Na Beatrice Lyimo
MAELEZO
21/09/2016
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista
Mhagama amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera kufanya
ukarabati wa haraka wa kuziba nyufa zilizotokea katika taasisi za
Serikali zilizoathirika kutokana na tetemeko la ardhi lilitokea hivi
karibuni Mkoani humo.
Waziri
Mhagama aliyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya kukagua taasisi
mbalimbali za Serikali zilizoathirika kutokana na maafa ya tetemeko la
ardhi lililotokea mkoani humo tarehe 10 Septemba mwaka huu.
Katika ziara hiyo, Waziri Mhagama alimtaka Mkuu wa Wilaya hiyo kutoa misaada kwa waathirika waliofanyiwa tathmini ili kuwawezesha kupata huduma muhimu za kijamii.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Wilaya hiyo, Festo Kiswaga alisema kuwa Ofisi yake
imeshaanza kuwaga baadhi ya maturubai na chakula ikiwemo sukari kwa
waathirika wa tetemeko hilo.
Aidha
Waziri Mhagama pia alitembelea Shule ya Msingi Byeju iliyopo Wilayani
humo ili kujionea baadhi ya vyoo na madarasa ya shule ambayo
yalivyoathirika na tetemeko hilo na kuagiza ukarabati wa miundombinu
hiyo kuanza mara moja.
0 comments:
Post a Comment