Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Luteni
Kanali Denice Mwila kuhusu changamoto za mpaka huo wngine ni Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Suleman Jaffo, Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Masauni, Naibu Waziri wa Maji na
Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Suzan Kolimba.
Jiwe la mpaka wa Tanzania na Uganda
namba 30.
Ujumbe wa Mawaziri kutoka Serikali ya
Jamhuri ya Muungano Tanzania wakiwa juu ya Jiwe la mpaka wa Tanzania na Uganda
namba 30.
Moja ya jiwe la mpaka wa Tanzania na Uganda
ambalo Mawaziri wamefanya ziara ya kuliona.
Ujumbe wa Mawaziri kutoka Serikali ya
Jamhuri ya Muungano Tanzania wakipita katika eneo la kivuko cha mpaka wa
Tanzania na Uganda kilichopo Mtukula mkoani Kagera.
Ujumbe wa Mawaziri kutoka Serikali ya
Jamhuri ya Muungano Tanzania wakikagua huduma za vibali vya kuingia na kutoka
nchini Tanzania na Uganda zilizopo Mtukula mkoani Kagera.
Eneo la mpaka ya Tanzania na Uganda
kwa upande unapo pita mto Kagera.
Aidha, ziara hii ni maandalizi ya Mkutano wa ujirani mwema kati ya Mawaziri wa serikali ya Uganda na Mawaziri kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao unatarajiwa kufanyika mnamo tarehe 29 Julai 2017, Bukoba mkoani Kagera.
Na. Hassan Mabuye
Mawaziri watano wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watembelea mpaka wa Tanzania na
Uganda ili kutatua changamoto zinazoukabili mpaka huo na kuuboresha.
Mawaziri hao ni
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Masauni, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Suleman Jaffo, Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Suzan Kolimba na Naibu
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe.
Miongoni mwa maeneo
yaliyotembelewa na Mawaziri hao ni eneo la mpaka ya Tanzania na Uganda kwa
upande unapo pita mto Kagera na eneo la kivuko cha mpaka wa Tanzania na Uganda
kilichopo Mtukula mkoani Kagera.
Katika ziara hii
Mawaziri hao wameweza kujionea hali halisi ya maisha ya wakazi wa mipakani na
jinsi wanavyohusiana na wenzao wa nchi ya jirani ya Uganda ambapo wamekuwa
wakishirikiana na kuishi kwa amani katika shughuli zao za kila siku.
Aidha, ziara hii ni maandalizi ya Mkutano wa ujirani mwema kati ya Mawaziri wa serikali ya Uganda na Mawaziri kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao unatarajiwa kufanyika mnamo tarehe 29 Julai 2017, Bukoba mkoani Kagera.
0 comments:
Post a Comment