ZITTO: HERI NIWE MSALITI WA CHAMA SI TAIFA

KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Bw. Zitto Kabwe, amesema ni heri aendelee kuitwa msaliti na watu wasio na dhamira nzuri ya kupigania masilahi ya nchi kuliko kuwasaliti wananchi.


Alisema ataendelea na msimamo wa kuhakikisha masilahi ya Taifa yanawekwa mbele badala ya kukubali kukumbatiwa na watu wenye dhamira ya kunufaisha matumbo na familia zao.

Bw. Kabwe aliyasema hayo Mjini Bukoba, mkoani Kagera juzi kwenye mkutano wa hadhara ikiwa ni mara yake ya kwanza kuwahutubia wakazi wa mji huo tangu aingie kwenye siasa.

Aliongeza kuwa, kabla ya kufumuka mgogoro katika chama chake cha zamani (CHADEMA), wapinzani walikubaliana masuala mbalimbali ya kusimamia likiwemo la kukataa kuchukua posho za vikao, kutotumia mali za umma kwa manufaa ya chama.

Alisema dhamira ya makubaliano hayo ni kuibana Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), hasa inapotaka kusamehe kodi kiholela, kutumia mali za umma kwa masuala yao ya chama na kujipatia posho zisizo na sababu.

"Ndugu zangu wana Bukoba, kilichoniponza ni kusimamia masilahi ya umma si kingine, nilitaka tujitofautishe na CCM lakini wenzangu hawakuwa tayari, kama wote tunachukua posho, kama wote hatutaki kufutiwa msamaha wa kodi na kutumia mali za umma kwa ajili ya vyama vyetu, tofauti yetu itakuwa nini na chama tawala," alihoji Bw. Kabwe.

Aliongeza kuwa, wote wanaomuita msaliti wanapaswa kuwaeleza wananchi wamewafanyia nini ili kutimiza majukumu yao ya kibunge muda wote waliokuwa bungeni.

Alisema kamwe ACT-Wazalendo hakitapita katika makosa ambayo yamefanywa na vyama vingine na kukubaliana kuzindua Azimio la Tabora kutoka katika mazuri ya Azimio la Arusha.

Bw. Kabwe alisema jambo lingine ambalo aliliweka wazi wakati akiwa mbunge na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ni kutaka vyama vya siasa vikaguliwe hesabu zao kwa kuwa vinapokea ruzuku ya Serikali ambayo ni kodi ya wananchi.

"Katika kulitetea Taifa, mimi nilionekana msaliti kwa sababu nilipigania masilahi ya wananchi ambao bado wana kipato cha chini, nipo tayari kuitumikia nchi si kukitumikia chama kwani chama kinapita," alisema Zitto na kuongeza;

"Fedha hizi lazima zikaguliwe ili ifahamike matumizi halali si vinginevyo, nilipokuwa Mwenyekiti wa PAC, nilisema lazima ukaguzi ufanyike kwa vyama vyote kwani hapa tunatetea masilahi ya umma," alisema.

Aliongeza kuwa, Taifa la Tanzania ni la wananchi ambao wengi wao ni maskini; hivyo wanahitaji kuwa na kiongozi jasiri mwenye uthubutu wa kufanya yale anayohubiri hadharani.

Aliongeza kuwa, Tanzania inahitaji mabadiliko na chama cha ACT-Wazalendo kimeanza kutekeleza kwa kuzindua Azimio
la  Tabora ambalo limehuishwa kutoka Azimio la Arusha.

Bw. Kabwe alifafanua kuwa, kiongozi yeyote wa chama hicho ambaye atachaguliwa kwenye nafasi ya kiserikali, hatapokea posho za  vikao wakiwemo  wabunge kwani vikao vya Bunge ni sehemu ya kazi zao.

Alisema hivi sasa nchi imekithiri kwa rushwa na ufisadi mkubwa kutokana na kundi la watu wachache walio wafanyabiashara na wanasiasa.

"Hata watia nia wa nafasi ya urais waliojitokeza hadi sasa katika vyama mbalimbali, wengi wao hawana dhamira ya kupambana na rushwa kwa kuwa wengi wao ni wala rushwa na mafisadi wakubwa.

"Wakati wa hayati Mwalimu Julius Nyerere, si kwamba hakukuwa na rushwa ilikuwapo ndogo ndiyo maana Mwalimu aliweka miiko
na maadili ya viongozi kwa kufuata Azimio la Arusha, hivi sasa nchi haipo katika rushwa; bali ufisadi hali ambayo ni hatari kwa Taifa letu," alisema Bw. Kabwe.

 Chanzo:Majira

MAPOKEZI YA MH. LOWASSA MJINI BUKOBA HAYANA MFANO, AZIDI KUDHAMINIWA KWA KISHINDO‏

 Sehemu ya Wakazi wa mji wa Bukoba Mkoani Kagera wakiwa nje ya Uwanja wa Ndege wa Bukoba, wakimsubiri kumlaki Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa, tayari kwa kupokea fomu ya wanaCCM wa kumdhamini.
 Wadau wa CCM wakijadiliana jambo.
 Ndege iliyombeba Mh. Edward Lowassa ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Bukoba, Mkoani Kagera leo.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Kagera, Mzee Pius Ngeze wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Bukoba, Mkoani Kagera leo Juni 15, 2015. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
 Mh. Lowassa katika tabasamu.
 Umati wa wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera ukiwa umemzunguka Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa, wakati alipowasili kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Kagera, leo Juni 15, 2015.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa akimsikiliza Katibu wa UWT wilaya ya Bukoba Vijijini, Agness Bashemu alipokuwa akitoa taarifa fupi ya namna ya kumkabidhi fomu hizo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba Mjini, Yussuf Ngaiza.



 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa, Hypolitus Matete akiwasalimia wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera leo Juni 15, 2015.

 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoba, Dkt. Aman Kaborou akiwasalimia wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera leo Juni 15, 2015. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mngeja.
 Mjumbe wa Mkutano Mkuu (NEC) Bukoba, Nazir Karamagi akuzungumza machache mbele ya wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera leo Juni 15, 2015. 
 Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Kagera, Mzee Pius Ngeze akizungumza mbele ya umati wa wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera leo Juni 15, 2015, na kutangaza kwamba yeye pia ni mmoja ya wana Safari ya Matumaini.
 Shangwe kila kona.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa akipongezwa na Bibi huyu (ambaye jina lake halikuweza patikana kwa haraka) mara baada ya kupokea fomu za wanaCCM zaidi ya 6000 waliomdhamini ili apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.  
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa akipokea fomu kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Bukoba mjini, Acheni Mwinshehe, zenye majina ya wanaCCM wa Mkoa wa Kagera waliomdhani ili apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. 
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa akizungumza na umati wa wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera leo Juni 15, 2015, Wakati akitoa shukrani zake kwa kumdhamini ili apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Zaidi ya wanaCCM 6000 wamdhamini mkoani Kagera.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa akiwaaga wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera leo Juni 15, 2015, mara baada ya kupokea fomu za wanaCCM zaidi ya 6000 waliomdhamini ili apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. 

KOMREDI KINANA AHITIMISHA ZIARA KAGERA,ASAFIRI KM 4884 KWA MAGARI, MITUMBWI NA MABASIMAGARI,

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Biharamulo leo,wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi cya chama hicho pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Komredi Kinana ambaye katika ziara hiyo  ya Mkoa wa Kagera,ameambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Mnauye, ametembea kwa gari na usafiri wa mitumbwi  katika mkoa huo umbali wa Km 3,374.Pia alisafiri wa basi kutoka Dar es Salaam kwenda Bukoba kwa umbali wa km 1510.

Kinana na msafara wake wamefika katika Wilaya 8 zenye majimbo 9, ambapo amehutubia jumla ya mikutano 74, 11 ya ndani na 63 ya hadhara,Imezinduliwa jumla ya miradi 46 ikiwemo ya CCM 5 na 41 ya maendeleo.Pia wamevuna wanachama wapya 5678 wakiwemo wapinzania 488.

 Komredi Kinana akitoka kukagua mradi wa maji wa Nyakahura uliopo wilayani Biharamulo, Mkoa wa Kagera ambao umekwama kutokana na Wizara ya Maji kuwapatia zabuni ya ujenzi wakandarasi wasio faa. Mradi huo unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa gharama ya sh. bil. 1.4 hadi sasa haujakamilika jambo linalotia hofu kwamba fedha za mradi huo zimeliwa badala kufanyia kazi iliyokusudiwa.

Komredi Kinana ameamuru wale waote waliohusika kuhujumu mradi mradi huo wasakwe na kuwajibishwa.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akisoma moja ya mabango yaliyoshikwa na wananchi yenye maandishi ya tatizo la maji katika kijiji cha Nyakahura lililosababishwa na mradi huo wa maji usiofaa.
 Nape akihutubia katika mkutano wa hadhara na kuwaeleza wananchi kwamba kilio chao hicho wamekisikiliza na kwamba kitafanyiwa kazi.
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano huo, ambapo aliitaka Serikali kuwawajibisha viongozi wote waliohusika katika kuudidimiza mradi huo wa Nyakahura.
 Mkazi wa Wilaya ya Biaharamulo, Yohana Kanyahugali akioba msaada wa Seikali kwajengea shule jamii ya wafugaji na wakulima  ambao wanateseka kwa kwa kutokuwa na majengo  ya shule na kusafiri umbali mrefu kwenda shule.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wananwake wa CCM (UWT), Kijiji cha Busili, wilayani  Biaharamulo, Mamatandu Mniko, akilalamika mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtuhumu Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Busili kwamba ni mnyanyasaji kwa wananchi kiasi cha kuwasweka sero watu wasio na hatia, tuhuma ambazo zilizpingwa vikali na mwenyekiti wa kijiji hicho, Enock Kuhindwa ambaye alidai kuwa waliosekwa sero akiwemo mama huyo walikuwa wamefanya kosa la kutoa na kupokea rushwa ili raia wa Burundi aaandishwe katika Daftari la Wapiga kura.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Busili, Enock Kuhindwa (kulia), akijibu tuhuma hizo zilozoelekezwa kwake na Mwenyenyekiti wa UWT wa  Kijiji cha Busili,Mamatandu Mniko kwamba an atabia ya unyanyasaji wananchini, tuhuma ambazo alizikana.
 Mzee Peter Kalingula, akimuomba Komredi Kinana asidie gharama za ujenzi wa majengo ya shule ya Busili na nyumba za walimu.
 Komredi Kinana akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Meneja Umeme wa Tanesco Wilaya ya Biharamulo, Ernest Milyango kuhusu tatizo la umeme linavyotokea mara kwa mara katika wilaya hiyo wakati alipotembelea mitambo ya umeme ya Biharamulo inayotumia mafuta ya dizeli.
 Komredi Kinana akitembelea mitambo ya umeme ya Biharamulo
 Komredi Kinana akipata maelezo kutoka Mganga msaidizi wa Hospitali ya Wilaya ya Biharamulo. kuhusu ujenzi wa Wodi ya Wazazi.
 Komredi Kinana akitoka kushiriki ujenzi wa Shule ya Kiislamu ya Arahman mjini Biaharamulo
 Wnanchi wakimsalimia komredi Kinana alipokuwa akiwasili kwenye Uwanja wa Soko palipofanyika mkutano wa hadhara mjini Biaharamulo, mkoani Kagera.
 Komredi Kinana wasanii wakitumbiza katika mkutano huo.
 Nape akihutubia katika mkutano huo wa hadhara
Wananchi wakisikiliza kwa makini wakati wa mkutano huo

ziara ya kinana ngara‏

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi wa Benaco waliojitokeza kumpokea alipowasili wilayani Ngara kwa ziara ya kukagua, kuhimiza na kusimamia utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akisalimia wakazi wa Benaco wilayani Ngara.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpatia chanjo mmoja wa watoto katika kituo cha afya cha Nyakisasa, Kashinga wilayani Ngara.
 Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe. John Mongella akizungumza mara baada ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana(kulia) kuzindua chanjo kwa watoto wadogo walio chini ya miaka 5 ambapo watoto wamekuwa wakipewa chanjo ya Vitamini A na chanjo ya Minyoo, Mkuu wa mkoa amehimiza Mama wajawazito pamoja na wenye watoto wasiozidi miaka 5 kuhakikisha wanapata chanjo kwa wakati.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza mara baada ya kuzindua chanjo kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano katika kituo cha afya cha Nyakisasa, Kashinga wilayani Ngara.



 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupanda mti kama ishara yautunzaji mazingira mara baada ya kuzindua chanjo katika kituo cha afya cha Nyakisasa, Kashinga wilayani Ngara mkoani Kagera.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiana na baadhi ya viongozi wa CCM wilaya ya Ngara kuezeka bati katika ofisi ya Tawi la CCM Munjebwe,Ngara mkoani Kagera.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya  Rulenge, Ngara mkoani Kagera.
 Wananchi wa kata ya Rulenge wakisikiliza houba za viongozi kwa makini kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Rulenge wilayani Ngara mkoa wa Kagera.

 Kadi za wanachama waliorudi CCM kata ya  Rulenge ,Ngara mkoani Kagera mara baada ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kumaliza kuhutubia.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo juu ya mradi wa umeme Djuruligwa alipoutembelea wilayani Ngara, mkoa wa Kagera.
 Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe.John Mongella akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kumaliza kuutembelea mradi wa umeme Djuruligwa, katikati ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoka nje ya jengo maalum la kuendeshea pampu za maji katika mradi wa maji Ngara mjini.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga ngoma za asili mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa mikutano Posta ya Zamani ,Ngara mkoani Kagera.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipita kuona na kusabahi vikundi vya ngoma za asili na wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa mkutano Posta ya Zamani Ngara.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake mkoa wa Kagera Revina Jovin akiwasalimu wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa CCM kwenye viwanja vya Posta ya Zamani Ngara ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alikuwa mgeni rasmi.
 Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kagera Ndugu Yahya Kateme akisalimu wananchi wa Ngara kwenye viwanja vya Posta ya Zamani kwenye mkutano wa hadhara wa CCM ambao Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alikuwa mgeni rasmi.
 Wananchi wa Ngara mjini wakimkaribisha Kinana kwenye uwanja wa mkutano.

Mkuu wa Wilaya ya Ngara Ndugu Costantine Kanyasu akisalimia wananchi kwenye mkutano hadhara ambao Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alikuwa mgeni wa heshima.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Ngara mjini ambapo alisisitiza kuwa umoja na mshikamano ndani ya CCM ndio nguzo kuu ya uhai wa chama na pia alisisitiza Siasa isichanganywe na Dini hasa pale yanapozungumziwa mambo ya msingi kama Katiba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Ngara mjini kwenye viwanja vya mkutano Posta ya Zamani ambapo aliitaka serikali kusegeza huduma karibu na jamii badala ya mtu kufunga safari kutoka Ngara kwenda Bukoba mjni kufuata leseni za biashara ama za udereva,Katibu Mkuu aliwahakikishia wananchi wa Ngara kuwa CCM itashinda vizuri na ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu mwezi oktoba mwaka huu.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihojiwa na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara Ngara mjini.
 Wananchi wakimuuliza masali Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya mkutano kumalizika.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na wananchi wa Ngara mjini mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara.
(Picha zote na Adam Mzee)

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa