Na:
Frank Shija, MAELEZO
SERIKALI
imewataka walimu wa shule za msingi na sekondari nchini kuwasilisha madai yao
yasiyo kuwa ya Mishahara ikiwemo stahili za likizo ili waweze kulipwa madai
hayo kwa wakati.
Hayo yamesemwa jana
na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako wakati wa
mahojiano ya kipindi maalum cha TUNATEKELEZA kinachorushwa na kituo cha
Televisheni cha Taifa (TBC1).
Profesa Ndalichako
alisema kuwa Madeni ya Walimu yamegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni madai
yatokanayo na mishahara na yasiyokuwa ya mishahara ambayo yamekuwa yakilipwa na
Serikali kupitia Wizara yake ambapo hadi hivi sasa hakuna mtumishi ambaye
hajalipwa.
“Hakuna jalada la
madai ya walimu yasiyokuwa ya mishahara na kama yapo madai walete ili walipwe
kwani fedha zipo”. Alisema Profesa Ndalichako na kuongeza kuwa madai ya
mishahara yamekuwa yakishughulikiwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma ambapo nayo yamekuwa yakifanyika.
Kwa mujibu wa Profesa
ndalichako alisema Serikali imekuwa ikipata ufadhili kutoka Serikali ya Sweden
kwa ajili ya kusaidia katika kulipa stahili mbalimbali za walimu ili kuboresha
weledi wa taaluma yao.
Kwa upande wa ubora
wa Elimu, Ndalichako alisema kuwa pamoja na changamoto zilizopo katika sekta
elimu, ubora wa Elimu ya Tanzania umekuwa ukifanyiwa kazi kupitia program
mbalimbali zikiwemo za mpango wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).
Akitolea mfano Waziri
Ndalichako alisema kuwa kumekuwapo na maboresho makubwa tokea enzi za mpango wa
UPE miaka ya 1970 ambao lengo lake lilikuwa kuwawezesha wanafunzi wengi zaidi
kujiunga na elimu ya msingi.
Waziri Ndalichako
mwaka 2013 Serikali iliendelea kufanya maboresho kwa kuongeza sifa za kujiunga
na vyuo vya ualimu ili kupata walimu wenye ubora ndipo udahili wa ikiwemo ufaulu
wa daraja la tatu kwa wahitimu wa kidato cha nne na ufaulu wa masomo mawili
katika kidato cha sita.
“Serikali ilianzisha
Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 ambayo ilibainisha kuwa elimu ya msingi
na mafunzo mwanafunzi atatakiwa atasoma darasa la kwanza hadi la 6 kwa msingi
na mafunzo ni kuanzia darasa la 7 hadi la 12”.
0 comments:
Post a Comment