Rais Dkt. John Magufuli leo Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu
Tawala wa Mkoa wa Kagera, Amantius Msole na Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Bukoba, Steven Makonda baada ya kubaini kuwa wamefungua
akaunti nyingine ya benki kwa kutumia jina linalofanana na akaunti rasmi
ya kuchangia maafa iitwayo "Kamati Maafa Kagera" kwa lengo la kujipatia
fedha.
Kwa mujibu wa Ikulu jijini Dar es Salaam taarifa iliyotolewa na
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa muda mfupi baada ya kupokea hundi ya msaada
kutoka kwa Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi iimeeleza kuwa pamoja na
kutengua uteuzi huo Rais Magufuli ameagiza vyombo vya dola vichukue
hatua dhidi ya wote waliohusika katika njama za kufungua akaunti hiyo.
Msaada huo ni wa shilingi Milioni 545.
Aidha, Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa
Mkoa wa Kagera, Simbaufoo Swai kutokana na kuhusika katika njama hizo.
Hata hivyo Waziri Mkuu ametoa wito kwa wananchi na taasisi mbalimbali
kuendelea kuchangia misaada kwa ajili ya walioathirika kwa kutumia
akaunti rasmi ya "Kamati Maafa Kagera" ambayo imetangazwa na Serikali.
CHANZO HABARI LEO
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment