Home » » SABABU UZALISHAJI MAZAO DUNI ZATAKWA

SABABU UZALISHAJI MAZAO DUNI ZATAKWA


MAGONJWA na visumbufu vinavyoshambulia mazao mkoani Kagera husababisha wakulima kuzalisha mazao duni ya ndizi, maharage, mahindi na mihogo na kushindwa kufikia hitaji la kiwango cha mkoa.
Hayo yalisemwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Diwani Athuman, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha maonyesho ya Nanenane kwa niamba ya Mkuu wa mkuoa huo, Meja Jenerali mstaafu, Salimu Kijuu katika viwanja vya Kyakailabwa Manispaa ya Bukoba juzi.

Athumani alisema ili kutatua changamoto hizo, wakulima wanapaswa kushirikiana na wataalamu wa kilimo ambao ndio wanaoweza kutambua visumbufu vya magonjwa kwa kuwatembelea katika mashamba yao na kuwapatia elimu.

“Njia rahisi ya kuwafikiwa ni kukaa kwenye vikundi na kujiunga pamoja muweze kupatiwa elimu kutoka kwa wataalamu kwani ndio wenye kutambua tatizo la visumbufu hivyo,” alisema Athumani.

Aidha, alisema vikundi vya Saccos, AMCOS vinaweza kutoa mikopo ya kuwawezesha kuendeleza na kuinua kilimo pamoja na kukabiliana na visumbufu.

Hata hivyo, alisema mkoa huo unazalisha kwa kiwango cha chini ambapo ndizi huzalishwa tani 3.5 kwa ekari, mahindi huzalishwa ni tani 0.8 kwa ekari 1.6, mhogo huzalishwa tani 20 maharage tani moja kwa ekari.

Aliongeza kuwa utumiaji wa teknolojia unahitajika kwa ajili ya kuzalisha mazao ya chakula na ya biashara, hivyo kufikia uchumi wa viwanda.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa