MAWAZIRI watano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
wametembelea mpaka wa Tanzania na Uganda ili kutatua changamoto
zinazoukabili mpaka huo na kuuboresha.
Mawaziri hao ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,
William Lukuvi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni,
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Selemani Jaffo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Dk Suzan Kolimba na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,
Mhandisi Isack Kamwelwe.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara ya ardhi, miongoni mwa
maeneo yaliyotembelewa na mawaziri hao ni eneo la mpaka ya Tanzania na
Uganda kwa upande unapopita mto Kagera na eneo la kivuko cha mpaka wa
Tanzania na Uganda kilichopo Mtukula mkoani Kagera.
Katika ziara hiyo, mawaziri hao walijionea hali halisi ya maisha ya
wakazi wa mipakani na jinsi wanavyohusiana na wenzao wa nchi ya jirani
ya Uganda, ambapo wamekuwa wakishirikiana na kuishi kwa amani katika
shughuli zao za kila siku.
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment