Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba.
Shirika
la Kiristo la Kuhudumia Wakimbizi Tanganyika (TCRS) limechangia vifaa
vyenye jumla ya Sh. milioni 60.92 ikiwa ni mchango wao wa kuwafuta
machozi wanakagera baada ya kuathiriwa na tetemeko la ardhi.
Katika kuhakikisha hali za wananchi na ttaasisi za kutolea huduma za kijamii zinaimarika na kurudi kwenye hali ya kawaida, wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi bado michango yao inahitajika.
Akikabidhi
mchango huo, Mratibu wa Miradi inayoendeshwa na TCRS Oscar Rutenge
pamoja na Jasmine Gwamsy wametaja mchanganuo wa msaada huo kuwa ni
pamoja na blanketi, 1680, mashuka 840, ndoo za kutumia 840, nguo za
kutumia kwawanawake, wanaume na watoto box 50, sabuni katoni 1680 pamoja
na vifaa vingine 2250.
Akipokea
msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu
amemelishukuru shirika hilo kwa mchango wao huo kwani ni wa thamani hasa
baada ya tetemeko hilo kuwaaathiri wananchi wa mkoa huo.
Aidha,
Meja Jenerali Mstaafu Kijuu amewakaribisha na kuwataka wadau wengine
waguswe kwa namna ya kipekee na waendelee kutoa michango yao waweze
kuwasaidia wananchi na kurudisha hali yao na kuendelea na shughuli zao za kijamii na kimaendeleo.
0 comments:
Post a Comment