Wengi watahoji nitafugia wapi! Hautakuwa una shida
ya hela ndugu yangu, lakini sikulaumu sana kwa kuwa mfumo wa sisi hasa
watanzania ni kuajiriwa, na ajira zetu hizi za kupata mwisho wa mwezi kiasi
kidogo cha hela na kuridhika, huwa kinatudanganya sana. Wengi wetu hujiingiza katika makundi ya
udanganyifu kwa kuwa tunatafuta kipato cha ziada kwa njia isiyo halali, na
mwisho wa siku ajira zetu sasa zina dhambi, dhambi ya rushwa, kutokuaminika,
kuharibiana ajira. Hii yote ni dhambi
tu, hatutaki kushirikiana ili kuweza kufanya kazi kwa bidii na kukuza kipato
chetu na kufanya kazi za umma kwa maslahi binafsi, na maslahi ya umma.
Sio mada yangu hii leo lakini naomba tujue baadhi ya
sababu zinazojenga ukanjanja kazini.
Hatujipangi kikamilifu, tunacheza na majukwaa (tunataka kuonekana na
jamii tuna uwezo kumbe si kweli)
Bata Mzinga ni bata anayefugwa nyumbani, na ana
uwezo wa kukua hadi kufikia kilo 15, ni
pambo la nyumba pia.
Kwanini namuongelea Bata Mzinga leo, nimegundua kila
ninapoenda katika Super Markets kubwa nakuta nyama ya bata hawa inauzwa na tena
bei kubwa tu, mfano mimi nilinunua kifaranga cha bata mzinga kwa shilingi
25,000 walikuwa watano ambayo ni sawa na shilingi 125,000.
Kwa wale wanaojua kilo moja ya bata mzinga inauzwa
kuanzia shilingi 10,000 na bata mzinga ana kilo 15 ni sawa na shilingi 150,000
hivi huoni kuwa huyu muuzaji wa kilo moja moja anafaida kubwa sana kuliko wewe
mkulima?
Bata mzinga mmoja mwenye kilo 12 kwa jike na kilo 15
kwa dume anauzwa hivi;
Bata mzinga jike ni shilingi 60,000
Bata mzinga dume ni shilingi 70,000
Mfano una bata mzinga 2,000, majike 1,000 na madume
1,000 unajua utakuwa una miliki shilingi ngapi?
Ukiwa na majike 1,000 wenye thamani ya shilingi
60,000 = 60,000,000
Ukiwa na madume 1,000 wenye thamani ya shilingi
70,000 = 70,000,000
Mfano ukijiingiza katika biashara hii kwa kununua bata
mzinga wadogo 40 kwa shilingi 25,000 kwa kila mmoja unaweza kupata majike 25 na
madume 15 kwanza ili uanze kutengeneza kizazi cha kufuga kwanza. Chukulia mfano jike moja likitotoa vifaranga
10 x 25 = 250. Fanya kila bata mzinga
atotoe mizunguko mitano itakuwa 250 x 5 = 1,250
Sasa chukua hao watoto 1,250 nao wawe madume nusu na
majike nusu 625 x 10 = 6,250. Chukua
idadi ya kwanza 40 + 250 + 1,250 + 6,250 = 7,790 unaona wanavyoongezeka kutoka
40 hadi sasa una bata mzinga 7,790 tayari hapa wewe ni milionea hizi ni sawa na
shilingi 467,400,000 unazo ndani.
Bata mzinga 7,790 ukiwagawa madume na majike nusu
kwa nusu utapata majike 3,895 chukua kila bata mzinga atotoe vifaranga 10 kila
mmoja utapata bata mzinga 38,950
UUZAJI VIFARANGA
Hawa bata mzinga 38,950 unaweza kuuza kama
vifaranga, na kila kifaranga utakiuza kwa shilingi 25,000. 38,950 x 25,000 = 973,750,000 hii ni fedha
taslimu utaipata kwa kuuza vifaranga.
Katika
miaka kumi ya ufugaji wako wa bata mzinga unaweza kujikuta unakuwa bilionea
kama ukiwa makini na mwenye nia kweli ya kuzitafuta pesa kwa kuwafuga hawa
bata.
Leo
tumeanza na bata mzinga 40 lakini tunamaliza na bata mzinga 46,740 wastani wa
bata mzinga 50,000.
Kazi
yangu ni kukupa changamoto mdau mwenzangu katika kutengeneza maisha ya ufugaji
na fedha. Unaweza kustaafu kazi ya
kuajiriwa lakini ukaanza ufugaji na ukatengeneza hela nyingi zaidi, usikate
tama. Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, alianza madaraka mwaka 2005 jana tu
tulimpigia kura kwa shangwe na vigelegele, kumbuka 2010 tena tumempigia kura na
sasa amebakiza mwaka mmoja tu wa madaraka yake, je huoni kuwa jana tu
imeshageuka leo? Hujachelewa bado kwa mwaka huu wa madaraka yake na mwezi huu
Januari, 2014 badilika anza ufugaji nenda na malengo kama haya, nakuhakikishia
nitakutafutia masoko pia, na nitakutangaza kwa moyo wangu wote. Sijui
atakayenisaidia mbele ya safari. Ila
wewe utakayefuata haya ninayokuambia na ukafanikiwa usinisahau katika ufalme
wako, hata kama sitakuwepo basi waangalie hata wanangu.
Ushauri
wangu kwako usitake makubwa haraka nimekupa mfano wa Raisi wan chi ili uone
kuwa miaka 10 ni mingi kuitaja, lakini ni michache ukibung’aa huku unangoja
maisha bora na elimu yako unapanda jukwaani unalalamika pamoja na asiyena
elimu, ni wakati sasa wakutoa vilivyo kichwani na kuviweka katika maandishi na
vifanyiwe kazi.
Maoni yako ni Muhimu
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment