Home » » BAKOBA FC MABINGWA KAMALA CUP 2018, WAIFUNGA IJUGANYONDO BAO 3-0 KWENYE FAINALI UWANJA WA KAITABA

BAKOBA FC MABINGWA KAMALA CUP 2018, WAIFUNGA IJUGANYONDO BAO 3-0 KWENYE FAINALI UWANJA WA KAITABA


Nahodha wa timu ya Bakoba Fc akiwa amebeba Kombe la Ubingwa leo hii jioni kwenye Uwanja wa Kaitaba mara baada ya kuibuka Kidedea kwa kuifunga Timu ya Ijuganyondo bao 3-0. Katika Mchezo huo Kipindi cha kwanza hakuna Timu iliyopata bao kipindi cha kwanza, Kipindi cha pili goli zote tatu zilipatikana Goli la kwanza likifungwa na Denis Msuva, Bao la pili lilifungwa na Datius Peter na bao la tatu lilifungwa na Ezekiel Izack aliyekuwa amevaa jezi namba 10.
Picha zote na Faustine Ruta, Bukoba.
Picha ya Pamoja ya Mabingwa Bakoba Fc na Mdhamini wa Ligi hiyo ya Kamala Cup 2018 pamoja na Mgeni rasmi na Viongozi wengine.
Mabingwa Bakoba Fc wakiwa wamebeba Mwali wao.
Ligi hii ya Kamala Cup 2018 ilianza Mwezi Februari tarehe 18, 2018 na kushirikisha Timu za Kata 16 na hii leo imehitimishwa kwa Timu ya Bakoba kuibuka Bingwa.
Ndg. Salum Umande Chama akiongozana na  Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya Bukoba Bw. Deodatus Kinawilo pamoja na mdhamini wa Ligi hii Diwani Kamala Kalumuna (kulia) kwenda Uwanjani kukabidhi Wachezaji zawadi zao. Mshindi wa Kwanza kapata milioni 2 na Nusu, Wa pili kapata milioni 1 na Laki 8 na wa tatu kapata milion moja na Laki mbili.

Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya Bukoba Bw. Deodatus Kinawilo akitoa neno wakati wa ufungaji wa Ligi hiyo ya Kamala Cup 2018.
Picha zote na Faustine Ruta, Bukoba.
Mkuu wa Wilaya Bukoba Bw. Deodatus Kinawilo(katikati) ndiye alikuwa mgeni Rasmi katika Fainali hii akiambatana na Diwani Kamala Kalumuna (kulia) ambaye ndiye alikuwa mdhamini wa Ligi hii iliyohitimishwa leo hii na Timu ya Bakoba Kuibuka Kidedea kwa kuifunga Timu ya Ijuganyondo Fc Bao 3-0.  Picha zote na Faustine Ruta, Bukoba.
Viongozi mbalimbali wakiwemo Madiwani wakisalimia Timu Uwanjani.
Viongozi mbalimbali wakiwemo Madiwani wakisalimia Timu Uwanjani.
Viongozi mbalimbali wakishuhudia Timu zote mbili
Timu zote mbili zilisalimiana muda mfupi kabla ya kucheza mchezo huo kati ya Bakoba Fc vs Ijuganyondo Fc kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Kikosi cha Timu ya Bakoba kilichoanza dhidi ya Timu ya Ijuganyondo Fc
Kikosi cha Timu ya Ijuganyondo Fc kilichoanza.
Picha ya Pamoja
Wachezaji wa Timu ya Ijuganyondo wakiomba katikati ya Uwanja muda mfupi na kuanza mchezo huo kwa kasi ambao mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika ilikuwa 0-0.
Straika wa Timu ya Bakoba akimiliki mpira wakati wa kipindi cha kwanza cha mchezo huo wa Fainali.
Akiendesha mpira...
Mkuu wa Wilaya Bukoba Bw. Deodatus Kinawilo(katikati) kulia ni Ndg. Salum Umande Chama wakiwa meza kuu.
Ndg. Salum Umande Chama akiteta jambo na Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya Bukoba Bw. Deodatus Kinawilo meza kuu wakati mtanange unaendelea..
Mwali wa mshindi wa kwanza.
Makombe ya Mshindi wa kwanza, wa pili na Watatu.
Mashabiki waliingia kwa Wingi Uwanjani Kaitaba kushuhudia Fainali hiyo.
Mashabiki waliingia kwa wingi Kaitaba leo.
Mdhamini wa Ligi Mh. Kamala Kalumuna akicheza pamoja na watumbuizaji wa nyimbo mbalimbali wakati wa Mapumziko.
Huku Mashabiki wakimpogeza kwa Ligi hiyo ambayo ilikuwa ikishehenesha Mashabiki kibao Uwanjani hapo Kaitaba. Pia Mdhamini huyo amesema Ligi hiyo ni Endelevu na Mwaka kesho 2019 ataiboresha zaidi ya mwaka huu.
Taswira mbalimbali wakati wa Mtanange huo mkali wa kukata na shaka kati ya Bakoba Fc dhidi ya Ijuganyondo Fc.
Taswira mbalimbali, Kaitaba watu waliingia kwa wingi kushuhudia mtanange huo wa Fainali.
Wakati wa Fainali Kati ya Timu ya Bakoba Fc dhidi ya Ijuganyondo FC
Bao la pili lilipatikana kwa mkwaju wa Penati
Kipa wa Ijuganyondo Fc hakuona ndani...
Mfungaji wa bao la pili Datius Peter akishangilia bao lake kipindi cha pili.
Shangwe!!!
2-0 kiulaini!!!
2-0 Baadhi ya Wachezaji wa Bakoba Fc wakipongezana kwa bao.
3-0 Ezekiel Izack akipongezwa kwa kumwagiwa maji mara baada ya kuipachikia bao la tatu Timu ya Bakoba Fc
Mashabiki mnasemaje?????

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa