasa, kuvisihivyama vyote vya siasa, kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria, katiba na kanuni zake. Pia kuwa mfano mzuri kwa jamii kwa kudumisha amani na utulivu ndani ya vyama vya siasa.

WAZIRI WA JK ATEMA CHECHE

WAZIRI katika Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, ametaka viongozi wote walionufaika na fedha za kutoka akaunti ya Tegeta Escrow, washtakiwe, wafungwe na kufilisiwa mali zao, kwani kuwafuta kazi au kujiuzulu hakusaidii Watanzania.

“Kitendo cha kufukuzwa kazi viongozi walionufaika na fedha za akaunti ya Escrow hakutoshi... kuwafanya hivyo, ni sawa na kuwafanyia watu send off na kuwapeleka fungate kwa pesa ya wananchi.”

Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, wakati alipofanya ziara katika Hospitali ya Mwananyamala ili kuwajulia hali wajawazito na watoto ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Alisema endapo watafilisiwa na kufungwa jela itakuwa ni kujenga Taifa lenye kuogopa fedha za umma zinazohitajika kutumika sehemu nyingi kwa ajili ya manufaa ya nchi yetu.

“Watu wanaokula pesa za wananchi ni lazima wafukuzwe, kufungwa na hata kufilisiwa pesa hizo ni kodi ya wananchi ambayo ingetumika sehemu nyingine kama hospitali...kitendo cha wajawazito kulala watu wawili ni aibu kwa nchi yetu, hivyo inatakiwa ukusanywaji wa kodi ufanywe kwa kina ili kuondoa changamoto zilizopo hospitalini,”alisema Nchemba.

Aliongeza kuwa tayari watumishi saba wamesimamishwa kazi ni wale ambao walioiachia kodi katika sakata la escrow. “

Hivyo wanatakiwa kuhojiwa na katika mahojiano hayo wakisema kuwa walikuwa hawajui kama pesa hizo zilikuwa zinatakiwa kukatiwa kodi itajulikana kuwa walikuwa si watumishi wa TRA au BoT na wakisema kuwa walikuwa wanajua ni lazima hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Nchemba aliwashangaa viongozi wenzake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuacha kufanya majukumu waliyonayo na kuanza kusimulia habari za uchukuaji wa fomu za urais.

“Hii inachekesha mno badala ya sisi viongozi kufanya majukumu yetu tuliyoagizwa tunawaza namna ya kuchukua fomu ya urais wakati muda bado haujafika, wana- CCM wenzangu muda ukifika kila mtu atawajibika kuchukua fomu,”alisema Nchemba.

Naye, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala Dkt. Sophinias Ngonyani, alisema anashukuru kwa msaada alioutoa Waziri katika hospitali hiyo kwa kuwa utawaletea tija.

Chanzo:Majira

UKOSEFU WA KAZI KWA VIJANA NI JANGA LA DUNIA‏

DSC_0499
Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari (UTPC), Abubakar Karsan akionyesha gazeti la "Tuwasiliane" linalochapishwa na UTPC na kusambazwa kwa wadau na maeneo mbalimbali ya jijini Mwanza kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyetembelea makao ya ofisi hizo kwa ajili ya mazungumzo na kuboresha ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa Umoja huo wa vilabu vya waandishi wa habari nchini.
Na Mwandishi Wetu
WIMBI kubwa la kuwa na vijana wasiokuwa na kazi limeelezwa kuwa tatizo duniani kote na serikali mbalimbali zinatakiwa kuliangalia hilo kwa undani na kulitatua.
Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.
Mratibu huyo alisema hayo katika mazungumzo yake na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari (UTPC) Abubakar Karsan.
Alisema ukosefu wa kazi kwa sasa ni tatizo la kijamii na kwamba, shauri hilo lisipoangaliwa kwa makini linaweza kuwa chanzo cha matatizo makubwa ya usalama na amani katika taifa.
Alvaro Rodriguez ambaye alifika katika ofisi za UTPC kuangalia mambo yanayofanyika katika ofisi hiyo wakati akiwa ziarani Mwanza wiki iliyopita, alisema kama tatizo la ajira litaendelea kuwapo, vijana wanaoathirika wanaweza kufikiria njia nyingine isiyo ya kistaarabu kufanikisha mambo yao.
DSC_0440
Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari (UTPC), Abubakar Karsan akizungumza na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) aliyeambatana na Mshauri wa masuala ya haki za binadamu kutoka ofisi ya mratibu mkazi wa UN Tanzania, Bi. Chitra Massey (kulia) alipotembelea makao makuu ya ofisi hizo jijini Mwanza.
Alisema Umoja wa Mataifa unaendelea kushirikiana na serikali mbalimbali kuhakikisha kwamba tatizo la ajira kwa vijana linamalizwa ili jamii isiingie katika mtafaruku utakaokosesha amani na usalama na hivyo kusimamisha maendeleo yaliyofikiwa katika jamii.
Bila kutaja makundi ya kigaidi yanayotikisa dunia kwa sasa kama Al - Qaeda na washirika wake Boko Haram, Al - Shabab, Islamic State of Iraq na Levant (ISIL) alisema makundi mengi ya kigaidi duniani yanatokana na vijana kutojua wafanye nini na mazingira waliyonayo na hivyo kuwa rahisi kushawishika.
Alisema makundi ya hatari mara nyingi ni ya vijana ambao wanashindwa kupata riziki au hawajui wafanye nini kupata riziki na serikali zimewaacha bila kuwaangalia.
Aidha alisema Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia kuhakikisha kwamba masuala muhimu yanayowezesha maendeleo kama demokrasia yanazingatiwa ili kuiwezesha jamii kufanya maamuzi sahihi ya vile wanavyotaka kupanga maendeleo yao.
DSC_0487
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (kulia) akichangia jambo wakati wa mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari (UTPC) Abubakar Karsan makao makuu ya ofisi za umoja huo jijini Mwanza.
Alisema Demokrasia huwezesha wananchi kujua namna wanavyoweza kutengeneza mustakabali wao katika masuala ya ustawi wa jamii na maendeleo huku haki zao za msingi zikilindwa.
Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC, Bw. Karsan alimwambia mratibu huyo mambo ambayo yamefanywa na umoja huo na changamoto walizokumbana nazo kwa kuzingatia mpango mkakati wake wa mwaka 2011-2013.
Umoja huo ambao ulianzishwa mwaka 1996 na kusajili na wizara ya mambo ya ndani kama taasisi isiyokuwa ya kiserikali (NGO) mwaka uliofuata, umefanikiwa kuanzisha mfuko wa kusaidia vyombo vya habari kwa jina la Daudi Mwangosi, aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari wa Iringa (IPC).
DSC_0481
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari (UTPC), Abubakar Karsan wakati wa mazungumzo ya kuboresha mahusiano baina ya mashirika ya umoja wa mataifa na umoja wa vilabu vya waandishi wa habari nchini Tanzania.
Aidha alimwambia kwamba wamefanikisha mafunzo ya kuongeza umahiri wa uandishi wa habari na pia kuwaelezea umma juu ya uhuru wa vyombo vya habari.
Pia alielezea mafanikio yaliyopatikana katika kampeni za kuelimisha umma na kuelewana miongoni mwa wadau mbalimbali wa sekta ya habari.
Alisema hata hivyo bado wanaendelea na kampeni yao kutaka mabadiliko ya malipo kwa waandishi wa habari wanaojitegemea ambao ndio wanatoa mchango wa asilimia 75 hadi 80 za habari zinazotangazwa au kuchapishwa.
Aidha wanaendelea kutoa mafunzo ya kanuni na maadili kwa waandishi wa habari na kuendelea kukabiliana na tatizo la usalama katika mpango mkakati wa mwaka 2015 – 2019.
Katika ziara hiyo ya kanda ya Ziwa, mratibu huyo aliambatana na mshauri mwandamizi wa masuala ya haki za binadamu Dk Chitralekha Massey na Mtaalamu wa mawasiliano wa umoja huo hapa nchini HoyceTemu.

SOMA KWA MAKINI SANA HII : FAHAMU SIRI NZITO YA BIASHARA YA BATA MZINGA ,CHANGAMKIA FURSA HII YA WAZI


Wengi watahoji nitafugia wapi! Hautakuwa una shida ya hela ndugu yangu, lakini sikulaumu sana kwa kuwa mfumo wa sisi hasa watanzania ni kuajiriwa, na ajira zetu hizi za kupata mwisho wa mwezi kiasi kidogo cha hela na kuridhika, huwa kinatudanganya sana.  Wengi wetu hujiingiza katika makundi ya udanganyifu kwa kuwa tunatafuta kipato cha ziada kwa njia isiyo halali, na mwisho wa siku ajira zetu sasa zina dhambi, dhambi ya rushwa, kutokuaminika, kuharibiana ajira.  Hii yote ni dhambi tu, hatutaki kushirikiana ili kuweza kufanya kazi kwa bidii na kukuza kipato chetu na kufanya kazi za umma kwa maslahi binafsi, na maslahi ya umma.
Sio mada yangu hii leo lakini naomba tujue baadhi ya sababu zinazojenga ukanjanja kazini.  Hatujipangi kikamilifu, tunacheza na majukwaa (tunataka kuonekana na jamii tuna uwezo kumbe si kweli)
Bata Mzinga ni bata anayefugwa nyumbani, na ana uwezo wa kukua hadi kufikia kilo 15, ni
pambo la nyumba pia.

Kwanini namuongelea Bata Mzinga leo, nimegundua kila ninapoenda katika Super Markets kubwa nakuta nyama ya bata hawa inauzwa na tena bei kubwa tu, mfano mimi nilinunua kifaranga cha bata mzinga kwa shilingi 25,000 walikuwa watano ambayo ni sawa na shilingi 125,000.
Kwa wale wanaojua kilo moja ya bata mzinga inauzwa kuanzia shilingi 10,000 na bata mzinga ana kilo 15 ni sawa na shilingi 150,000 hivi huoni kuwa huyu muuzaji wa kilo moja moja anafaida kubwa sana kuliko wewe mkulima?
Bata mzinga mmoja mwenye kilo 12 kwa jike na kilo 15 kwa dume anauzwa hivi;
Bata mzinga jike ni shilingi 60,000
Bata mzinga dume ni shilingi 70,000
Mfano una bata mzinga 2,000, majike 1,000 na madume 1,000 unajua utakuwa una miliki shilingi ngapi?
Ukiwa na majike 1,000 wenye thamani ya shilingi 60,000 = 60,000,000
Ukiwa na madume 1,000 wenye thamani ya shilingi 70,000 = 70,000,000
                                                                                                                       
Mfano ukijiingiza katika biashara hii kwa kununua bata mzinga wadogo 40 kwa shilingi 25,000 kwa kila mmoja unaweza kupata majike 25 na madume 15 kwanza ili uanze kutengeneza kizazi cha kufuga kwanza.  Chukulia mfano jike moja likitotoa vifaranga 10 x 25 = 250.  Fanya kila bata mzinga atotoe mizunguko mitano itakuwa 250 x 5 = 1,250

Sasa chukua hao watoto 1,250 nao wawe madume nusu na majike nusu 625 x 10 = 6,250.  Chukua idadi ya kwanza 40 + 250 + 1,250 + 6,250 = 7,790 unaona wanavyoongezeka kutoka 40 hadi sasa una bata mzinga 7,790 tayari hapa wewe ni milionea hizi ni sawa na shilingi 467,400,000 unazo ndani.
Bata mzinga 7,790 ukiwagawa madume na majike nusu kwa nusu utapata majike 3,895 chukua kila bata mzinga atotoe vifaranga 10 kila mmoja utapata bata mzinga 38,950

UUZAJI VIFARANGA
Hawa bata mzinga 38,950 unaweza kuuza kama vifaranga, na kila kifaranga utakiuza kwa shilingi 25,000.  38,950 x 25,000 = 973,750,000 hii ni fedha taslimu utaipata kwa kuuza vifaranga.



Katika miaka kumi ya ufugaji wako wa bata mzinga unaweza kujikuta unakuwa bilionea kama ukiwa makini na mwenye nia kweli ya kuzitafuta pesa kwa kuwafuga hawa bata. 
Leo tumeanza na bata mzinga 40 lakini tunamaliza na bata mzinga 46,740 wastani wa bata mzinga 50,000.
Kazi yangu ni kukupa changamoto mdau mwenzangu katika kutengeneza maisha ya ufugaji na fedha.  Unaweza kustaafu kazi ya kuajiriwa lakini ukaanza ufugaji na ukatengeneza hela nyingi zaidi, usikate tama.  Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, alianza madaraka mwaka 2005 jana tu tulimpigia kura kwa shangwe na vigelegele, kumbuka 2010 tena tumempigia kura na sasa amebakiza mwaka mmoja tu wa madaraka yake, je huoni kuwa jana tu imeshageuka leo? Hujachelewa bado kwa mwaka huu wa madaraka yake na mwezi huu Januari, 2014 badilika anza ufugaji nenda na malengo kama haya, nakuhakikishia nitakutafutia masoko pia, na nitakutangaza kwa moyo wangu wote. Sijui atakayenisaidia mbele ya safari.  Ila wewe utakayefuata haya ninayokuambia na ukafanikiwa usinisahau katika ufalme wako, hata kama sitakuwepo basi waangalie hata wanangu.

Ushauri wangu kwako usitake makubwa haraka nimekupa mfano wa Raisi wan chi ili uone kuwa miaka 10 ni mingi kuitaja, lakini ni michache ukibung’aa huku unangoja maisha bora na elimu yako unapanda jukwaani unalalamika pamoja na asiyena elimu, ni wakati sasa wakutoa vilivyo kichwani na kuviweka katika maandishi na vifanyiwe kazi.
Tuwasiliane kwa kupeana mawazo
Maoni yako ni Muhimu
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

SAD: BABA AMTOBOA MWANAYE MACHO NA YEYE KUJINYONGA!

Godfrey Joseph Kajuna (45) mkazi Muleba Mkoa wa Kagera ampiga kwa fimbo nzito na kumtoboa macho bintiye wa miaka 12 Agripina Godfrey kisha naye kujinyonga hadi kufa
Chanzo ni kwamba Baba alitoka na kuwambia wanae kuwa Mama yao akirudi wasimfungulie mlango, hivyo mama aliporudi watoto kwa kumuogopa Baba yao wakakataa kumfungulia Mlango. Basi Mama akaondoka kujihifadhi kwingine.
Vijimambo Blog

ASHA BARAKA AMUONYA DIAMOND KWA UNGA


Mkurungezi wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ Asha Baraka.

Na Laurent Samatta
Mkurungezi wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ Asha Baraka amemuonya msanii anayefanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kutojaribu kujihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya na kusema akijaribu atapotea.

Akizungumza na Ijumaa hivi karubini, Asha Baraka ‘Iron Lady’ alisema Diamond anaweza kufanya vizuri kwa miaka mingi inayokuja lakini akijaribu kutumia dawa hizo ataishia pabaya.

“Tumeona wasanii wengi wa Tanzania ambao awali walikuwa wanafanya vizuri lakini baada ya kujaa sifa na kukutana na marafiki wengi pamoja na makundi wakazama kwenye dawa za kulevya na sasa wanatapatapa na kubaki kulaumu wakati wenyewe wamejiharibia,” alisema Iron Lady.

Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Wasani ambao awali walikuwa wakifanya vizuri kimuziki lakini baadaye ‘wakadrop’ baada ya kujiingiza kwenye matumizi ya unga ni pamoja na Chid Benzi, Ray C, Q Chiller, Lord Eyez, Msafiri Diof na wengine ambao sasa wameshafariki.
Chanzo: Vijimambo blog
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa