Kamanda wa polisi mkoa wa Geita, Joseph Konyo
Kutokana na hofu ya kuwapo kwa wageni wengi katika mikoa hiyo,
makamanda hao wameamua kuzindua mpango endelevu wa kuangamiza mtandao wa
uhalifu wa kutumia silaha unaotishia maisha ya wananchi wengi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita, Joseph Konyo, alisema wananchi
lazima wachukue tahadhari baada ya Januri 19 mwaka huu katika kitongoji
cha Mhama kijiji cha Ilyamchele wilayani Bukombe, Geita, kuwakarimu
majambazi kwa kuwapa chakula na vinywaji wakiamini ni wasamaria wema,
lakini baadaye wakafanya uhalifu na uporaji kwa kutumia silaha za moto.
Konyo alisema alisema wagani hao ambao wengi wao huvuka mipaka toka
nchi za jirani, jeshi la polisi la mikoa hiyo mitatu imeamua kuzindua
mkakati kabambe wa kuuteketeza mtandao huo.
Naye kamanda wa polisi mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe, alizindua
mkakati huo Januari 20 katika kijiji cha Nyakanazi wilayani Biharamulo
mkoa wa Kagera.
Majambazi hao ambao baada ya kufanya uharamia wa uporaji, walisakwa
na polisi na kuishia kupora mchele kilo 60 na baiskeli tatu ambazo
walitumia kubebea mchele huo wa uporaji.
Aidha, alisema majambazi hao baada ya kufanya uporaji waliondoka
katika kijiji hicho na kuteketekeza kwa moto kwa kuwatisha wanakijiji na
polisi ili wasiwafuatilie.
Hata hivyo, ilielezwa mtandao huo wa ujambazi wa kutumia silaha
umeshamiri katika miji ya Lunzewe, Namonge, Kasanda na Mabamba iliyopo
mikoa ya Geita, Kagera na Kigoma, baada ya kufanya uhalifu huvuka mipaka
na kukimbilia nchi jirani.
Mwaka jana watu wanaosadikiwa majambazi, walivamia kituo kikuu cha
polisi wilaya ya Bukombe mkoani Geita ,kuua polisi wawili na kupora
silaha mbalimbali lakini na ushirikiano na wananchi uliwezesha polisi
kuwakamata watuhumiwa pamoja na silaha zilizoibwa.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment