Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala wa
kwanza kutoka kushoto akikagua vichochoro vinavyotumiwa na wahamiaji
haramu kuingia nchini katika kijiji cha Mugulika Kata ya Bwerenyange
wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera. Kamishna Jenerali yuko mkoa wa
Kagera kujionea shughuli zinazotekelezwa na Idara yake mkoani humo.
Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala wa
kwanza kutoka kushoto akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya
Karagwe mkoa wa Kagera Godfrey Mheluka watatu kutoka kulia katika
kijiji cha Muguluka Kata ya Bwerenyange wilaya ya Karagwe Mkoa wa
Kagera.Kamishna Jenerali huyo amefanya ziara katika Vipenyo
vinavyotumiwa na wahamiaji haramu kutoka nchini nyingine kuingia
Tanzania.
Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala wa
nne kutoka kulia akiwa katika Mkutano wa Hadhara na baadhi ya
Wananchi (hawapo pichani) wa Kijiji cha Muguluka Kata ya Bwerenyange
wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera.Kamishna Jenerali huyo amefanya
ziara katika Vipenyo vinavyotumiwa na wahamiaji haramu kutoka nchini
nyingine kuingia Tanzania.
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Muguluka Kata ya Bwerenyange
wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa
Idara ya Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala katika Mkutano wa Hadhara baina
ya wanakijiji hao na Ujumbe huo wa Idara ya Uhamiaji kutoka Makao
Makuu ambapo katika Mkutano huo Dk. Makakala alitoa wito kwa
wanakijiji hao kutowahifadhi wahamiaji haramu kwenye makazi yao
sambamba na kuwataka kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola pale
wanapogundua kuna mgeni asiyeeleweka na wanamtilia mashaka kwenye
makazi yao.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
0 comments:
Post a Comment