Home » » Serikali yaahidi kukamilisha mradi wa umeme Chato

Serikali yaahidi kukamilisha mradi wa umeme Chato

SERIKALI kupitia wizara ya Nishati na Madini imeahidi kumaliza kero ya mgao wa umeme inayowakabili wakazi wa wilaya ya Chato mkoani Geita hali ambayo imechangia kuzorota kwa uzalishaji mali katika maeneo hayo.

Kauli hiyo ya serikali imetolewa na waziri wa Nishati na Madini Prof,Sospeter Muhongo baada ya kuahidi kufunga mashine mpya ya kufua umeme kwenye wilaya hiyo ili kuepuka adha ya mgao wa umeme unaotokana na mashine zilizoko wilaya jirani ya Biharamulo.

Prof Muhongo amesema hayo jana(JUMATATU) kwenye mkutano wa hadhara muda mfupi baada ya ombi lililotolewa na Mbunge wa jimbo la Chato,Dk John Magufuli kutokana na adha kubwa ya kukatika kwa umeme mara kwa mara hali inayodaiwa kukwamisha ukuaji wa uchumi.

Amesema serikali imekubali kutoa mashine moja kubwa itakayozalisha umeme katika wilaya hiyo na kwamba itafungwa katika wilaya hiyo badala ya kuendelea kutumia mshine zilizoko wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera.

Amesema mashine zinazotumika kufua umeme katika wilaya ya Biharamulo na Chato ni chakavu ambazo wakati zinafungwa zilikuwa tayari zimeshatumika sehemu nyingine hapa nchini.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa