Na
Mwandishi Wetu-KAGERA
Waziri
Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa ameipongeza Serikali kwa namna ilivyojipanga
kukabiliana na athari za tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo.
Bw.
Lowassa amesema hayo kupitia salamu zake alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Kagera,
Meja Generali Salum Kijuu, ofisini kwake kumpa pole kutokana na athari
zilizotokana na tetemeko hilo.
“Napenda
nikupongenze mkuu wa mkoa kwa namna ulivyokabili tukio hili, wala hatukuwa na
mashaka wewe ni mtaalam wa majeshi wa siku nyingi kwa hiyo jambo hili limempata
mwenyewe mpiganaji na tunaona kwa pamoja mmelishikilia vizuri,” alisema Lowassa.
Adha
Mhe. Lowassa alisema kuwa suala hili ni kubwa na halipaswi kuiachia Serikali
peke yake katika kulikabili nalo kwani madhara yanaonekana ni makubwa hivyo
watanzania wote wana budi kuwasaidia waathirika.
Katika
kushirikiana na wananchi wa Kagera, Bw. Lowassa ameahidi kutoa mifuko 400 ya
saruji kwa ajili ya ujenzi ya miundombinu iliyoharibika.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja, Generali Salum Kijuu ameendelea
kuwasisitiza watanzania kuchangia kile walichonacho ili kusaidiana na serikali
katika kuwafariji waathirika wa tetemeko hilo.
“Tunashukuru
watanzania kwa misaada wanayoendelea kutoa kwa ajili ya kuwasaidia waathirika
wa tetemeko ila bado tunaendelea kuwasisitiza tuendele kujitoa kwa ajili ya
kuwasaidia watu wenye mahitaji,” alisema Meja Generali Salum Kijuu.
0 comments:
Post a Comment