WILFRED LWAKATARE (CHADEMA) ATANGAZWA KUWA MBUNGE WA BUKOBA MJINI



Hatimaye Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chama cha demokrasia na maendeleo -Chadema Bw. Wilfred Muganyizi Lwakatare ameibuka kidedea na kuwa Mbunge wa Bukoba Mjini dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kwa tiketi ya CCM, Khamis Kagasheki. Matokeo hayo yalitangazwa usiku na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini Bw. Aron T. Kagurumjuli. Kura za Udiwani Chadema/ Ukawa imeshinda Kata zifuatazo: Kahororo, Kagondo, Kibeta, Kitendaguro, Nshambya, Hamugebe, Kashai, Bakoba na Bilele. CCM imepata Kata ya Rwamishenye, Buhembe, Miembeni, Nyanga na Ijunganyondo. Picha na Faustine Ruta, Bukoba

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini Bw. Aron T. Kagurumjuli akitoa matokeo usiku wa jana majira ya saa 2:30 usiku mara baada ya kumalizika kuhesabu kura zilizopigwa jimboni hapo na kumtangaza Lwakatare kwamba ndie mshindi na Nafasi hiyo ya Ubunge Bukoba Mjini. 
Bw. Aron T. Kagurumjuli (Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini) akiendelea na zoezi la kutangaza matokeo usiku huu.
Mshindi wa nafasi ya Ubunge wa Bukoba Mjini Bw. Wilfred Muganyizi Lwakatare kupitia Chama cha CHADEMA akifurahia baada ya kuibuka kidedea katika kinyang'anyiro hicho baada ya kumwangusha mgembea mwenza aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo la Bukoba Mjini kwa tiketi ya CCM, Khamis Sued Kagasheki jana usiku.

LICHA ya kuonekana kana kwamba hapakuwa na dalili zozote za fujo wakati wa zoezi la upigaji kura za Ubunge na udiwani, hali ilibadilika jana jumatatu asubuhi baada ya wafuasi wa chama cha Chadema kutaka matokeo mapema baada ya kupata matokeo hayo usiku wa kuamkia jana kuwa Chadema imeshinda katika Kata 9 kati ya 14 wafuasi hao waliandamana katika maeneo ya mji wa Bukoba wakitaka majibu yatolewe mapema. Kitu ambacho hakikufanyika na kupelekea kuleta ghasia jimboni hapo. Hali hiyo ilisababisha polisi wa kutuliza ghasia kuingilia kati na kuwatawanya wafuasi wa chama cha Chadema ambao mpaka usiku wa jana walikuwa wamejaa katika eneo la ofisi za Halmashauri ya Bukoba Mjini waishinikiza matokeo kutangazwa. Wafuasi wa chama cha Chadema walisababisha vurugu zikiwemo kurusha mawe na ndipo ndipo jeshi la polisi mjini hapo walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliokusanyika katika Ofisi za Halmashauri. Hali hiyo ilitulia baada ya Viongozi wa Chadema kuwatuliza na ndipo Matokeo yakatangazwa. 

Taarifa zinasema kuwa kulikuwa na mchuano mkali kati ya wagombea hao wawili ambao ni Wilfred Lwakatare wa chama cha Chadema na aliyekuwa Mbunge wa Bukoba Mjini kupitia chama cha CCM Khamis Sued Kagasheki. Kitu kilichopelekea kurudiwa kuhesabiwa kwa kura zote na kupata uhakika wa kutosha.
Kura zilizokubalika ni 54,211 sawa na asilimia 98.54, kura zilizoharibika ni 805 sawa asilimia 1.46, Matokeo ni kama ifuatavyo TLP kura 81 sawa na asilimia 0.2, ACT kura 453, Khamis Sued Kagasheki wa CCM amepata kura 25,565 sawa na asilimia 47.2, Wilfred Muganyizi Lwakatare wa Chadema amepata kura 28,112 sawa na asilimia 51.9Wafuasi wa Chadema walionekana wakiwa wamekusanyika katika Ofisi za Halmashauri Bukoba wakidai kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa huo wa Wabunge.
Waandishi wa habari na Makada wa Chama cha Chadema wakiwa katika Ofisi za Halmashauri ya Bukoba wakisubilia matokeo kutangazwa.
Diwani wa Kata ya Kahororo Chif Kalumuna(kulia)  akiwa amembeba mshindi wa ubunge jimbo la Bukoba Mjini bw. Wilfred Lwakatare mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi.
Wafuasi wa Chadema walionekana wakiwa wamekusanyika kutaka kuvamia Ofisi za Halmashauri ya Bukoba kudai kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa wabunge na Polisi walikuwa tayari kuwakabili vilivyo na kuzuia umati huo mkubwa.
Wafuasi wa Chadema wakitaka Matokeo yatolewa baada ya kuchukuwa muda tangu asubuhi mpaka jioni hii.
Hali ilivyokuwa hapo jana jioni maeneo ya karibu na Ofisi za Halmashauri.
Hapa ikabidi kiongozi wa Chadema aliyeshinda katika Kata ya Kashai kupitia chama hicho awatulize kwamba matokeo yanaenda kutolewa jioni hii.
Wafuasi wa Chadema wakitaka Matokeo
Wafuasi wa Chadema wakitaka Matokeo ya Kiongozi wao.

Lowassa: Mliobaki CCM sasa nifuateni Chadema.

Mgombea wa urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.
Na Jacqueline Massano
Mgombea wa urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, amewataka viongozi na makada wengine waliobaki ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoroka na kujiunga na Chadema kwani hivi sasa ni wakati wa mabadiliko.
 
Lowassa alitoa kauli hiyo jana katika mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Soko jipya wilayani Biharamulo, Mkoa wa Kagera.
 
Lowassa alisema huu ni wakati wa mabadiliko, hivyo aliwaomba viongozi wengine ambao bado wamo ndani ya CCM kujiunga na Chadema.
 
“Kama viongozi wengine bado wapo CCM wanataka kuja Chadema waje ili tuungane katika safari hii ya mabadiliko,” alisema.
 
Aidha, alimpongeza Katibu Mkuu mstaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Balozi Juma Mwapachu, kwa uamuzi wake wa kujiondoa CCM na kujiunga na wana-mabadiliko. 
 
Akizungumzia walimu, Lowassa alisema akiingia madarakani hatataka kusikia mishahara na posho za walimu zinachelewesha.
 
Lowassa alisema akiingia madarakani atahakikisha walimu wanalipwa vizuri ili wawape wanafunzi elimu bora.
 
“Sitaki kusikia kuna mizengwe mizengwe ya walimu kucheleweshewa mishahara au posho,” alisema Lowassa.
 
Aidha, mgombea huyo alisema akiingia madarakani atahakikisha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linaanzisha vyuo vya Elimu ya Ufundi Stadi (Veta) ili vijana wanapomaliza mafunzo wanatoka na utaalamu.
 
“Nataka ndani ya JKT kuwe na vyuo vya ufundi vya kufundisha watu kutengeneza pikipiki, baiskeli hata na magari. Nina imani kwa miaka mitano tutapata wataalamu wazuri,” alisema.
 
Aidha, alimpongeza Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe, kwa kuijenga Chadema, akisema imekuwa imara na yenye nguvu.
 
Kabla ya kuwahutubia wananchi, Lowassa aliwaomba watulie kwa dakika kadhaa kwa ajili ya kumkumbuka Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, ambaye jana Watanzania waliadhimisha kumbukumbu ya miaka 16 ya kifo chake.
 
MBOWE
Mwenyekiti wa Chadema, Mbowe, alisema ilani ya Chadema imeeleza mambo ya msingi ambayo serikali ya Lowassa itayatekeleza. 
 
“Baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 kilikuwa ni kilio cha Chadema cha kuwa na katiba ambayo itawawajibisha viongozi na kusimamia rasilimali za nchi,” alisema.
 
Hata hivyo, alisema Serikali ya Rais Jakaya Kikwete ilipiga vita rasimu ya katiba iliyoandaliwa na iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo ilitokana na maoni ya wananchi. 
 
Aidha, alisema ujio wa Lowassa, Kingunge Ngombale Mwiru na na Frederick Sumaye imekuwa ni baraka kwa Chadema na Watanzania kwa ujumla.
 
KINGUNGE
Kwa upande wake muasisi wa CCM, Kingunge Ngombale Mwiru, alisema huu ni wakati muhimu kwa Watanzania wote kutambua kuwa muda wa kufanya mabadiliko umefika.
 
“Nusu karne imetosha na kwa bahati nzuri uongozi wa sasa wa CCM umeishiwa pumzi, hauwezi kuwaongoza Watanzania tena,” alisema na kuongeza:
 
“Ndiyo maana Lowassa ameondoka, Sumaye ameondoka na mimi Kingunge ambaye hakuna mwingine zaidi yangu nimeondoka CCM, huu ni wakati wa kuiweka CCM benchi.”
 
MASHA
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha, alisema CCM ingeweza kufanya vizuri kama si ufisadi uliopo ndani ya chama hicho ambao unasababisha wapatikane viongozi wasiofaa.
 
“Kinana (Adrulrahman), ndiye wa kwanza kuwaeleza wananchi kuhusu mawaziri mizigo na yeye ndiye anazunguka nchi nzima kukikosoa chama chake,” alisema na kuongeza:
 
“Haya mwisho wake ni Oktoba 25, mwaka huu...ingawa katika kipindi hiki watu wanaweza kuonewa na wengine kuambiwa si raia, lakini lazima yafike mwisho.”
 
Aidha, aliwataka wananchi kutii sheria na kuliheshimu Jeshi la Polisi katika kipindi hiki.
 
“Naomba nyie polisi mkumbuke kuwa na nyinyi ni Watanzania, tunafahamu mpo hapa kwa ajili ya kulinda amani, lakini tunaomba mtumie busara na hekima pia,” alisema Masha.
 
Jana Lowassa alihutubia mikutano ya kampeni katika maeneo ya Biharamulo, Ngara Mjini na Vijijini pamoja na Mbogwe.
 
MBOWE AMJIBU JK
Akiwa katika mkutano wa jana jioni uliofanyika Mbogwe, wilayani Geita, Mbowe alimtaka Rais Kikwete kutovuruga amani ya nchi na badala yake aondoke salama.
 
Alisema Rais Kikwete aondoke madarakani salama kama walivyofanya marais wenzake wastaafu.
 
“Rais Kikwete ameamua kuwa mpiga debe wa Magufuli (mgombea wa CCM), sasa mimi naomba nimjibu yeye kama mpiga debe na si rais,” alisema.
 
Alisema Rais Kikwete ameamua kuwaaminisha  Watanzania kuwa wapiga kura wapo milioni 28 badala ya milioni 22 kama ilivyotangazwa na Tume ya Taifa ya Taifa ya Uchaguzi (Nec).
 
“Sasa nataka kumuuliza Rais Kikwete hao wapiga kura wengine milioni sita wametoka wapi?” alihoji Mbowe na kuongeza:
 
“Naomba kumwambia Rais Kikwete kuwa hii nchi si yake, hii nchi si ya CCM na hii nchi si ya familia yake...hii ni nchi ya Watanzania,” alisema.
 
Alisema hatua ya Rais Kikwete na CCM inayoungwa mkono na Nec kuwataka wananchi wapige kura na kuondoka vituoni haiwatendei haki Watanzania.
 
“Kikatiba Watanzania wana haki ya kulinda kura zao kwa sababu zile ni kura zao, nashangaa Rais Kikwete anawaambia watu waondoke,” alisema.
 
Mbowe, aliwaomba Watanzania wote kwenda kwenye vituo kwa ajili ya kupiga kura ikiwa ni pamoja na kuzilinda kura zao.
 
Pia alisema anashangazwa na kauli ya Rais Kikwete ya kuliagiza Jeshi la Polisi kuwaondoa wananchi kwa nguvu katika vituo vya kupigia kura.
 
“Hao askari walioagizwa na Rais Kikwete, nao wana watoto na familia zao, naomba nikwambie Rais Kikwete kuwa huwezi kuzuia mabadiliko. Zimebaki siku 11, Mungu atajibu maombi yetu...nawaambia wananchi nendeni mkapige kura kaeni mita 200 lindeni kura zetu,” alisema.
 
CHANZO: NIPASHE

DW YAKANUSHA UJUMBE UNAOSAMBAA FACEBOOK NA WHATSAPP

Idhaa ya kiswahili ya DW hapa nchini inapenda kuwataarifu kuwa Wapendwa wake na watumiaji wa ukurasa wetu wa Facebook na wasikilizaji kwa jumla.


Kuna ujumbe unaosambazwa kwa njia wa Whatsapp katika mitandao ya kijamii kwamba DW inakusanya maoni kuhusu wagombea wawili wakuu wa uchaguzi wa Tanzania, John Magufuli wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Edward Lowassa anayewakilisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA). Tungependa kuwajulisha hatufanyi utafiti wowote wa maoni kuhusu wagombea hao.

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa