Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Kanali Mstaafu Fabian Massawe Akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) Ofisini kwake.
Baadhi ya Waandishi wa Habari Wakimsikiliza kwa Makini Mheshimiwa Massawe Mkuu wa Mkoa wa Kagera Wakati Alipoongea nao ofisini Kwake.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kanali Mstaafu Fabian Massawe aongea na waandishi na wamiliki wa vyombo vya habari juu ya masuala mbalimbali yahusuyo mkoa wa Kagera. Mkutano huo wa Mkuu wa Mkoa na waandishi na wamiliki wa vyombo vya habari ulifanyika jana tarehe 17/04/2012 katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Katika mkutano huo, Mkuu wa Mkoa aliongelea masuala mbalimbali yanayohusu mkoa wa Kagera ikiwa ni pamoja na kuwaasa waandishi wa habari kuandika habari ambazo zinauhakika kwa kupata vielelezo vya habari hizo kutoka kwa watu wanaohusika. Aidha pia aliwapongeza waandishi wa mkoa wa Kagera kwa kuandika habari zinazoutangaza mkoa pia na kuwaomba kuendelea kuutangaza mkoa ili kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza katika mkoa.
Elimu, akiongelea elimu Mhe. Massawe alisema waandishi waendelee na jitihada zao za kuhamasisha jamii kuendelea kuwapeleka watoto shule wenye umri wa kwenda shule. Watoto wa kike kupewa kipaumbele cha elimu, aidha Mhe. Massawe aliendelea kutangaza vita juu ya mafataki wanowaharibu watoto wa kike na kuwaharibia masomo yao kuwa atawashughulikia ipasavyo.
Wananchi kujichukulia sheria mikonononi; kutokana na tabia ya wananchi kujichukulia sheria mikononi Mhe. Massawe alitoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Kagera kupitia kwenye vyombo vya habari kuwa, jamii haipaswi kujichukulia sheria mikononi bali kufuata taratibu kwa kuwafikisha watuhumiwa kwenye vyombo vya sheria husika polisi na mahakama ili vifanye kazi zake.
Ulinzi na usalama katika mkoa wa Kagera; Mhe Massawe aliwaomba waandishi wa habari kuelimisha jamii juu ya wahamiaji haramu wanaoingia katika mkoa wa kagera. Mhe Massawe aliiomba jamii kufichau wahamiaji haramu ambao tayari wapo kwenye jamii na wanaishi na wananchi wa mkoa wa Kagera na baadhi ya wahamiaji haramu hao ni viongozi vijiji.
Aidha Mhe. Massawe alisisitiza juu ya kuwalinda wazee na Albino katika mkoa wa Kagera na kuwapiga vita waganga wa kienyeji wanaochonganisha jamii kwamba wanaweza kupata dawa za bahati au kuleta utajiri.
Na mwisho Mkoa wa Mkoa wa Kagera alisistiza wananchi wa Mkoa wa Kagera kufanya kazi kwa bidii na kuacha kunywa pombe na kucheza karata na pool wakati wa saa za kazi. Vilivile kuendelea na usafi ili kuufanya mkoa kuwa safi zaidi.
Kwa hisani ya Issa Michuzi Blog
Kwa hisani ya Issa Michuzi Blog
0 comments:
Post a Comment