TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Halmashauri
Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera jana tarehe 13/08/2013 katika kikao chake cha siku
moja kilichofanyika mjini Bukoba imetangaza uamuzi wake wa kuwafutia dhamana ya
CCM hivyo kuwavua Udiwani Madiwani wanane wa Manispaa ya Bukoba waliotokana na
CCM.
Kwa
mujibu wa utaratibu wa kutoa adhabu kwa viongozi wa CCM walio kwenye vyombo vya
dola hasa Wabunge na Madiwani uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Mkoa sio wa
mwisho. Uamuzi huo unapaswa kupata
Baraka za Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ndipo utekelezwe.
Hivyo
basi, mpaka sasa Madiwani hao wanane waliosimamishwa wanapaswa kuendelea na
kazi zao kama kawaida wakisubiri kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya
Taifa kitakachoketi tarehe 23 Agosti, 2013 mjini Dodoma ambacho pamoja na mambo mengine
kitapitia uamuzi huo wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Kagera.
Pamoja
na hilo,
tumepokea barua za Madiwani hao za kukata rufaa kupinga uamuzi huo wa
Halmashauri Kuu ya Mkoa kwa msingi wa madai ya kukiukwa kwa utaratibu katika kufikia
uamuzi huo.
Tunawasihi
wananchi wa Bukoba na Kata husika, wanachama na viongozi wote kuwa watulivu
katika kipindi hiki ambapo suala hili linashughulikiwa na vikao vya Kitaifa.
Imetolewa
na:-
Nape M. Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI
KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
14/08/2013