Na Benedict Liwenga-MAELEZO
Serikali
imepanga kuijenga shule ya msingi ileega na kufanya ukarabati wa vyumba
viwili vya madarasa katika shule ya msingi Nyamilima zote zilizopo
wilayani kyerwa mkoani Kagera kufuatia uharibifu uliotokana na tetemeko
la ardhi lililotokea mkoani huko mapema mwezi September.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.
Mhandisi Stella Manyanya alipofanya ziara wilayani huko kuangalia athari
za tetemeko katika sekta na elimu.
Mhe.
Manyanya alisema kuwa kama serikali imejikita katika kurudisha
miundombinu ya umma ikiwemo shule ili kuwawezesha wanafunzi kuendelea na
masomo kama kawaida
“Tumeona
hali ni mbaya kwenye shule hizi mbili na sisi kama serikali hatuwezi
kuliacha suala hili lazima tuzikarabati na kuzijenga zile zinazohitaji
kujengwa upya na dhumuni ni kuhakikisha wanafunzi wanaendelea na masomo
na kuondokana na changamoto hii: Alisema Mhandisi Manyanya
Aidha
Mhandisi Manyanya amemtaka mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Nyamilima
kuacha tabia ya kutoa ruhusa hovyo kwa walimu suala ambalo linaathiri
taaluma kwa wanafunzi.
Wakati huohuo Mhandisi Manyanya amesema walimu watakaoshindwa kuwawezesha wanafunzi wao kujua kusoma na kuandika watashushwa vyeo.
0 comments:
Post a Comment