Home » » MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUTURU NA WAKAZI WA KAGERA WILAYA YA MISENYI JANA.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUTURU NA WAKAZI WA KAGERA WILAYA YA MISENYI JANA.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Kagera, baada ya kufuturu nao futari ya pamoja aliyoiandaa katika Kiwanda cha Kagera Sugar, jana Julai 24, 2013. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, Kanali Mstaafu, Issa Njiku (kushoto) ni Mmiliki wa Kiwanda cha Kagera Sugar, Nassor Seif.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Kagera Sugar, Hashim Ranner, baada ya kumalizika kwa hafla ya Futari ya pamoja na wananchi wa Mkoa wa kagera iliyofanyika katika Kiwanda cha Kagera Sugar Wilaya ya Misenyi jana Julai, 24, 2013. Katikati ni Mmiliki wa Kiwanda hicho, Nassor Seif.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkk. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya wananchi alioshiriki nao Futari ya pamoja katika Kiwanda cha Kagera Sugar Wilaya ya Misenyi Mkoa wa Kagera, baada ya kumalizika kwa hafla hiyo jana Julai 24, 2013

 Baadhi ya wananchi waumini wa dini ya Kiislamu waliohudhuria hafla ya futari ya pamoja, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akizungumza nao jana Julai, 24, 2013. 
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa