Afisa
Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma
Ledama akizungumza na Mkuu wa Shule ya Sekondari Ndama ya Wilayani
Karagwe Mwl. Emmanuel Muganyizi kuhusiana na umuhimu wa wanfunzi wa
shule yake kuanzisha Vilabu vya Umoja wa Mataifa na faida zake.
Afisa
Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma
Ledama akizungumza na walimu wa shule ya Sekondari Ndama na kuwapa
hamasa ya kuwa walezi wazuri wa vilabu hivyo vitavyoanzishwa shuleni
hapo ikiwa ni kama somo la ziada kwa wanafunzi wao ili wasipate muda wa
kushiriki matendo ya ajabu na yasiyo na maadili.
Usia
Nkhoma Ledama akiongozwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Ndama ya
wilayani Karagwe kuelekea madarasani kuzungumza na wanafunzi wa shule
hiyo.
Afisa
Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma
Ledama akizungumza na vijana wa shule za sekondari Ndama wilayani
Karagwe mkoani Kagera, kuwaelezea umuhimu wa kujiunga na vilabu vya
Umoja wa Mataifa (UN Club) vinavyoanzishwa mashuleni kwa kuwa kwanza
vitawasaidia kujitambua.
Amewaambia
kwa vijana kama wao ambao tayari wameanzisha na kuendesha vilabu hivyo
mashuleni kujiunga kwa wingi zaidi na kutawawezesha kujifunza shughuli
za umoja wa mataifa duniani, kuhusishwa na mashirika mengine ya
kimataifa, kushiriki katika mafunzo mbalimbali, warsha na mikutano ndani
na nje ya nchi kama vile National Model UN, the Eastern Africa Model
UN, the Africa Regional Model UN na mengineyo, ikiwemo kupata nafasi ya
kuisaidia jamii zao kupitia program mbalimbali.
Bi.
Usia pia amewafafanulia vijana kuwa katika klabu hizo wataweza kuwa na
mtandao na vijana wengine kitaifa na kimataifa, kupata nafasi ya kufanya
kazi za kujitolea.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Ndama wakimsikiliza kwa makini Afisa
Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) Usia
Nkhoma Ledama (hayupo pichani).
Usia
Nkhoma Ledama katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari
Ndama pamoja na Mkurugenzi wa Radio Jamii FADECO ya wilayani Karagwe
Bw, Joseph Sekiku (kushoto).
Afisa
Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma
Ledama akijitambulisha kwa baadhi ya walimu wa Shule ya Sekondari
Kayanga ya Wilayani Karagwe Mkoani Kagera. Kushoto mwenye suti ni
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Johnbosco Paul.
Afisa
Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma
Ledama akikagua Maktaba ya Shule ya Sekondari Kayanga. Kulia ni Mwl.
Mkuu wa Shule ya Kayanga Johnbosco Paul.
Afisa
Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma
Ledama akizungumza na wazazi wa watoto wanaosoma katika shule ya
sekondari ya Kayanga amewaelezea kuwa pindi watoto wao wanapojiunga na
klabu za Umoja wa mataifa zilizopo mashuleni watapata elimu na uzoefu
utakaotengeza thamani ya CV zao na kuzipa uzito zaidi na pia watapata
ufahamu wa mambo mengi utakao wasaidia wasijiunge na vikundi visivyofaa
wala kushiriki matendo ya ajabu na yasiyo na maadili.
Amewaambia
wazazi hao ndani ya klabu hizo hutokea kupata tarajali, uzoefu wa kazi,
na kwamba kwa kupitia klabu hizo vijana wote shule zilizopo mikoa yote
ya Tanzania watakuwa na nafasi ya kuwa karibu na taratibu na kanuni za
Umoja wa Mataifa.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Kayanga ya Wilayani Karagwe mkoani Kagera wakiwa mapumzikoni kuelekea kupata uji.
Picha na maelezo kwa hisani ya fullshangweblog.com
0 comments:
Post a Comment