MKUU WA MKOA WA KAGERA ATOA MAAGIZO MAKALI KWA WANANCHI NA WATENDAJI WA SERIKALI WANAOENDELEA KUKAIDI MAAGIZO YA RAIS MAGUFULI

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu wa Pili Kutoka Kulia Akisikiliza Maelezo Kutoka kwa Mhifadhi wa Msitu wa Biharamulo Mrefu Kuliko Wote
  Baadhi ya Eneo la Msitu wa Biharamulo Lililoharibiwa Kwa Kuchoma Mkaa
 Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe. Kijuu Akiongea na Wananchi wa Nemba Biharamulo
 Mkuu wa Mkoa na Msafara Wake Wakiangalia Eneo Lililozibwa na Mwananchi na Kuzuia maji kutiririka kufuata Mkondo wakae katika Msitu wa Nyantakara Karibu na Kijiji Mpago
 Huyo ndiye anajiita Balozi wa wananchi walioanzisha makazi katikati ya Msitu Nyantakala makazi yanyoitwa MOBASA RAHA​
 Eneo Hili Mwananchi anachimba mtaro kuizuia maji yasifuate mkondo wake Mkuu wa Mkoa Kijuu aliagiza eneo hilo kurekebishwa na kurudia katia hali ya ya zamani mara moja

Na: Sylvester Raphael

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu afanya ziara katika Misitu ya Hifadhi ya Biharamulo na Nyantakala Wilayani Biharamulo kuona kama agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli wavamizi wa misitu hiyo kuondoka mara moja alilolitoa tarehe 19 Julai, 2017 alipofanya ziara yake Mkoani Kagera.

Rais Magufuli akiwa Wilayani Biharamulo Julai 19, 2017 aliagiza wavamizi wote wa Misitu ya Asili na Wafugaji waliovamia Mapori ya Akiba kuhakikisha wanaondoka mara moja katika hifadhi na watakaokaidi wachukuliwe hatua za kisheria.

Hatua hiyo ilitokana na operesheni ondoa mifugo iliyofanyika Mkoani kagera kunusuru Misitu ya asili, mapori ya akiba na vyanzo vya maji ambavyo vilikuwa vimevamiwa na kuharibiwa kwa kiwango kikubwa kwa kukata mkaa, kuendesha kilimo na kuingiza mifugo katika Misitu na Mapori ya Akiba.

Mkuu wa Mkoa Mhe. Kijuu akitembelea Misitu ya Biharamulo na Nyantakala Wilaya Biharamulo Agosti 22, 2017 bado alikuta shughuli za uharibifu wa uchomaji wa mkaa katika misitu hiyo ukiwa unaendelea kwa baadhi ya wananchi wachache, pia waliokaidi kuondoka katika makazi waliyoyaanzisha katika Misitu hiyo jambo ambalo lilipelekea atoe maagizo makali kama ifuatavyo;

Mkuu wa Mkoa Kijuu alimwagiza Afisa Misitu wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo kufikia tarehe 26 Agosti, 2017 awe amesitisha mara moja vibali vyote vya umiliki na uvunaji wa miti kwenye mashamba ambayo yanamilikiwa na wananchi yaliyopo jirani na Hifadhi za Misitu ya Biharamulo na Nyantakala kwa kuwa wamiliki hao wanayatumia mashamba hayo ya miti kama ngao huku wakifanya uhribifu wa uchomaji mkaa katika misitu hifadhi.
Agizo la pili, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mpago Bw. Yasin Mahanga asimamie uvunjwaji wa matuta yanayozuia maji kupita katika mkondo wake kwenye bonde la msitu Nyantakala pia kuwaondoa wananchi wote wanaoendesha kilimo katika bonde hilo mara moja na kumzuia mwananchi anayewatoza fedha wafugaji kunywesha maji mifugo yao katika lambo lililopo katika bonde hilo kuacha tabia hiyo mara moja vinginevyo atachukuliwa hatua za kisheria.

Agizo la tatu la Mkuu wa Mkoa Kijuu ni kwa wananchi waliovamia na kuanzisha makazi katika Msitu wa Nyantakala na kuyabatiza makazi hayo jina la MOMBASA RAHA kuondoka mara moja ifikapo tarehe 9 Septemba, 2017. Wasipoondoka wenyewe hadi tarehe 10 Septemba, 2017 Mhe. Kijuu ameagiza Jeshi la Polisi kuvunja makazi hayo na kuwalazimisha wananchi wavamizi kuondoka kwa lazima.
Mhe. Kijuu anaendelea na ziara ya katika Mapori ya Akiba ya Burigi na Kasindaga kujionea mwenyewe kama agizo la Rais John Pombe Magufuli limezingatiwa na kutekelezwa kikamilifu.

Chanzo BukobaWadau

SERIKALI MKOANI KAGERA YAPOKEA VIFAA VYA AFYA VYENYE THAMANI YA MILIONI KUMI KUTOKA MPANGO WA USAID BORESHA AFYA

Bw. Charles Kato Meneja wa Mpango wa USAID Boresha Afya Mkoa wa Kagera (Kushoto) Akimkabidhi Vifaa vya Afya Mkuu wa Wilaya Bukoba Mhe. Deodatus Kinawilo Aliyevipokea Kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu.
 Bw. Charles Kato Meneja wa Mpango wa USAID Boresha Afya Mkoa wa Kagera (Kushoto) Akimkabidhi Vifaa vya Afya Mkuu wa Wilaya Bukoba Mhe. Deodatus Kinawilo Aliyevipokea Kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu.
 Picha ya Pamoja Mara baada ya Vifaa Kukabidhiwa


Serikali Mkoani Kagera yapokea vifaa vya Afya vyenye thamani ya shilingi Milioni Kumi kutoka kwa wadau wa maendeleo wa mpango wa USAID Boresha Afya ambao ni wadau muhimu katika Sekta ya Afya kwa Mkoa wa Kagera.
Vifaa hivyo vilikabidhiwa na Meneja wa mpango wa USAID Boresha Afya Mkoa wa Kagera Bw.Charles Kato katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Agosti 21, 2017 ambapo vilipokelwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu.
Akikabidhi vifaa hivyo Bw. Kato alisema ni mahsusi kwa kituo cha Afya Kabyaile ambacho kimejengwa upya na Serikali baada ya kile cha awali kuharibiwa na Tetemeko la Ardhi mwaka jana Septemba 10, 2017. 
Aidha, Dk. Kato alisema kuwa vifaa vimetolewa na Mpango wa USAID Boresha Afya ambao unatekelezwa katika Wilaya ya zote za Mkoa wa Kagera. “Mpango huu wenye malengo ya kuchangia juhudi za Serikali za kuboresha Afya ya Mama na mtoto  unafadhiliwa na USAID na PATH pamoja na Serikali.” Alifafanua Bw. Kato
Pia Bw. Kato alisema kuwa vifaa hivyo vimetolewa kwa lengo la kuchangia mikakati ya Serikali ya kuhakikisha kituo kipya cha Kabyaile kinatoa huduma bora hasa kwa wakina mama na watoto.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bukoba Deodatus Kinawilo kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera aliwashukuru wadau hao waliotoa vifaa hivyo na kusema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao ili kuboresha huduma za wananchi hasa wakina mama na watoto katika Mkoa wa Kagera.
Kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Deodatus Kinawilo alikabidhi vifaa hivyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Kanali Denice Mwila ambaye naye alitoa shukrani za Wilaya yake kwa USAID Boresha Afya  kuwa wamekuwa wadau wapili kutoa msaada wao katika Kituo cha Kabyaile baada ya Benki ya NMB nao kutoa msaada wao na kutoa wito kwa wadau wngine kujitolea.
Vifaa vilivyotolewa ni Seti moja ya vifaa vya upasuaji wakati wa kujifungua, Seti moja ya vifaa vya kuzalisha, Mashine moja ya utakasaji wa vifaa, Seti mbili za kumsaidia mtoto kupumulia na kitanda kimo cha kujifungulia.

Chanzo BukobaWadau

SABABU UZALISHAJI MAZAO DUNI ZATAKWA


MAGONJWA na visumbufu vinavyoshambulia mazao mkoani Kagera husababisha wakulima kuzalisha mazao duni ya ndizi, maharage, mahindi na mihogo na kushindwa kufikia hitaji la kiwango cha mkoa.
Hayo yalisemwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Diwani Athuman, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha maonyesho ya Nanenane kwa niamba ya Mkuu wa mkuoa huo, Meja Jenerali mstaafu, Salimu Kijuu katika viwanja vya Kyakailabwa Manispaa ya Bukoba juzi.

Athumani alisema ili kutatua changamoto hizo, wakulima wanapaswa kushirikiana na wataalamu wa kilimo ambao ndio wanaoweza kutambua visumbufu vya magonjwa kwa kuwatembelea katika mashamba yao na kuwapatia elimu.

“Njia rahisi ya kuwafikiwa ni kukaa kwenye vikundi na kujiunga pamoja muweze kupatiwa elimu kutoka kwa wataalamu kwani ndio wenye kutambua tatizo la visumbufu hivyo,” alisema Athumani.

Aidha, alisema vikundi vya Saccos, AMCOS vinaweza kutoa mikopo ya kuwawezesha kuendeleza na kuinua kilimo pamoja na kukabiliana na visumbufu.

Hata hivyo, alisema mkoa huo unazalisha kwa kiwango cha chini ambapo ndizi huzalishwa tani 3.5 kwa ekari, mahindi huzalishwa ni tani 0.8 kwa ekari 1.6, mhogo huzalishwa tani 20 maharage tani moja kwa ekari.

Aliongeza kuwa utumiaji wa teknolojia unahitajika kwa ajili ya kuzalisha mazao ya chakula na ya biashara, hivyo kufikia uchumi wa viwanda.

BALOZI KAMALA ATEMBELEA KATA KITOBO NA KUZINDUA MRADI WA DARAJA LA KYANKOKO

 Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala siku ya jana alitembelea Kata ya Kitobo Wilayani Missenyi na  kuzindua  Daraja la Kyankoko lenye sehemu tatu zilizowekewa Kalavati ,mrasdi uliopewa jina la la Novati Rutegaruka Memorial Bridge ambalo ni jina la muasisi na mwanasiasa mkongwe ambaye aliangaingia eneo hilo katika kipindi cha Uhai wake.
Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala pichani wakati akizindua Daraja hilo lililogharimu kiasi cha shilingi milioni  kumi na nne za kitanzania (Tsh 14,000,0000)kulia pichani ni Diwani wa Kata ya Kitobo Mh.Willy Mtayoba.
 Muonekano wa Daraja la Kyankoko lililopewa jina la Novati Rutegaruka Memorial Bridge Daraja linalovikutanisha Vijiji vya Msibuka na Kayanga katika Kata ya Kitobo Wilayani Missenyi
 Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala (pichani) akiongea na wananchi wa Kijiji cha Kashasha kata Kitobo  waliohudhuria katika mkutano wake wa hadhara,Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala ameweza kuchangia miradi ya maendeleo inayoendelea katika kata hiyo na pamoja na kuahidi kuzifanyia kazi kero mbalimbali kama Uhaba wa wauguzi katika Zahanati na vituo vya Afya,Utaratibu wa Bima ya Afya kwa Wazee na watu wenye Ulemavu kwa kuwapunguzia changamoto wanazokutana
 Sehemu ya wananchi wakifatilia kwa umakini wakati mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiendelea kuwahutubia na kufanya majumuhisho ya changamoto alizozibaini katika ziara yake ya Siku 17 Jimboni Mwake.
 Baadhi ya wananchi waliohudhurio mkutano wameweza kupata nafasi ya kuelezea Kero zinazowakabili licha ya kuwepo mafanikio katika utatuzi wa baadhi ya kero kupitia kwa Mbunge wao Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala
 Baadhi ya wananchi waliohudhurio mkutano wameweza kupata nafasi ya kuelezea Kero zinazowakabili licha ya kuwepo mafanikio katika utatuzi wa baadhi ya kero kupitia kwa Mbunge wao Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala
Wananchi wakifurahia jambo katika mkutano huo uliofanyika Jana katika Kijiji cha Kashasha kata Kitobo Wilayani Missenyi,Picha kwa hisani ya #bukobawadaumedia
Afisa Maendeleo Kata Kitobo  Saudi Crispian wakati akisoma taarifa ya maendeleo ya kata kwa Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Balozi Dr. Diodorus Buberwa alipotembelea kata hiyo, Balozi Dr.Kamala amehitisha ziara yake  kwa kutembelea maeneo mbalimbali kwa kukagua miradi ya maendeleo na kubaini namna miradi mingi ya Maji Wilayani Missenyi ilivyotekelezwa chini ya kiwango.

Picha kwa hisani ya bukobawadaumedia

WAKIMBIZI RAIA WA BURUNDI WAITIKIA WITO WA RAIS MAGUFULI KUREJEA MAKWAO


Baadhi ya wakimbizi wakiwa katika boti tayari kurejea kwao



Na Mwandishi Wetu - MAELEZO

Kufuatia wito wa Rais John Pombe Magufuli alioutoa hivi karibuni, hadi kufikia jana tarehe 01 Agosti, 2017 jumla ya wakimbizi 6,700 raia wa Burundi wameshajiorodhesha kurejea nchini mwao kwa hiari.

Kufuatia hatua hiyo, Mkutano wa pande tatu utakaojumuisha Serikali za Tanzania, Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) unatarajiwa kufanyika mwishoni wa mwezi huu kujadili namna ya kuwarejesha nchini mwao wakimbizi hao kwa kuzingatia sheria za kimataifa zinazohusu wakimbizi.


 Katika mahojiano na mwandishi wetu ofisi kwake jana, Mkurugenzi Idara ya Huduma za Wakimbizi katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bwana Harrison Mseke alieleza kuwa tangu kutolewa kwa wito huo, Wizara imekuwa ikiwamahasisha wakimbizi hao wa kujiorodhesha kwa hiari ili waweze kurejea nyumbani.

Akiwa katika ziara yake kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa, Rais Magufuli alitoa wito kuwataka wakimbizi raia wa Burundi kurejea nyumbani kwa hiari kwa kuwa hali ya usalama nchini mwao ni nzuri ambapo wakati akitoa wito huo tarehe 20 Julai, 2017 huko Ngara aliambatana na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza ambaye nae aliwahakikishia wakimbizi hao kuwa hali ni shwari nchini Burundi. 

Kwa mujibu wa Bwana Mseke, hivi sasa kuna wakimbizi raia wa Burundi 276,692 kati ya wakimbizi 348,019 walioko nchini. Wengine ni  wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) 70,840, Wasomali 150, na wengine (mchanganyiko) 337. 

Alifafanua kuwa kati ya idadi hiyo ya wakimbizi raia wa Burundi 242,340 waliingia nchini baada ya mwezi Aprili, 2015 kufuatia machafuko ya kisiasa nchini humo.

Akizungumzia mwendo wa uingiaji wakimbizi kutoka Burundi, alieleza kuwa kwa sasa kasi imepungua kutoka wastani wa wakimbizi 1,000 kwa siku kati ya mwezi Agosti hadi Disemba, 2016 hadi wastani wa wakimbizi kumi kwa siku katika miezi ya hivi karibuni.

GAVANA WA JIMBO LA MASHARIKI LA RWANDA ATEMBELEA MKOA WA KAGERA


Gavana wa Jimbo la Mashariki la Rwanda Mhe.Judith Kazaira Atembelea Mkoa wa Kagera leo Jumatatu Julai 31,2017 na kukutana na Mhe.Salum Kijuu,Mkuu wa Mkoa wa Kagera na kufanya mkutano wa Ujirani mwema na uongozi wa Mkoa huo yeye na ujumbe wake. Pichani juu Mhe.Kazaira aliyeambatana na Balozi wa Rwanda nchini Mhe.Eugene wakipokekewa na Bw.Suleiman Saleh,Mkurugenzi Msaidizi,Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Gavana wa Jimbo la Mashariki la Rwanda Mhe.Judith Kazaira Atembelea Mkoa wa Kagera leo Jumatatu Julai 31,2017 na kukutana na Mhe.Salum Kijuu,Mkuu wa Mkoa wa Kagera na kufanya mkutano wa Ujirani mwema na uongozi wa Mkoa huo yeye na ujumbe wake. Pichani juu Mhe.Kazaira aliyeambatana na Balozi wa Rwanda nchini Mhe.Eugene wakipokekewa na Bw.Suleiman Saleh,Mkurugenzi Msaidizi,Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa