WANAOTUNZA TAKA NDANI YA SAA 48 KATIKA KAYA ZAO MANISPAA YA BUKOBA WAONYWA


Mganga Mkuu wa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera Dkt. Peter Mkenda
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera Dkt. Peter Mkenda

Na Lydia Lugakila - Bukoba

Wananchi katika Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera wametakiwa 

kutokutunza taka katika kaya zao na maeneo mbali mbali 

ya biashara kwani kwa kufanya hivyo ni hatari kwa afya zao

 huku watakaobainika kuchukuliwa hatua za kisheria.

Kauli hiyo imetolewa na Mganga Mkuu wa Manispaa ya 

Bukoba Mkoani Kagera Dkt. Peter Mkenda wakati 

Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake 

waliotaka kujua masuala mbali mbali yahusuyo afya 

ndani ya Manispaa hiyo.

Mkenda amesema Manispaa hiyo imeweka utaratibu mzuri

 wa ukusanyaji wa taka katika mitaa ambapo magari yanapaswa 

kuzoa taka licha ya wananchi kutokutoa taka hizo kwa wakati.

MWL. MBELWA AIKACHA CHADEMA, APOKELEWA NA MAKAMU MWENYEKITI WA CCM TAIFA WASIRA



Na Grace Mpondwe,Kagera

Katika hali isiyotarajiwa leo Machi 25, 2025 aliyekuwa mgombea wa kiti cha ubunge jimbo la Biharamulo mwaka 2020 kupitia CHADEMA amekihama chama hicho na kujiunga na CCM akipokelewa na kukabidhi kadi kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Masato Wasira akiwa mkoani Kagera. 

Ziara hiyo ni ya kwanza kwa kiongozi huyo mkubwa wa CCM kuifanya mkoani Kagera tangu aidhinishwe na chama hicho kushika wadhifa huo mnamo 18-19 Januari, 2025.

Mwanasiasa huyo kijana amesema kuwa CCM ni chama kilichokamilika kimfumo kwa ajili ya kuiongoza nchi kuleta maendeleo huku amani ikiwa ni kipaumbele cha kudumu. Mwalimu amesema kuwa chama chake cha awali CHADEMA bado kinajisuka huku kikiteswa na zimwi la uchanga, upendeleo, utovu wa nidhamu na mikakati isiyofanya kazi.

Mwalimu alisema "CHADEMA leo wanahubiri NO HATE, NO FEAR!, kesho wanahubiri JOIN THE CHAIN!, keshokutwa wanahubiri STRONGER TOGETHER!, mtondogoo wana NO REFORM, NO ELECTION, Bangi za LEMA zikikolea kichwani anawaimbisha tena wanachama TONE TONE, mara NIMO", hakuna mkakati unaokamilika na kuleta matokeo kwa chama. Waswahili husema miruzi mingi hupoteza mbwa. Nimeamua kukihama chama hicho kwa hizo inconsistencies katika mikakati yake"

Kuhusu suala NO REFORM NO ELECTION, Mbelwa amesema CHADEMA imeibuka na mkakati huo kutokana na maandalizi hafifu ya kushiriki uchaguzi hivyo hiyo kauli inatumiwa kama kichaka cha kujifichia ili wasishiriki uchaguzi".

Mbelwa aliongeza kwa kusema kuwa "kitendo kinachopangwa na CHADEMA cha kuzuia uchaguzi usifayike ni ndoto ya mchana kwa sura moja na ni uhaini kwa sura nyingine. Mimi siwezi kuoteshwa ndoto hizo na kamwe siwezi kuendelea kufikiria kufanya uhaini wa namna hiyo kwa nchi yangu, sikuwahi kuwa mwanasiasa mwenye malengo machafu kwa nchi yangu".

Mwl. Mbelwa amesema "ni vigumu kwa chama kilichoshindwa kuweka utulivu kwenye ofisi moja ya makao makuu iliyopo Mikocheni kuleta utulivu kwenye nchi yenye kilomita za mraba 945,000 na watu wake milioni 60".

Ameongeza kuwa kutokana na mahaba waliyonayo Watanzania kwa CCM, ukipingana na CCM unajitakia taabu za maksudi pamoja na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo moyo kuvimba.

Amesema "Mimi Mbelwa Petro nimeona nitosheke na taabu nilizozipata kwa kuwa mwanaCHADEMA, sasa inatosha."

"Mwaka 2020 nilipogombea ubunge jimbo la Biharamulo, nilipata shida za kujitakia na baada ya uchaguzi kuisha niliambulia kuitwa Mbunge wa wananchi, nikamuuliza Mh. Mbowe, sisi wabunge wa wananchi tutakwenda kuapia wapi? Akasema, atanijibu baadae. Hajanijibu mpaka leo tarehe 25 Machi, 2025.

"Nikamuacha nikaenda kwa Kaka Lissu kwa kuwa yeye ni mwanasheria, nikamuuliza vipi Mzee sisi wabunge wa wananchi tunaapa kwa katiba ipi? Ni lini? Na wapi?".

Lissu akaniambia niwe mtulivu kwani naye yupo anatorokea Ubelgiji kutokana na hali kuwa ngumu. Nilichoka, na kupata taabu mara mbili". Ameongeza.

Mbelwa amesema "nisiseme mengi, kwa sasa nawaomba wanaCCM mnipokee, kuanzia sasa nimeacha kukunjishwa ngumi pasipo kuwa na mtu wa kupigana naye".

Kuhama kwa kada huyo linaweza kuwa pigo kwa CHADEMA jimbo la Biharamulo kwa kuwa mwanasiasa huyo alikuwa na ushawishi mkubwa hasa kwa vijana katika jimbo na mkoa mzima kwa ujumla.

KAGERA, GEITA KUANZA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AGOSTI 5,2024

Meza kuu ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk (katikati) Mjumbe wa Tume, Mhe. Magdalena Rwebangira (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Bi. Giveness Aswile


Viongozi wa kimila ni miongoni mwa wadau muhimu wa Uchaguzi hivyo Tume iliwashirikisha viongozi hao kutoka Kagera. 
Wadau kutoka makundi mbalimbali ya wanawake na vijana nao walishiriki. 
Wahariri kutoka Vyomb0 vya habari nao walishiriki. 
Vyama vya siasa nao walishiriki 
Viongozi wa Dini nao walishiriki 

Makamu Mwenyekiti Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk akiongoza majadiliano wakati wa Mkutano huo.




Maswali na maoni mbalimbali yaliulizwa na kutolewa na wadau na kupatiwa majibu.Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Bi. Giveness Aswile akifafanua jambo. 


Maswali na maoni mbalimbali yaliulizwa na kutolewa na wadau na kupatiwa majibu.

Kashai Mtafanya Biashara Kidijitali: Waziri Nape


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Stephen Byabato wametinga katika Soko la Kashai mjini Bukoba jana usiku na kushiriki kikao cha wafanyabiashara wa soko hilo.

Wafanyabiashara wa soko hilo walikutana jana Julai 15, 2024 usiku kwa ajili kushiriki kikao kilichokuwa kikijadili namna ya kuboresha soko hilo ambalo linatakiwa kufanyiwa maboresho lililopo mjini Bukoba mkoani Kagera.

Mawaziri hao walifika sokoni hapo mida ya saa 2 usiku na kupata fursa ya kuzungumza nao kisha wakawapongeza wafanyabiashara hao kushiriki kikao hicho ambacho nao walikuwa wakitoa maoni yao ya kuboresha soko hilo baada ya kuona michoro ya awali kisha na wao kueleza nini kifanyiwe maboresho.

Nape amesema kushirikishwa kwa wafanyabiashara hao kutaondoa manung’uniko na lawama kwani kumekuwa na mtindo wa wafanyabiashara kutoshirikishwa kwenye baadhi ya miradi hivyo kupelekea misigano isiyokuwa na tija.

Waziri Nape ambaye alifika mkoani humo kwa ajili ya kuendelea na ziara yake mikoa ya Kanda ya Ziwa ya kukaguwa ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano inayojengwa mikoa 26 ya Tanzania Bara ambapo anatembelea mikoa ya Kigoma, Kagera, Geita, Mwanza na Shinyanga.

Sambamba na hayo pia Waziri Nape ameahidi pindi soko hilo litakapokamilika watafungiwa intaneti ya bure (Free Wi-Fi) ili kuwawezesha kufanya biashara kidijitali.

Byabato, Nape waibukia soko la Kashai usiku, wazungumza na wafanyabiashara



Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Stephen Byabato wametinga katika Soko la Kashai mjini Bukoba jana usiku na kushiriki kikao cha wafanyabiashara wa soko hilo.

Wafanyabiashara wa soko hilo walikutana jana Julai 15, 2024 usiku kwa ajili kushiriki kikao kilichokuwa kikijadili namna ya kuboresha soko hilo ambalo linatakiwa kufanyiwa maboresho lililopo mjini Bukoba mkoani Kagera.

Mawaziri hao walifika sokoni hapo mida ya saa 2 usiku na kupata fursa ya kuzungumza nao kisha wakawapongeza wafanyabiashara hao kushiriki kikao hicho ambacho nao walikuwa wakitoa maoni yao ya kuboresha soko hilo baada ya kuona michoro ya awali kisha na wao kueleza nini kifanyiwe maboresho.

Nape amesema kushirikishwa kwa wafanyabiashara hao kutaondoa manung’uniko na lawama kwani kumekuwa na mtindo wa wafanyabiashara kutoshirikishwa kwenye baadhi ya miradi hivyo kupelekea misigano isiyokuwa na tija.

Waziri Nape ambaye alifika mkoani humo kwa ajili ya kuendelea na ziara yake mikoa ya Kanda ya Ziwa ya kukaguwa ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano inayojengwa mikoa 26 ya Tanzania Bara ambapo anatembelea mikoa ya Kigoma, Kagera, Geita, Mwanza na Shinyanga.






MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MKOANI KAGERA NA KUANZA UZINDUZI WA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI YA ZAIDI YABILIONI 12

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Kamishina wa Polisi Diwani Athumani Akishika Mwenge Kutoka kwa Mkimbiza Mwenge Kitaifa Charles F Kabeho Kuashiria Kuwa Mwenge Upo Mkoani Kagera
Kiongozi wa Mbio  za Mwenge wa Uhuru Charles Kabeho Akitoa Ujumbe wa Mbio za Mwenge Nyakabango Wilayani Muleba.
Mkimbiza Mwenge Kitaifa Charles Francis Kabeho Akipima Kuhakikisha kuwa Vipimo Katika Daraja la Kishara  Vipo Sawa
Mkimbiza Mwenge Kitaifa Kiongozi Akizindua Mradi wa Maji Izigo
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Akimpokea Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Mkoani Kagera
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu (Kulia) Akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel.
Mradi wa Soko la Ndizi Uliozinduliwa na Mwenge wa Uhuru Wilayani Muleba
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu Kushoto Akimkabidhi Mwenge  wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Luyango Ili Ukimbizwe Wilayani Muleba
Na: Sylvester Rapahel
Mwenge wa Uhuru umepokelewa leo April 8, 2018 Mkoani Kagera na Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel katika Kijiji cha Nyakabango mpakani mwa Geita na Kagera ambapo katika Mkoa wa Kagera Mwenge wa Uhuru utapitia miradi ya maendeleo 65 yenye thamani ya shilingi bilioni 12,385,330,354.
Katika miradi hiyo 65 Mwenge wa Uhuru utazindua miradi 33, utakagua miradi 19, utaweka mawe ya msingi katika miradi 13 aidha,  mchanganuo wa gharama za miradi hiyo 65 itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru ni kama ifuatavyo, Serikali kuu imechangia kiasi cha shilingi bilioni 5,817,795,968 sawa na asilimia 47%.
Halmashauri za Wilaya zimechangia  kiasi cha shilingi 671,940,497 sawa na asilimia 6%. Aidha wananchi wamechangia shilingi bilioni 2,181,496,962 sawa na asilimia 17%.  Wahisani wamechangia shilingi bilioni 3,714,096,927 sawa na asilimia 30%. 
Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2018 umebeba kaulimbiu isemayo “Elimu ni ufunguo wa Maisha; Wekeza Sasa kwa Maendeleo ya Taifa letu.” Kauli mbiu hii inawahamasisha wananchi hususani wa Mkoa wa Kagera kuwekeza katika elimu kwa kuwapeleka watoto shule ili mkoa wetu na Taifa kwa ujumla lipate wataalam wa kutosha katika kada mbalimbali za kitaaluma na hapo taifa letu litapiga hatua kubwa ya maendeleo kwa kuwatumia wataalamu wetu wa ndani.
Pamoja na Kauli Mbiu tajwa hapo juu Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wetu zitaendelea kuwahamasisha wananchi kuhusu Mapambano dhidi ya Rushwa, Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Mapambano dhidi ya Matumizi ya Dawa za Kulevya na Mapambano dhidi ya Malaria.
Mara baada ya kupokea Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Luyango na Mwenge wa Uhuru ukaanza mara moja mbio zake wilayani humo za kukagua miradi ya maendeleo.
Akitoa ujumbe wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kiongozi wa Mbio hizo Charle Francis Kabeho katika eneo la Nyakabango aliwasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii masomo ya Sayansi kwani Serikali imefanya kazi yake ya kujenga shule na vyumba vya mahabara na kuweka vifaa vya kutoasha katika maabara hizo



MKOA WA KAGERA WAVUKA LENGO KATIKA UNDIKISHAJI WA WANAFUNZI AWALI NA DARASA LA KWANZA MWAKA 2018





 
 Pichani juu  ni Shule ya Sekondari Prof Joyce Ndalichako na Wanafunzi wakiwa wanajifunza darasani

Na: Sylvester Raphael
Mkoa wa Kagera wavuka lengo la uandikishaji wa Wananfunzi katika madarasa ya awali na Darasa la kwanza kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Machi 2018 kipindi cha miezi mitatu na ni kipindi ambacho wanafunzi hupokelewa na kuandikishwa shuleni aidha, ifikapo Machi 31 uandikishwaji hukoma rasmi.
Mkoa wa Kagera kwa mwaka 2018 uliotea kuandikisha wanafunzi wa awali 85,553 wavulana wakiwa 42,678 na wasichana 42,875 lakini mkoa umefanikiwa kuvuka lengo kwa kuandikisha  wanafunzi wa Elimu ya Awali 88,343 wavulana wakiwa 44,66o na wasichana 43,683 sawa na asilimia (103.3%).
Elimu ya darasa la kwanza Mkoa wa Kagera ulilenga kuandikisha wanafunzi jumla 89,043 wavulana 44,686 na wasichana 44,357 ambapo mkoa umevuka lengo kwa kuandikisha jumla ya wananfunzi 96,539 wavulana wakiwa 48,244 na wasichana 48,295 sawa na asilimia (108.42%)
Aidha katika hatua nyingine Mkoa wa Kagera umefanikiwa kuandikisha wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa asilimia 90.66 na tayari wanafunzi hao wameripoti shuleni na kuanza masomo yao ya sekondari.Wanafunzi waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na Elimu ya Sekondari wavulana walikuwa 17,191 na wasicha 17,971 jumla 35,161.
Wanafunzi walioripoti katika shule za Sekondari Mkoani Kagera hadi kufikia Machi 31, 2018 jumla ni 31,877  sawa na asilimia 90.66 wavulana wakiwa 14,814 sawa na asilimia 86.173 na wasichana 17,063 sawa na asilimia 94.953.
Mkoa unaendelea na juhudi za kuwafuatilia wanafunzi ambao bado hawajaripoti shuleni kuhakikisha wanaripoti mara moja ili kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza. Aidha, uongozi wa Mkoa wa Kagera unatoa rai kwa wazazi na walezi wa wanafunzi ambao bado hawajaripoti shuleni kuhakikisha wanafunzi hao wanaripoti vinginevyo wazazi na walezi watauchukuliwa hatua za kisheria kwa kutowapeleka watoto wao shule.
Vilevile Mkoa wa Kagera unaendelea na juhudi za kuweka mazingira mazuri ya kujifunza na kujifunzia ili kutoa elimu bora kwa wanafunzi. Pia kuhakikisha mkoa unashika nafasi za juu katika mitihani ya kitaifa  na ufaulu wa maksi za juu kama ilivyo desturi ya Mkoa wa Kagera.
 
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa