CHAMA Kikuu cha Ushirika, Mkoa Kagera (KCU 1990) LTD, kimefanya
mabadiliko ya kuwachagua viongozi wapya na kuwatupa wa zamani katika
Mkutano Mkuu Maalum.
Uchaguzi huo umefanyika jana chini ya usimamizi wa Mrajisi Msaidizi
wa Mkoa Kagera, Rweikiko Shorosi, ambaye alisema serikali inapenda kuona
vyama vya ushirika vikifanya vizuri
Alibainisha migogoro inayovikumba vyama vya ushirika vinakwamisha
harakati za wananchi kutafuta fursa za kujiwezesha kimaendeleo.
Akisoma majina ya watu waliojitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi
ya Wajumbe wa Bodi ya KCU 1990, katika Mkutano Mkuu maalum uliofanyika
mjini hapa, Shorosi alisema waliojitokeza kuchukua fomu walikuwa 22
Alisema majina yaliorudi baada ya kuchujwa ni 18 wote ni sura mpya tofauti na walivyotarajia watu wengi
“Haya majina ndiyo yaliyofikisha asilimia 50 na kuendelea na hivyo,
nitasoma majina ya wale waliofuzu vigezo ya kamati iliokaa kuyajadili
“alisema.
Katika uchaguzi huo kila Wilaya ilitoa wagombea wa wajumbe wa bodi
ambapo katika wilaya za Muleba, Halmashauri ya Bukoba, Missenyi walitoa
wagombea zaidi ya wanne huku Manipaa ya Bukoba ikitoa wagombea wawili.
Katika nafasi ya Mwenyekiti wagombea walikuwa wawili ambao ni Frank
Muganyizi, aliyepata kura 189 kati ya 246 zilizopigwa na Sylvanus
Muhyoza, aliyepata kura 50 hivyo, Muganyizi kutangazwa kuwa Mwenyekiti
Mpya wa Bodi hiyo.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilikuwa inawaniwa wajumbe watatu Festo
Paulo aliyepata kura 31, Sandru Nyangasha aliyepata kura 78, na Ingatus
Batanuzi aliyewashinda kwa kupata kura 136.
Wajumbe wapya wa bodi hiyo waliochaguliwa na Mkutano Mkuu ni pamoja
na Winfrida Kyombo aliyepata kura 102 kutoka Wilaya ya Missenyi na
Festo Paulo kura 56, wajumbe kutoka Bukoba mjini ni Sylvanus Muyoza
aliyepata kura 227.
Wajumbe kutoka Wilaya ya Muleba ni pamoja na Ignatus Batamuzi aliyepata kura 133, na Projestus Balengela aliyepata kura 44.
Wilaya ya Bukoba waliochaguliwa ni pamoja na sandru Nyangasha
aliyepata kura 60 na Frank Muganyizi aliyepata kura 90, pia wajumbe hao
walimchagua Dominick Kasaju kutoka Chama cha msingi Bukwali wilayani
Missenyi kuwa mwakilishi kutoka nje ya bodi ambapo alipata kura 182.
Akizungumza baada ya uchaguzi huo Mrajis Msaidizi, Moshi Chogero,
alisema uchaguzi huo umefanyika kwa mujibu wa sheria namba sita ya mwaka
2013 ni wa uhuru na haki.
Alisema kwa wajumbe ambao walichukua fomu na kujaza lakini majina yao
hayakuweza kurudi wanaweza kukata rufaa kwa mrajisi kwani ni haki yao
ya kidemokrasi kufanya hivyo.
Chanzo;Tanzania daima
0 comments:
Post a Comment