Bw. Charles Kato Meneja wa Mpango wa USAID Boresha Afya Mkoa wa Kagera
(Kushoto) Akimkabidhi Vifaa vya Afya Mkuu wa Wilaya Bukoba Mhe. Deodatus
Kinawilo Aliyevipokea Kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu.
Bw. Charles Kato Meneja wa Mpango wa USAID Boresha Afya Mkoa wa Kagera (Kushoto) Akimkabidhi Vifaa vya Afya Mkuu wa Wilaya Bukoba Mhe. Deodatus Kinawilo Aliyevipokea Kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu.
Picha ya Pamoja Mara baada ya Vifaa Kukabidhiwa
Bw. Charles Kato Meneja wa Mpango wa USAID Boresha Afya Mkoa wa Kagera (Kushoto) Akimkabidhi Vifaa vya Afya Mkuu wa Wilaya Bukoba Mhe. Deodatus Kinawilo Aliyevipokea Kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu.
Picha ya Pamoja Mara baada ya Vifaa Kukabidhiwa
Serikali
Mkoani Kagera yapokea vifaa vya Afya vyenye thamani ya shilingi Milioni
Kumi kutoka kwa wadau wa maendeleo wa mpango wa USAID Boresha Afya ambao ni
wadau muhimu katika Sekta ya Afya kwa Mkoa wa Kagera.
Vifaa
hivyo vilikabidhiwa na Meneja wa mpango wa USAID Boresha Afya Mkoa wa Kagera
Bw.Charles Kato katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Agosti 21, 2017 ambapo
vilipokelwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo kwaniaba ya Mkuu wa
Mkoa wa Kagera Mhe. Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu.
Akikabidhi
vifaa hivyo Bw. Kato alisema ni mahsusi kwa kituo cha Afya Kabyaile ambacho
kimejengwa upya na Serikali baada ya kile cha awali kuharibiwa na Tetemeko la
Ardhi mwaka jana Septemba 10, 2017.
Aidha,
Dk. Kato alisema kuwa vifaa vimetolewa na Mpango wa USAID Boresha Afya ambao
unatekelezwa katika Wilaya ya zote za Mkoa wa Kagera. “Mpango huu wenye malengo
ya kuchangia juhudi za Serikali za kuboresha Afya ya Mama na mtoto unafadhiliwa na USAID na PATH pamoja na
Serikali.” Alifafanua Bw. Kato
Pia
Bw. Kato alisema kuwa vifaa hivyo vimetolewa kwa lengo la kuchangia mikakati ya
Serikali ya kuhakikisha kituo kipya cha Kabyaile kinatoa huduma bora hasa kwa
wakina mama na watoto.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bukoba Deodatus Kinawilo kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa
Kagera aliwashukuru wadau hao waliotoa vifaa hivyo na kusema kuwa Serikali
itaendelea kushirikiana nao ili kuboresha huduma za wananchi hasa wakina mama
na watoto katika Mkoa wa Kagera.
Kwaniaba
ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Deodatus Kinawilo alikabidhi vifaa hivyo kwa
Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Kanali Denice Mwila ambaye naye alitoa shukrani za
Wilaya yake kwa USAID Boresha Afya kuwa
wamekuwa wadau wapili kutoa msaada wao katika Kituo cha Kabyaile baada ya Benki
ya NMB nao kutoa msaada wao na kutoa wito kwa wadau wngine kujitolea.
Vifaa
vilivyotolewa ni Seti moja ya vifaa vya upasuaji wakati wa kujifungua, Seti
moja ya vifaa vya kuzalisha, Mashine moja ya utakasaji wa vifaa, Seti mbili za
kumsaidia mtoto kupumulia na kitanda kimo cha kujifungulia.
Chanzo BukobaWadau
Chanzo BukobaWadau
0 comments:
Post a Comment