Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za janga
la tetemeko la ardhi lililotokea jana tarehe 10/09/2016 katika Mkoa wa
Kagera na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Mwanza na Shinyanga.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu kufuatia
vifo vilivyotokana na tetemeko hilo.
Katika
salamu zake Ndg Kinana amesema Chama cha Mapinduzi kinatoa pole kwa
wahanga na kwa familia, ndugu na jamaa waliopoteza wapendwa wao katika
janga hilo.
Chama cha Mapinduzi kipo pamoja na wahanga, kushirikiana nao kwa hali na mali katika kipindi hiki kigumu.
WanaCCM nchi nzima tunamuomba Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu pema peponi. Amina.
Imetolewa na:-
CHRISTOPHER OLE SENDEKA (MNEC)
MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
Tarehe 11/09/2016.
0 comments:
Post a Comment