TMA yatahadharisha wananchi kuhusu ongezeko la joto, Mvua kubwa isiyotabirika yaja, TMA yatahadharisha wananchi

Dar es Salaam. Mvua kubwa isiyotabirika inatarajiwa kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini hasa katika ukanda wa Pwani ya Kaskazini, maeneo ya Dar es Salaam, Tanga, Unguja na Pemba; pia katika ukanda wa Kaskazini Mashariki kwa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara.
Akitoa taarifa ya hali ya hewa jana kwa Januari na Februari mwaka ujao, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk Agness Kijazi alisema mvua ya msimu katika maeneo hayo inatarajiwa kwisha leo.
Hata hivyo, alisema mvua kubwa ya nje ya msimu inatarajiwa katika kipindi cha Januari, 2015. Dk Kijazi alisema hali kama hiyo pia itaikumba mikoa ya Kagera, Mwanza, Shinyanga na Geita.
“Maeneo mengine yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka yatakuwa na mvua ya wastani. Maeneo hayo ni Mbeya, Rukwa, Katavi, Iringa, Lindi, Dodoma na Mtwara.
Dk Kijazi alisema mvua hiyo inasababishwa na ongezeko la joto linalolifanya anga kushindwa kutengeneza unyevunyevu ambao hugeuka kuwa mvua. “Ninawashauri wananchi kuchukua hatua ya kujikinga na athari za kiafya na mazingira zinazoweza kusababishwa na ongezeko la joto linaloendelea sambamba na mvua kubwa inayonyesha,” alisema Dk Kijazi.
Juzi, mvua kubwa ilinyesha jijini Dar es Salaam kwa saa mbili na kusababisha vifo vya watu wawili katika Wilaya ya Kinondoni kuleta kero kwa wasafiri wanaotumia vyombo vya moto na watembea kwa miguu.
Mitaa ya Azikiwe, Bibi Titi na Morogoro ambayo juzi ilijaa maji, jana ilionekana kuwa mikavu baada ya maji yote kukauka.
huku watumiaji wa barabara wakiendelea na shughuli zao kama kawaida.
Yusuph Said, mmoja wa wafanyabiashara wa magezeti Mtaa wa Azikiwe, alisema eneo hilo hujaa maji kila mvua inaponyesha na kuwasababishi kufanya kazi yao katika mazingira magumu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura aliliambia gazeti hili jana kuwa hakuna madhara zaidi yaliyotokea ukiacha matukio ya watu wawili kufariki dunia kutokana na mvua hiyo.
Naye Kamanda wa Polisi Ilala, Mary Nzuki alisema: “Mkoani kwangu sijapokea taarifa yoyote ya maafa yaliyosababishwa na mvua mpaka sasa.” Kamanda Kihenya Kihenya wa Mkoa wa Kipolisi Temeke naye alisema hajapokea taarifa yoyote ya maafa.

Akizungumzia matukio ya mvua kipindi cha Oktoba – Disemba, 2014, Dk Kijazi alisema maeneo mengi ya nchi yalipata mvua za wastani hadi juu ya wastani isipokuwa maeneo machache ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Dodoma (Hombolo), Kilimanjaro (Same), Njombe, Mtwara na Lindi ambayo yalipata mvua za chini ya wastani.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa matukio ya mvua hizo ambayo yaliambatana na vipindi vifupi vya upepo mkali, yalisababishwa na kuimarika kwa ukandawa mvua magharibi mwa nchi ambao uliambatana na kuwepo kwa makutano ya upepo.
“Wananchi wajenge pia utamaduni wa kupanda miti ili kusaidia kupunguza kasi ya upepo unaombatana na mvua kubwa ambazo zinaweza kusababisha uharibifu wa mali na madhara kwao,” alisisitiza Dk Kijazi.
Peter Elias, Bakari kiango na Hadija Salum wa Mwananchi

BUNGE "RUBBER STAMPED" IPTL PROPOSAL



THE resolution passed by the National Assembly to nationalise the Independent Power Tanzania Limited (IPTL) was a rubber stamp of a proposal earlier given by Standard Chartered Bank (Hong Kong) Limited, it has been learnt.

It had been revealed that Standard Chartered Bank wrote to the then Chief Executive Officer of the Tanzania Electric Supply Company Limited (Tanesco), Dr Idris Rashid, proposing the nationalisation of IPTL so that it could be paid a sum of 112 million US dollars.

The letter, dated September 22, 2009, shows that the bank proposed to Tanesco’s legal advisers that the government of Tanzania immediately considers nationalisation of IPTL and that move would be with the support of the bank and with the express objective of implementing the agreed plan.

“If nationalisation was to be agreed upon and implemented, then the whole process could be conducted through the Tanzanian Parliament.

There would be no need to involve courts,” reads a section of the letter in question. The bank alleged in the letter that it believed it has been treated unfairly and inequitably before Tanzanian courts and therefore, was firmly of the view that any attempt to implement its agreed plan through the office of the provisional liquidator of IPTL at the time, would suffer the same fate.

It wrote further that rather than seeking to resolve its claims through international litigation and in light of the progress made with Tanesco on the agreed plan, the bank was prepared to give an opportunity for an early settlement through a consensual nationalisation.

“Accordingly, the bank and its lawyers would, if asked, work with you (Dr Rashid) and your legal advisers in an effort to secure the approval of the committee to a nationalisation proposal, within the next 14 days,” the letter further explains.

The bank went on to propose that the matter could be passed from there to the Cabinet for it to deliberate and with the approbation of the Cabinet, a bill could be placed before Parliament within a timetable consonant with Tanesco’s desire to dispatch power from the project.

“If Tanesco and government of Tanzania manifest a real desire to see a nationalisation achieved quickly and absent any avoidable delay, it can count on full support of the Bank, which would not in such circumstances, see any need to take matters further in any international forum,” the Bank’s letter says.
On November 29, this year, while deliberating the Escrow Account Saga, the National Assembly passed eight resolutions, including a proposal to the government to nationalise the IPTL power plant so that it becomes state owned company through Tanesco.

Addressing the nation through elders from Dar es Salaam Region, President Jakaya Kikwete ruled out the possibility to nationalise the power plant, saying such attempt would jeopardise the government’s good intention of encouraging foreign investment in the country.

SOMA HOJA ZA WAZIRI TIBAIJUKA KWANINI HATAKI KUJIUZULU JUU YA SAKATA LA ESCROW

  HOJA ZA MSINGI ZA PROFESA ANNA KAJUMULO TIBAIJUKA KWA NINI HAONI MANTIKI YA KUJIUZULU WALA KUWAJIBISHWA- UJUMBE MFUPI
1. Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), inayoongozwa na Zitto Kabwe hakuniita ili kupata nafasi ya kujitetea, kutokana na shutuma ambazo zimekuwa zikielekezwa kwangu, kwamba nilipewa fedha kupitia akaunti ya Escrow.

2. Kujiuzulu sio fasheni, kwa kuwa fedha nilizopata ni kwa ajili ya mchango wa shule ya Barbro Johansson ya jijini Dar es Salaam na kujiuzulu ni kitu ambacho kina sababu zinazohitaji uwajibikaji. Nijiuzulu kwa kuwa nimepata mchango wa shule?

3. “Nijiuzulu kwa sababu gani?… kwa kupata mchango wa shule!… kujiuzulu ni kitu chenye sababu zake, kujiuzulu sio fasheni, lazima kuwe na sababu, hata Rais aliyenipa kazi atashangaa. Naona ufahari kufanikisha mchango wa shule yangu.

4. Aidha, serikali haijatamka kama James Rugemalira ana fedha haramu na kama fedha hizo, zikitajwa kuwa za haramu, shule yangu itazirudisha, kwa kuwa shule yangu haiwezi kupokea fedha iliyo haramu.

5. “Nilipostaafu kazi UN, Sweden waliniambia kuwa sasa naweza kuendelea kuomba mchango katika nchi yangu na ni kweli kwamba kadri taifa linavyokua wapo watu wenye uwezo na wanaoweza kuchangia katika masuala mbalimbali,” alisema na kuongeza kuwa ndio maana alianza kuomba michango kwa watu mbalimbali wakiwamo wa ndani ya nchi. 
Na kutokana na kuomba mchango, hata Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi aliwahi kutuchangia Sh milioni 278 kwa kuona umuhimu wa kuendeleza elimu ya mtoto wa kike na mwaka 2012, ndipo nilipomuomba mchango James Rugemalira kupitia kampuni yake ya Mabibo akiwa kama ndugu yake.

6. Nilipomwandikia Rugemalira, alinjibu nitachangiwa, lakini kwa masharti ya kwamba fedha hizo zipitie Benki ya Mkombozi. Na mimi sikuwa na akaunti katika benki hiyo na Februari 23 mwaka huu ndipo nilifungua na haukupita muda mwingi alinipigia na kuniambia kuwa tayari ameshachangia.
 Baada ya kupata mchango huo, niliwapigia viongozi wa Bodi ya shule kuwaeleza kwamba wamepata mchango `babu kubwa’ na alihamisha fedha hizo na kuzipeleka Benki M kwa ajili ya kulipa mikopo ya shule.

7. Profesa Tibaijuka anasema: “Nimejitolea maisha yangu kutafuta wafadhili kwani ada za shule hizo ni kubwa kwani ya Dar es Salaam ni Sh milioni nne na nusu na ile ya Bukoba ni Sh milioni mbili huku pakiwepo pia wanafunzi ambao hawalipi ada wakipatiwa ufadhili.” 
Chanzo: Jiachie Blog

KAGERA KUJIVUNIA UWANJA WA NDEGE WA KISASA

Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwasili kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kagera kujionea maendeleo ya Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja hicho. Waliotangulia mbele ni Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto), Meneja Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba, Mhandisi Suleiman Athuman (Katikati) na Meneja wa kiwanja hicho, Bw. Julius Mulungwana (Kulia)
Ujenzi unaendelea! Mafundi wakiendelea na ujenzi wa jengo la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kagera.
Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa kiwanja hiko, Mhandisi Pius Gobolo akitoa maelezo ya namna ya kiwanja hicho kitakavyoonekana mara kitakapokamilika. PICHA NA SAIDI MKABAKULI

Na Saidi Mkabakuli, Kagera
Mkoa wa Kagera na maeneo ya jirani wataanza kujivunia uwanja wa ndege wa kisasa kufuatia kukamilika kwa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba.
Akizungumza na Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo toka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Meneja Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kagera, Mhandisi Suleiman Athuman, amesema kwamba maendeleo ya ujenzi wa jengo la abiria la kiwanja hicho upo kwenye hali nzuri na mkandarasi atabidhi kazi hiyo mapema mwakani.
“Katika mwaka wa fedha wa 2013/14 kazi zilizopangwa ni ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya kiwanja, ikijumuisha barabara ya kuruka na kutua ndege, maegesho ya ndege, barabara ya kiungio, kwa sasa ujenzi unaendelea vizuri na Mkandarasi atatukabidhi kazi mapema mwakani,” alisema Mhandisi Athuman.
Akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Kiwanja cha Bukoba, Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa kiwanja hiko, Mhandisi Pius Gobolo amesema kuwa kazi za usimikaji wa mfumo wa taa za kuongozea ndege, ujenzi wa jengo jipya la abiria na uzio wa usalama zimeshakamilika kwa asilimia 80.
“Kama unavyojionea, sehemu kubwa ya kazi imekamilika, kwa makadirio ni zaidi ya asilimia 80 ya ujenzi wa kiwanja hiki imeshakamilika,” aliongeza Mhandisi Gobolo.
Kwa mujibu wa mpangokazi wa ujenzi wa kiwanja hicho hadi kufikia mwezi Juni 2014, hatua iliyofikiwa ni pamoja na kukamilika kwa ukarabati wa barabara ya kuruka na kutua ndege, barabara ya kiungio na maegesho ya ndege kwa kiwango cha lami; na ujenzi wa jingo jipya la abiria kufikia hatua ya usimikaji wa paa na mifumo ya maji safi, maji taka na umeme; na kuendelea kwa ujenzi wa jengo la abiria na kituo cha umeme.
Naye, Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri amesema kuwa Serikali imeazimia kuendelea kuboresha miundombinu ya viwanja vya ndege hususan miradi iliyoibuliwa katika Programu ya Matokeo Makubwa Sasa.
“Kwa mujibu Programu ya Matokeo Makubwa Sasa, serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini ipo kwenye mkakati wa kuuendeleza viwanja vya ndege vyote ili viwe na kiwango kizuri kwa watumiaji wa viwanja hivyo,” alisema Bibi Mwanri.

RC: NATAKA USHINDI KESI FEDHA ZA JK

SERIKALI mkoani Kagera imemtaka mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, Colnery Ngudungi kuhakikisha halmashauri hiyo inashinda kesi inayohusu upotevu wa kiasi cha Sh milioni 30.
Fedha hizo ni sehemu ya Sh milioni 150 zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya mradi wa maji Kibimba wilayani humo.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera John Mongella, alipofanya ziara katika eneo la mradi huo unaojengwa kwa ajili ya matumizi ya maji kwa wananchi wa mji mdogo wa Ngara ikiwemo hospitali teule ya wilaya iitwayo Mulugwanza.
Alitoa kauli hiyo baada ya kupata taarifa kwamba kuna mradi wa maji ambao fedha yake ilitolewa na Rais Kikwete, lakini kuna watu wameuhujumu.
Kutokana na taarifa hiyo, RC huyo aliamua kwenda kukagua mradi huo na kujionea maendeleo yake, ikiwa ni sambamba na kupata maelezo kutoka kwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo Ngudungi.
Mkurugenzi alitoa maelezo kwa mkuu huyo wa mkoa ambapo alisema halmashauri hiyo iliomba kiasi cha Sh milioni 200 kwa ajili ya kuboresha miundombimu ya maji mjini Ngara na Rais Kikwete alipofanya ziara wilayani humo mwezi Julai mwaka jana aliahidi kuchangia mradi huo kiasi cha Sh milioni 150.
Alisema Rais alituma kwanza kiasi cha Sh milioni 50 na mara ya pili ilitolewa Sh milioni 100. Alisema fedha hiyo ilitumwa kupitia akaunti ya mamlaka ya maji Ngara jambo lililompa mwanya aliyekuwa Meneja wa mamlaka hiyo, Edward Magai kujichotea kiasi cha Sh milioni 32.
Alisema ili mradi huo ukamilike una unahitaji Sh milioni 43 na baraza la madiwani limeishakaa vikao na kuazimia kuwa hizo fedha zipatikane na kumalizia mradi huo ili kupunguza adha ya ukosefu wa maji katika mji huo ambao wananchi hufuata maji zaidi ya kilometa saba.
Kutokana na maelezo hayo mkuu wa mkoa alitoa agizo halmashauri itafute fedha hizo ili mradi ukamilike lakini pia akaagiza kuhakikisha kesi iliyoko mahakamani halmashauri inashinda.
Chanzo;Habari Leo

KCU WACHAGUA VIONGOZI WAPYA, ‘WATOSA’ WA ZAMANI

CHAMA Kikuu cha Ushirika, Mkoa Kagera (KCU 1990) LTD, kimefanya mabadiliko ya kuwachagua viongozi wapya na kuwatupa wa zamani katika Mkutano Mkuu Maalum.
Uchaguzi huo umefanyika jana chini ya usimamizi wa Mrajisi Msaidizi wa Mkoa Kagera, Rweikiko Shorosi, ambaye alisema serikali inapenda kuona vyama vya ushirika vikifanya vizuri
Alibainisha migogoro inayovikumba vyama vya ushirika vinakwamisha harakati za wananchi kutafuta fursa za kujiwezesha kimaendeleo.
Akisoma majina ya watu waliojitokeza kuchukua fomu  ya kuwania nafasi ya Wajumbe wa Bodi ya KCU 1990, katika Mkutano Mkuu maalum uliofanyika mjini hapa, Shorosi alisema  waliojitokeza kuchukua fomu walikuwa 22
Alisema  majina yaliorudi baada ya kuchujwa ni 18  wote ni sura mpya tofauti na walivyotarajia watu wengi
“Haya majina ndiyo yaliyofikisha asilimia 50 na kuendelea na hivyo, nitasoma majina ya wale waliofuzu vigezo ya kamati iliokaa kuyajadili “alisema.
Katika uchaguzi huo kila Wilaya ilitoa wagombea wa wajumbe wa bodi ambapo katika wilaya za Muleba, Halmashauri ya Bukoba, Missenyi walitoa wagombea zaidi ya wanne huku Manipaa ya Bukoba ikitoa wagombea wawili.
Katika nafasi ya Mwenyekiti wagombea walikuwa wawili ambao ni Frank Muganyizi, aliyepata kura 189 kati ya 246 zilizopigwa na Sylvanus Muhyoza, aliyepata kura 50 hivyo, Muganyizi kutangazwa kuwa Mwenyekiti Mpya wa Bodi hiyo.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilikuwa inawaniwa wajumbe watatu Festo Paulo aliyepata kura 31, Sandru Nyangasha aliyepata kura 78, na Ingatus Batanuzi aliyewashinda kwa kupata kura 136.
Wajumbe wapya wa bodi hiyo waliochaguliwa na Mkutano Mkuu ni pamoja na  Winfrida Kyombo aliyepata kura 102 kutoka Wilaya ya Missenyi na Festo Paulo kura 56, wajumbe kutoka Bukoba mjini ni Sylvanus Muyoza aliyepata kura 227.
Wajumbe kutoka Wilaya ya Muleba ni pamoja na Ignatus Batamuzi aliyepata kura 133, na Projestus Balengela aliyepata kura 44.
Wilaya ya Bukoba waliochaguliwa ni pamoja na sandru Nyangasha aliyepata kura 60 na Frank Muganyizi aliyepata kura 90, pia wajumbe hao walimchagua Dominick Kasaju kutoka Chama cha msingi Bukwali wilayani Missenyi kuwa mwakilishi kutoka nje ya bodi ambapo alipata kura 182.
Akizungumza baada ya uchaguzi huo Mrajis Msaidizi, Moshi Chogero, alisema uchaguzi huo umefanyika kwa mujibu wa sheria namba sita ya mwaka 2013 ni wa uhuru na haki.
Alisema kwa wajumbe ambao walichukua fomu na kujaza lakini majina yao hayakuweza kurudi wanaweza kukata rufaa kwa mrajisi kwani ni haki yao ya kidemokrasi kufanya hivyo.
Chanzo;Tanzania daima

HALMASHAURI ZAAGIZWA KUHAKIKI WAKANDARASI

HALMASHAURI za wilaya zimeagizwa kuunda kamati ndogo kwa ajili kuhakiki wakandarasi waliopewa zabuni za kutengeneza barabara.

Agizo hilo lilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Enosi Mfuru, katika kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika Manispaaa ya Bukoba.

Alisema uhakiki na ukaguzi huo utasaidia kuondoa tatizo la wakandarasi kujenga barabara chini ya kiwango na kulipwa fedha, hali inayochangia kuzisababishia hasara halmashauri na serikali kwa ujumla.

Mfuru alisema ukaguzi huo utasaidia kupunguza malalamiko yaliyoanza kujitokeza kuwa baadhi ya barabara zinatengenezwa chini ya viwango na kusababisha kushindwa kupitika muda mfupi baada ya kutengenezwa.

“Halmashauri zihakikishe kila kijiji kinaweka ulinzi katika barabara hilo, ili kuweza kuzilinda hasa zile za Stabex zilizokuwa zinahudumiwa na jumuiya hiyo kutoka Ulaya, kwani mkataba wake umekwisha zitunzwe kama zamani kabla ya msaada huo,” alisema Mfuru.
Aliwakataza wale ambao wameanza kuchimba madini karibu na barabara hizo, kwani wamekuwa wakisababisha uharibifu wa barabara na kuwataka watafute sehemu nyingine.

Meneja wa TanRoads mkoani hapa, Jonh Kalupale, alisema jumla ya sh bilioni 6 ziliidhinishwa kwa ajili ya matengenezo ya barabara kuu za mkoa katika mwaka wa fedha 2008/09. Kati ya hizo sh bilioni 3.6 ni kwa ajili ya kuhudumia barabara kuu zenye urefu wa kilomita 468.62 na madaraja 126.

Aidha, Kalupale alikiomba kikao hicho kwa kupitia kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kuwawekea ulinzi wa kutosha makandarasi wanaofanya kazi katika mapori ya Burigi Kasindaga na Kimisi, ili kulinda mali zao na usalama wao kwa ujumla 
 Chanzo;Tanzania Daima

BANDARI YA KASANGA KUANZA KUBORESHWA


Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Watatu kushoto) akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Bandari ya Kasanga, Bw. Mponjoli Thompson Mwamafupa (Kulia) mara walipowasili katika bandari hiyo kujionea shughuli mbalimbali za maendeleo bandari hapo.
Mkuu wa Bandari ya Kasanga, Bw. Mponjoli Thompson Mwamafupa (Kushoto) akiwaongoza wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kujionea moja ya meli za kigeni zinazotia nanga katika bandari hiyo. Meli hiyo ni MV Rwegura kutoka nchini Burundi.
 Mkuu wa Bandari ya Kasanga, Bw. Mponjoli Thompson Mwamafupa (Kulia) akiwaonesha maghala ya kuhifadhia mizigo katika Bandari ya Kasanga. Maghala hayo yalifunguliwa rasmi na Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilali tarehe 22 Februari 2012
 Mkuu wa Bandari ya Kasanga, Bw. Mponjoli Thompson Mwamafupa (Kushoto) akimfafanualia jambo Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kulia) wakati akimkabidhi taarifa ya maendeleo ya bandari hiyo.
 Mkuu wa Bandari ya Kasanga, Bw. Mponjoli Thompson Mwamafupa (Kulia) akitoa ufafanuzi juu ya namna bandari yake inavyohudumia meli kutoka nchi jirani. Wanaomsikiliza ni Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiongozwa na Bibi Florence Mwanri (Kushoto aliyevaa fulana nyeusi).

Mkuu wa Bandari ya Kasanga, Bw. Mponjoli Thompson Mwamafupa (Kushoto) akiongea na wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kuhusu namna ya kuhudumia meli kutoka nje ya nchi.
 Mkuu wa Bandari ya Kasanga, Bw. Mponjoli Thompson Mwamafupa (Kulia) akitoa ufafanuzi juu ya namna bandari yake inavyohudumia meli kutoka nchi jirani. Wanaomsikiliza ni Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiongozwa na Bibi Florence Mwanri (Kushoto aliyevaa fulana nyeusi)
 Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwa katika picha ya pamoja katika jiwe la msingi la uzinduzi wa maghala ya kuhifadhia mizigo katika Bandari ya Kasanga. Maghala hayo yalifunguliwa rasmi na Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilali tarehe 22 Februari 2012.
 Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwa katika picha ya pamoja katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) zilizopo kwenye Bandari ya Kasanga.
---
Na Saidi Mkabakuli, Sumbawanga
Serikali imeazimia kuanza kuiboresha bandari ya kimkakati ya Kasanga inayohudumia nchi za Burundi, Rwanda na Kongo iliyopo katika Ziwa Tanganyika, mkoani Rukwa.
Ahadi hiyo imetolewa na Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miundombinu katika Bandari ya Kasanga.
Bibi Mwanri alisema kuwa serikali kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania imepanga kuboresha bandari zote ili kuwa malango kuu la biashara kwa soko la ndani na kwa nchi jirani ili kuongeza uwezo wa kuhudumia shehena kwa ufanisi.
“Tumedhamiria kuendelea kuboresha miundombinu ya bandari hususan miradi iliyoibuliwa katika Programu ya Matokeo Makubwa Sasa ikiwemo Bandari ya Kasanga ili kuweza kukidhi mahitaji ya utoaji wa huduma katika eneo hili,” alisema.
Bibi Mwanri aliongeza kuwa serikali pia imejipanga kuendelea kuboresha miundombinu na ununuzi wa vifaa mbalimbali vya kuhudumia shehena katika bandari za Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, Kasanga na Kigoma na kukamilisha maandalizi ya ujenzi wa bandari mpya za Mwambani (Tanga), Mbegani (Bagamoyo) na Bandari Kavu ya Kisarawe.
Akizungumza na ugeni huo, Msimamizi Mkuu wa Bandari ya Kasanga, Bw. Mponjoli Thompson Mwamafupa alisema kuwa Bandari hiyo ina fursa nyingi katika kuhudumia shehena na abiria wanaopitia bandarini hapo.
“Bandari yetu ina fursa kubwa za kibiashara kwani tuna wateja wengi kutoka ndani na nje ya nchi wanaotumia bandari yetu kupitishia bidhaa zao, pamoja na abiria wanaosafiri kwenda nje na ndani ya Tanzania,” alisema.
Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo kwa mwaka ujao wa fedha Serikali imedhamiria kuboresha mazingira yatakayowezesha sekta binafsi kuwekeza katika kujenga miuondombinu na kuboresha usafirishaji wa mizigo katika bandari zote nchini.
Pia, Mpango huo unaweka bayana kuendeleza na ukarabati na ununuzi wa vyombo vya usafiri na usafirishaji katika maziwa.
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa