WATU 11 wamefariki Dunia na wengine sita kujeruhiwa kutokana na ajali ya gari aina ya hiace kugongana na malori matatu iliyotokea mnamo majira ya saa tano usiku wa kuamkia leo,katika kijiji cha Mubigera kata ya Nyantakara wilaya ya biharamulo mkoani kagera ,wakati wakisafiri kutoka wilaya ya kibondo kuelekea kahama mkoani Shinyanga.
Mganga mkuu wa hospitali teule ya Biharamulo Dr Grasmus Sebuyoya amethibitisha kupokea miili ya watu hao wakiwa maiti na majeruhi sita na kwamba kati ya majeruhi hao wawili hali zao ni mbaya na waliofariki wa jinsia ya kiume ni saba na jinsia ya kike ni watatu
Dr Sebuyoya amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Juma Samo (25) Joseph Otieno (30), Oscar Leonard Sebastian (27), Baseke Mashinga Nyabashiki (31), Mahalulo Charles (25) na majeruhi wa sita hajafahamika kwa kuwa hajajitambua na kwamba maiti waliofia eneo la tukio ni Tisa na wawili wamefariki baada ya kufikishwa hospitalini hapo.
Awali Mwenyekiti wa kijiji cha Mubigera Bw Mapunda Kayuki amesema ajali hiyo imetokea jana majira ya Saa 11 jioni ambapo hiece ilitaka kukwepana na roli kwenye barabara ya biharamulo kwenda kahama kwenye kijiji hicho na kugongana ambapo dereva wa hiece na tingo wake ni miongoni mwa waliofariki
Bw Kayuki amesema hiece hiyo yenye namba za usajili T.542 DKE ilikuwa ikitokea kibondo kwenda kahama ambapo maroli yaliyohusika kwenye ajali hiyo ni T.860CGS, T.103 DUJ na T.147 DUJ magari yako chini ya usalama wa jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Agustino Olomi amesema hajakamilisha taarifa kamili ya tukio hilo ikiwa ni pamoja na kutambua majina ya waliopoteza maisha mpaka ajiridhishe na taarifa, zitatolewa kwa umma bila kutia mashaka ili ndugu wa marehemu waweze kujua na kufuatilia kwa uhakika
0 comments:
Post a Comment