Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Kyerwa, Kagera
Ukame
unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi ulioathari mazao ya ndizi na
kahawa wilaya Kyerwa mkoani Kagera umemlazimu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Muhagama
kuwaomba wananchi wa mkoa huo wabadilike waanze kulima mazao mengine ya
chakula yanayokomaa kwa muda mfupi.
Athari
hiyo ya ukame imemlazimu Waziri Mhagama kuwataka wananchi wa wilaya
hiyo na mkoa wa Kagera kwa ujumla w0aanze kulima mazao mengine
yanayokomaa kwa muda mfupi yaweze kuwapunguzia adha ya upungufu wa
chakula unaotokana na kutegemea zao la ndizi pekee.
Akiwa
katika kijiji cha Ntare kata ya Itera wilayani Kyerwa Waziri Mhagama
aliongea na wananchi wa kata hiyo ambapo alisema “Mabadiliko ya tabia
nchi ni makubwa, msiendelee kutegemea zao moja tu la chakula la ndizi,
ni lazima mkubali sasa tuende kwenye mazao mengine ya chakula, limeni
mihogo, limeni mahindi. Nendeni kwenye mazao yanayokomaa kwa muda mfupi,
vinginevyo tukisema kila kila mwaka tuendelee kutegemea kahawa na ndizi
kwa hali ya hewa ilivyo sasa tutaendelea kukosa chakula”.
Waziri
Mhagama aliyataja mazao hayo kuwa yanaweza kukomaa kwa muda mfupi
kuanzia miezi mitatu ndiyo yanaweza kuwa mkombozi wa katika kukabiliana
na upungufu wa chakula na kuwahakikishia wananchi chakula cha kutosha
hatua ambayo itawafanya waendelee na shughuli zenye tija kwa maendeleo
yao.
Mkulima
wa kata hiyo Shakiru Issa anathibitisha kuwa upo uwezekano wa kulima
mazao mengine zaidi ya ndizi na kahawa ambayo yanamuongezea kipato
ambapo yeye analima pia zao la viazi mviringo kwa ajili ya chakula
pamoja na kuuza hatua inayomsaidia kumuongezea kipato na kuendesha
maisha yake ya kila siku.
Ili
kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi Waziri Mhagama amewataka
wananchi wa mkoa wa Kagera kuacha tabia ya kuchoma mapori moto mara moja
kwa kuwa tabia hiyo huhatarisha maisha ya watu, kupoteza mazao
shambani,miti na hifadhi ya misitu ambayo ndiyo kivutio kikuu cha mvua.
Aidha,
ziara hiyo wa Waziri Mhagama imekuwa faraja kwa wananchi wa Kata ya
Itera ambapo amemwagiza Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya
Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Mbazi Msuya aende kufanya tahmini ya hali
ukame ilivyo athiri wilaya hiyo na kutoa taarifa mapema iwezekanavyo.
Katika
kuhakikisha upatikanaji wa chakula cha kutosha wilayani Kyerwa, Waziri
Mhagama ametoa wito na kumuagiza Mkuu wa Wilaya hiyo Kanali Mstaafu
Shaban Lissu pamoja kulima zao la ndizi, aanza haraka kampeni ya
kuwahamasisha wananchi hao kulima mazao yanayokomaa kwa muda mfupi
ambayo yataweza kuwapatia chakula cha kutosha kwa mahitaji yao ya kila
siku.
0 comments:
Post a Comment