WATUHUMIWA wanne wakiwemo waliokuwa askari polisi kutoka Biharamulo na
Kagera waliokamatwa na vipande 18 vya meno ya tembo wilayani
Serengeti wamepandishwa kizimbani kwa makosa mawili ya uhujumu uchumi.
Mwandishi wetu Anthony Mayunga anaripoti kutoka SerengetiWaliofikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya hiyoAmoni Kahimba ni Boniphace John Kurwa(31)
Gerard Tuti (33) David Delina(36) wakulima wakazi wa Biharamulo na
Bukoba na Zainabu Hamisi Msabaha(26)fundi cherahani mkazi wa
Biharamulo.
Mwendesha mashitaka wa polisi sajenti wa polisi Paskael Nkenyenge
mahakama iliyofurika wasikilizaji kuwa katika muda ,siku wala tarehe
isiyojulikana watuhumiwa hao walikamatwa kwa kosa la kula njama za
kufanya biashara haramu ya nyara za taifa kinyume na sheria ya kanuni
ya adhabu namba 384(16) iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Alisema watuhumiwa hao na wengine ambao hawajakamatwa Tuguro
Zakayo,Nyarata Mewama,Emanuel Kananjire(Mnyarwanda)ambao wanatafutwa
wanakabiliwa na kosa hilo .
Katika kosa la pili mwendesha mashitaha huyo aliliambia mahakama kuwa
katika kosa la pili kuwa mnamo januari 4,2013 majira ya saa 5 usiku
katika eneo la Morotonga wilayani Serengeti alikamatwa na vipande 18
vya meno ya tembo vyenye uzito wa kg 104 vyenye thamani ya
tsh,66,760,000= kinyume cha sheria.
Alisema kosa hilo ni kinyume na sheria ya kanuni ya adhabu namba 86
kifungu cha 1,2 cha sheria namba 5 ya mwaka 2009 pia kifungu cha
14(d)cha sheria za uhujumu uchumi namba 60(ii) sura ya 200
iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Kutokana na kosa hilo la uhujumu uchumi mshitakiwa hakutakiwa kujibu
lolote kwa kuwa kosa hilo mpaka wapate kibali cha mwendesha mashitaka
wa serikali(DPP).
Katika kosa la kwanza washitakiwa wote walikana,na mwendesha mashitaka
akaomba siku nyingine ya kutajwa kwa shitaka hilo kwa kuwa upelelezi
haujakamilika na kuwa dhamana .
Hata hivyo mwendesha mashitaka wa polisi Inspekta msaidizi Abdallah
Idd aliyekuwa akishirikiana na Nkenyenge aliomba dhamana izingatie
sheria namba 148 kifungu cha (5)(e)kuwa wadhamini wawasilishe fedha
taslimu zaidi ya tsh,mil.10 au hati ya mali isiyohamishika.
Hata hivyo Hakimu Kahimba alitaka kujua sharti hilo ni kwa washitakiwa
wote ama mmoja,ambapo mwendesha mashitaka Nkenyenge alidai ni kwa
mshitakiwa mmoja Kurwa,madai aliyoyakataa kwa madai kuwa yanawahusu
wote.
Mbali na hilo aliwataka warekebishe mashitaka yao kwa kuwa hayaeleweki
,kwa kutoweka muda na sehemu walikowakamatia inatia shaka ,na kuhoji
wamejuaje wanastahili kushitakiwa Mugumu na si kwingineko.
Akitoa masharti ya dhamana Hakimu Kahimba alisema kila mshitakiwa
anatakiwa atajidhamini mwenyewe kwa dhamana ya tsh,mil.2 ya maneno,pia
mshitakiwa atadhaminiwa na watu wawili wanaoaminika na kueleweka na
wawe wakazi wa Serengeti kwa dhamana ya tsh,mil.10 za maneno.
Sharti la tatu wadhamini ambao ni wakazi wa wilaya hiyo wanatakiwa
kuweka fedha taslimu mil.34 mahakamani ama mali isiyohamishika yenye
thamani ya zaidi ya tsh,mil.35
Na kuwa mali hiyo iwe na hati inayotambuliwa na imefanyiwa uthamini na
mthamini anayetambulika na serikali na wala si barua za watendaji
ambazo amesema zimechangia watu wengi kukimbia kesi zao na
hawaeleweki.
Washitakiwa ,wadhamini na ndugu waliomba mahakama ilegeze masharti kwa
madai kuwa wao ni wageni na hawawezi kuwapata wadhamini wenye sifa
hizo wilayani hapo.
Kabla ya kutoa masharti ya dhamana alitoa angalizo kwa watu
waliojitokeza kuwadhamini washitakiwa hao wakati hawafahamiani na kuwa
watanunua kesi zisizowahusu.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi januari 28 mwaka huu itakapotajwa tena na
watuhumiwa wote wamerudishwa mahabusu baada ya kukosa wadhamini wenye
sifa zilizotajwa na mahakama,na kibali kimetolewa watuhumiwa wengine
watafutwe ili waunganishwe na wenzao.
Kabla ya kufikishwa mahakamani hapo Tuti na Derina ambao walikuwa
askari upepelezi Biharamulo na Kagera walifukuzwa kazi januari 10,2013
baada ya kupatikana na kosa kijeshi ili washitakiwe kiraia.
Washitakiwa hao walikamatwa januari 6,mwaka huu katika nyumba ya
kulala wageni baada ya Kurwa kuwataja na kubainika kuwa walikuwa
askari kanzu kutoka Biharamulo na Kagera ambao ni D/c Gerard Tuti
mwenye namba za F5553 ambaye ni mpelelezi katika ofisi ya kamanda wa
makosa ya jinai wilayani Bukoba .
Askari mwingine ni D/c koplo David Delina mwenye namba E9172 kutoka
ofisi ya upelelezi Biharamulo ambao walikuwa na gari aina ya Toyota
Ballon lenye namba za usajiri T403 BJK mali ya mtuhumiwa
David.Mtuhumiwa mwingine ni Boniphace John Kurwa(31) ambaye ni raia
mkazi wa Geita ambaye alikuwa na pikipiki
yenye namba za usajili T784 CCC aina ya Sunlog.
Ambaye akiwa na mwenzake aliyetajwa kwa jina moja la Nyarata akiwa na
pikipiki yenye namba za usajili T 834 BPH Toyo ambaye alitelekeza
pikipiki na mizigo na kutokomea walikuwa wakitokea kijiji cha
Rwamchanga wakiwa na meno hayo ambayo ni sawa na tembo watatu.
Januari 10 mwaka huu askari hao walifukuzwa kazi rasmi baada ya
mashitaka ya kijeshi kukamilika na kubainika kuwa walitenda kosa la
jinai na hatimaye januari 14 mwaka huu wakapandishwa katika mahakama
ya wilaya kujibu mashitaka yanayowakabili..
0 comments:
Post a Comment