Home » » Madiwani wailalamikiwa barabara iliyozinduliwa na Rais Kikwete

Madiwani wailalamikiwa barabara iliyozinduliwa na Rais Kikwete

BARABARA iliyozinduliwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete katika Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera imelalamikiwa na madiwani wa halmashauri hiyo kufuatia baadhi ya barabara zinazoingia katika taasisi za huduma za jamii kuharibiwa na kampuni ya Chico inayotengeneza barabara hiyo kwa kiwango cha Lami.
Madiwani Wamesema hayo katika kikao kilichofanyika leo(Jumanne) kufuatia barabara hizo kuharibiwa na hali ambayo imesbabisha wananchi wa maeneo hayo kulazimika kutembea umbali mrefu kwenda kwenye huduma za kijamii badala ya kutumia vyombo vya usafiri yakiwemo magari,na pikipiki.

Mmoja wa madiwani hao Diwani wa kata ya Rusahunga,Amon Mizengo akichangia hoja hiyo kwenye baraza la madiwani la kujadili taarifa za robo mwaka amesema hali hiyo imesababisha magari yanayopeleka huduma za kijamii kushindwa kuingia na mbaya zaidi kunapotokea mgonjwa inakuwa vigumu kumwahisha kwenye huduma ya matibabu.

Taasisi zilizoadhirika na uharibifu wa barabara hizo ni makao makuu ya tarafa,kata na kijiji cha Rusahunga ambako kuna Zahanati shule ya msingi Nyambale,Shule ya sekondari Rusahunga,tatizo ambalo limekuwepo tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Hoja hiyo ilikuja kufuatia majibu yaliyotolewa na mkurungezi wa halmashauri hiyo,Nassib Mmbagga kwamba ukarabati wa barabara hizo umeanza kutekelezwa ambapo kampuni ya Chico imeanza kuzingatia agizo la madiwani lililowahi kufikishwa pia kwenye kikao cha bodi ya barabara Taroad mkoani hapa.

Julai 26 mwaka huu rais Kikwete alizindua barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 154 inayotekelezwa na Kampuni ya Chico ambapo ambapo toka ujenzi huo uanze baadhi ya barabara zinazoelekea sehemu zingine ziriharibiwa hali ambayo imeleta usumbufu mkubwa kwa wananchi.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa