Home » » RAIS MAGUFULI AMKABIDHI VIFAA VYA UJENZI MJANE MKOANI KAGERA.

RAIS MAGUFULI AMKABIDHI VIFAA VYA UJENZI MJANE MKOANI KAGERA.

Na Eleuteri Mangi-MAELEZO.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemchangia vifaa vya ujenzi Mjane Agripina Angelo Mkazi wa Kitoma Wilayani Karagwe Mkoani Kagera.

Akimkabidi vifaa hivyo kwa niaba ya Rais, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali (Mst) Salum Kijuu alisema kuwa Rais Dkt. Magufuli amefanya hivyo baada ya kuona kupitia vyombo vya habari jitihada za Mjane huyo kuanza kuijenga nyumba yake upya kutokana na kuharibika baada ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo mapema mwezi septemba.

Aidha Mkuu wa Mkoa Kijuu alitoa wito kwa wananchi ambao hawajaanza juhudi za kurejesha makazi yao waige mfano wa mjane huyo kwa kuanza ujenzi wa nyumba zao.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo Bi. Agripina alisema kuwa anamshukuru Rais kwa mchango huo kwani vifaa hivyo vitamsaidia kukamilisha ujenzi wa nyumba yake  na hatimaye kupata mahali pa kuishi yeye na familia yake baada ya nyumba yake ya awali kuharibiwa na tetemeko la ardhi.

Vifaa alivyokabidhiwa mjane huyo ni pamoja na Mbao pisi 30, Mabati 35 ya futi kumi ,Saruji mifuko 25 ,Misumari ya mabati  kilo 4, Misumari ya kenchi kg 7 na waya za kufungia makenchi kilo 3.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa