Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Sinohydro Corporation Ltd
anayejenga barabara ya Uyovu-Bwanga KM 45 kwa kiwango cha lami, mkoani
Geita.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Bwanga-Biharamulo yenye urefu wa KM 67, mkoani Geita.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Geita Eng. Harun Senkuku akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, kuhusu maendeleo yaliyofikiwa ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga yenye urefu wa KM 45, mkoani Geita.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema mradi wa ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga-Biharamulo yenye urefu wa KM 112 inayojengwa na mkandarasi wa Kampuni ya Synohydro Corporation itakamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Prof.
Mbarawa amezungumza hayo mkoani Kagera, wakati akikagua maendeleo ya
ujenzi wa barabara hiyo na kumtaka mkandarasi aongeze kasi ili barabara
hiyo iweze kukamilika kwa wakati.
“Hakikisheni mnaongeza kasi ya ujenzi ili muweze kukamilisha ujenzi huu kwa wakati iwezekanavyo”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.Amemsisitiza
mkandarasi kuzingatia viwango vilivyopo katika mkataba kwani mwisho wa
siku lazima watanzania wapate barabara inayokidhi mahitaji yao na ubora
wake.
Amewapongeza
wasimamizi wa barabara hiyo ambao ni kutoka kwa Wakala wa Barabara
nchini (TANROADS) kupitia kitengo chake maalum cha wahandisi washauri
wazawa (TECU), kwa kuhakikisha wanamsimamia mkandarasi M/S Sinohydro
Corporation kwa ukaribu.
Kwa
upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa
Geita Eng. Harun Senkuku amemueleza Waziri Prof. Mbarawa kuwa changamoto
ya fidia iliyokuwa inawakabili sasa imemalizika na kiasi cha shilingi
milioni 700 zimetumika kukamilisha ulipaji fidia kwa wakazi wote.
Amemhakikishia
Waziri kuwa TANROADS itaendelea kumsimamia mkandarasi huyo ili
kuhakikisha thamani halisi ya fedha ya Serikali inapatikana.Mradi
wa ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga-Biharamulo KM 112 umehusisha
ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga yenye urefu wa KM 45 na barabara ya
Bwanga-Biharamulo yenye urefu wa KM 67.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
0 comments:
Post a Comment