Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (mstaafu), Salum Kijuu, (kushoto), akimkaribisha ofisini kwake, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, alipomtembelea Septemba 17, 2016 ofisini kwake mkoani humo ili kumpa pole kufuatia athari za tetemeko la ardhi
Mkuu wa Mkoa, Meja Jenerali (mstaafu), Salum Kijuu, akitoa taarifa za athari hizo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba na ujumbe wake
NA
K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID, BUKOBA
SHIRIKA
la Umeme Nchini Tanzania, TANESCO, limewahadharisha wananchi mkoani Kagera kutogusa
nyaya za umeme kwenye nyumba zilizoanguka
au kupata athari kubwa kutokana na tetemeko la ardhi lililoukumba mkoa wa
Kagera wakati wafanyakazi wa Shirika hilo wakiendelea na zoezi la kuondoa nyaya
hizo.
Wito
huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Mhandisi Felchesmi
Mramba, (anayezungumza juu), wakati alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (mstaafu),
Salum Kijuu, Septemba 17, 2016 ili kumpa pole kutokana na maafa haayo.
Sambamba
na wito huo, Mkurugenzi huyo pia alimuhakikishia Mkuu huyo wa Mkoa kuwa upatikanaji
wa umeme mkoani humo utakuwepo bila shaka yoyote isipokuwa tu kwenye maeneo
ambayo nyumba zimeathirika vibaya ili kuepusha athari zozote zinazoweza kutokea
kutokana na kuguswa kwa nyaya hizo.
“Ninachoweza
kusema Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa, hakuna kifo kilichotokana na madhara ya umeme
wakati wa tetemeko hilo, na vijana wetu walichukua hatua mara moja za kukata
umeme tatizo hilo lilipotokea,” alisema Mhandisi Mramba.
Mkurugenzi
huyo Mtendaji pia alisema, kutokana na ukubwa wa janga hilo, uongozi wa TANESCO
ulichukua uamuzi wa kuwapeleka wafanyakazi wengine wa Shirika hilo kutoka
mkoani Mwanza ili kuwaongezea nguvu wenzao wa Kagera katika jitihadav za
kuhakikisha wananchi wanakuwa salama kutokana na kuharibika kwa miundombinu ya
umeme kwenye majengo mbalimbali yaliyopata athari za tetemeko hilo.
Sambamba
na wito huo, Mhandisi Mramba pia alimwambia Mkuu wa mkoa kuwa, Wafanyakazi wa
TANESCO nchi nzima, wameanza zoezi la kuchanga fedha ili kuwasaidia wananchi wa
Bukoba. “Sisi kwa upande wetu kama Shirika, tumekwisha kabidhi mchango wetu
kupitia Msajili wa Hazina,” Aliongeza Mhandisi Mramba.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali (mstaafu), Salum Kijuu, alisema,
tetemeko hilo lililokuwa na ukubwa wa kipimo cha richa 5.7, lilipelekea vifo
vya watu 17, na kusababisha majeruhi zaidi ya 200, na kuacha nyumba zaidi ya 2,000
zikiharibika na nyingine kubomoka kabisa.
Alsiema
mkoa unaendelea na kuratibu zoezi la kukuanya rasilimali fedha na vifaa ili
kuwasaidia walioathirika.
Baada
ya mkutano huo na Mkuu wa mkoa, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, alitembelea
baadhi ya maeneo yaliyoathirika sana na tetemeko hilo huko Hamugembe, ili
kukagua zoezi la utoaji elimu kwa wananchi kuhusu athari za nyaya zilizokaa
vibaya kwenye makazi yao na kuwatia moyo wafanyakazi wa Shirika hilo ambao
walikuwa wanaendelea na kazi hiyo.
Mhandisi
Mramba, alipata fursa ya kuzungumza na Afisa Mtendaji wa Kata ya Hamugembe,
Sudi Ahmada, na kumueleza kuwa, wakati wafanyakazi wa TANESCO wakiendelea na
zoezi hilo, uongozi wa Kata nao ushirikiane na wafanyakazi wa Shirika hilo
katika kuwaelimisha wananchi juu ya hatua zinazochukuliwa na TANESCO kwa sasa.
“Ningeomba
muwaelimishe wananchi kuwa ni bora kutokuwa na umeme kwa kipindi hiki kifupi
ambacho Shirika linachukua hatua za kuhakikisha usalama wao, na waonapo au kuwa
na shaka yoyote juu ya nyaya au jambo linalowatia hofu kuhusu umeme, watoe
taarifa haraka TANESCO na tutachukua hatua haraka,” alimuhakikishia Afisa huyo
Mtendaji.
Naye
Afisa huyo Mtendaji wa Kata ya Hamugembe, aliishikuru TANESCO kwa kuchukua
hatua za haraka siku ya tukio hilo na kueleza furaha yake kwa jinsi anavyoona
jitihada mbalimbali za wafanyakazi wa TANESCO katika kuhakikisha wananchi
wanakuwa salama.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Kagera, Mhandisi Francis Maze, akitoa elimu ya namna ya kuchukua hatua endapo patatokea athari zozote za umeme kwenye nyumba moja iiyoathirika na tetemeko huko Hamugembe
Fundi akiwa kazini, Hamugembe
Fundi wa TANESCO mkoani Kagera, akiondoa nyaya za umeme baada ya kukata umeme kwenye nyumba moja eneo la Hamugembe, ikiwa ni hatua ya kuchukua tahadhari
Mhandisi Mramba, akitembelea maeneo yaliyoathirika na tetemeko hilo huko Hamugembe
Bi Slivia Philip, akiwa ameketi nje ya nyumba yake iliyoharibiwa vibaya na tetemeko eneo la Hamugembe-Mkishenyi mkoani Kagera, Septemba 17, 2016
Violet Anaclet, mkazi wa Hamugembe-Mkishenyi, akiwa na mawazo wakati akijipumzika kwenye eneo la wazi baada ya nyumba aliyokuwa akiishi kuharibiwa na tetemeko, Septemba 17, 2016
Mhandisi Mramba, akisalimiana na Afisa Mtendaji wa Kata ya Hamugembe,
Sudi Ahmada, Septemba 17, 2016
Kaimu Meneja wa TANESCO Kanda ya Ziwa, Mhandisi Kalisa, (kulia), akizungumza na fomeni wa genge la TANESCO Kanda ya Ziwa, Freddy Lusama, wakati Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Mhandisi Mramba alipowatembelea wafanyakazi wa Shirika hilo waliokuwa wakiendelea na kazi kwenye eneo la Hamugembe mkoani Kagera, Septemba 17, 2016
Meneja wa TANESCO mkoani Kagera, Mhandisi Francis Maze, (katikati), akiwa amezungukwa na wafanyakazi wa shirika hilo akiwapa maelekezo, Septemba 17, 2016
Mhandisi Mramba, alipofika eneo la Hamugembe, kuona jinsi wafanyakazi wa Shirika hilo wakiendelea na kazi
Kwa bahati nzuri hakuna nguzo za umeme zilizoathirika na tetemeko hilo, hata hivyo TANESCO imeamua kuchukua tahadhari kwa kukagua ili kuona kama kuna nguzo yoyote iliyoathirika na kuchukua hatua za kubadilisha, kama ambavyo lori hili lililoonekana maeneo ya Hamugembe likiwa na nguzo hizo
Mhandisi Mramba, akiongea na waanishi wa habari kwenye eneo moja lililoathirika vibaya na tetemeko la ardhi huko Hamugembe
Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania, 9TANESCO), Leila Muhaji, akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya kiusalama ambayo wananchi wanapaswa kuzingatia pindi waonapo nyaya zilizoanguka au kutilia shaka yoyote kuhusiana na miundombinu ya Shirika
Genizora Magili, anayehusika na masuala ya nyaya za umeme, akiwa amebeba vifaa vya kazi
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (mstaafu), Salum Kijuu, akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba na ujumbe wake, mara baada ya mazungumzo yao, Septemba 17, 2016
Meja Jenerali Kijuu, akiagana na Mhandisi Mramba na ujumbe wake
0 comments:
Post a Comment