Hivi
Karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la Migogoro ndani ya vyama vya Siasa.
Jambo hili linaleta Taswira mbaya kwa jamii, hasa kipindi hiki ukielekea
katika uchaguzi Mkuu wa nchi.
Athari
za migogoro hii ni nyingi, ikiwemo chama cha kushindwa kutekeleza
majukumu yake kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa, kupoteza mvuto
kwa jamii na wanachama wake, ukosefu wa amani na utulivu ndani ya chama
na kupoteza sifa za usajili.
Hivi
sasa mfumo wa demokrasi ya vyama vingi vya siasa una takribani miaka 23
tangu urejee tena mwaka 1992. Hivyo jamii inategemea kuwa mwanasiasa na
vyama vya siasa kuonyesha ukomavu na busara katika kuokuongoza na
kushiriki shughuli za chama.
Mojawapo
ya ukomavu na ustarabu huo ni kuweka mifumo, kuongoza na kushiriki
shughuli za chama katika namna ambayo itaepusha migogoro.
Mojawapo
ya Mambo ya kuzingatia ni chama kudhibiti tofauti za wanachama na baina
ya viongozi kwa njia ya kidemokasia na utawala bora katika kuongoza na
kushiriki shughuli za chama na kuheshimu na kufuata sheria, katiba na
kanuni za chama.
Hivyo
natumia nafasi hii kama ninavyotambulika na jamii kuwa ni mlezi wa
vyama vya siasa, kuvisihivyama vyote vya siasa, kutekeleza wajibu wao
kwa mujibu wa sheria, katiba na kanuni zake. Pia kuwa mfano mzuri kwa
jamii kwa kudumisha amani na utulivu ndani ya vyama vya siasa.
0 comments:
Post a Comment