Pichani juu ni Shule ya Sekondari Prof Joyce Ndalichako na Wanafunzi wakiwa wanajifunza darasani
Na:
Sylvester Raphael
Mkoa wa Kagera wavuka lengo la uandikishaji wa Wananfunzi katika
madarasa ya awali na Darasa la kwanza kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari
hadi Machi 2018 kipindi cha miezi mitatu na ni kipindi ambacho wanafunzi
hupokelewa na kuandikishwa shuleni aidha, ifikapo Machi 31 uandikishwaji hukoma
rasmi.
Mkoa wa Kagera kwa mwaka 2018
uliotea kuandikisha wanafunzi wa awali 85,553 wavulana wakiwa 42,678 na
wasichana 42,875 lakini mkoa umefanikiwa kuvuka lengo kwa kuandikisha wanafunzi wa Elimu ya Awali 88,343 wavulana
wakiwa 44,66o na wasichana 43,683 sawa na asilimia (103.3%).
Elimu ya darasa la kwanza Mkoa wa
Kagera ulilenga kuandikisha wanafunzi jumla 89,043 wavulana 44,686 na wasichana
44,357 ambapo mkoa umevuka lengo kwa kuandikisha jumla ya wananfunzi 96,539
wavulana wakiwa 48,244 na wasichana 48,295 sawa na asilimia (108.42%)
Aidha katika hatua nyingine Mkoa
wa Kagera umefanikiwa kuandikisha wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa asilimia
90.66 na tayari wanafunzi hao wameripoti shuleni na kuanza masomo yao ya
sekondari.Wanafunzi waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na Elimu ya Sekondari
wavulana walikuwa 17,191 na wasicha 17,971 jumla 35,161.
Wanafunzi walioripoti katika
shule za Sekondari Mkoani Kagera hadi kufikia Machi 31, 2018 jumla ni
31,877 sawa na asilimia 90.66 wavulana
wakiwa 14,814 sawa na asilimia 86.173 na wasichana 17,063 sawa na asilimia
94.953.
Mkoa unaendelea na juhudi za
kuwafuatilia wanafunzi ambao bado hawajaripoti shuleni kuhakikisha wanaripoti
mara moja ili kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza. Aidha, uongozi wa Mkoa
wa Kagera unatoa rai kwa wazazi na walezi wa wanafunzi ambao bado hawajaripoti
shuleni kuhakikisha wanafunzi hao wanaripoti vinginevyo wazazi na walezi
watauchukuliwa hatua za kisheria kwa kutowapeleka watoto wao shule.
Vilevile Mkoa wa Kagera
unaendelea na juhudi za kuweka mazingira mazuri ya kujifunza na kujifunzia ili
kutoa elimu bora kwa wanafunzi. Pia kuhakikisha mkoa unashika nafasi za juu
katika mitihani ya kitaifa na ufaulu wa
maksi za juu kama ilivyo desturi ya Mkoa wa Kagera.
0 comments:
Post a Comment