HARAKATI
ENDELEVU ZA KIKUNDI CHA “BUKOBA MPYA PROJECT”
ZOEZI LA KUTOKOMEZA
MAZALIA YA MBU KATA ZA MANISPAA YA MJI BUKOBA
Ndugu
Wadau,
“Bukoba Mpya Project” ni zao la harakati endelevu
chini ya Bukoba Wadau Media katika kuchangia kuhamasisha Wanabukoba wa ndani na
nje ya Tanzania kushiriki katika kuinua hali ya mji na maisha ya wakazi wa
Bukoba. Wanachama wa harakati hizi ni
waamini wa itikadi ya UMOJA na MAENDELEO. Mpaka sasa jumla ya wanachama wasioupungua
50 kutoka ndani na nje ya Bukoba na Tanzania kwa ujumla wanashiriki harakati
hizi.
Wakiongozwa na imani kwamba “maendeleo yanaletwa na
mimi”, Wana Bukoba Mpya wamepanga kuanza jitihada ya kupambana na Malaria kwa
kutokomeza mazalia ya mbu kwenye maeneo yote ya Manispaa ya Bukoba. Jitihada
hii itatekelezwa kwa zoezi la kupulizia dawa za kuua mazalia ya mbu kwenye Kata
zote 14 za Manispaa ya Bukoba. Zoezi
litaanzia na Kata za Greenbelt (Kahororo,Buhembe,
Kitendaguro ,Ijuganyundo,Nyanga,Kibeta na Nshambya) mara tu baada ya siku kuu
kuisha kisha litaendelea kwenye kata zingine zote kadri ratiba itakavyotolewa.
Kila mmoja anayeguswa na athari za mbu na anavutiwa
na jitihada hii anaalikwa kushiriki kwa njia moja au nyingine. Unaweza kufanya
hivyo kwa:
·
Kuthibitisha kushiriki moja kwa moja kwenye zoezi tarehe na mahali
litakapofanyika
·
Kwa kuhamasisha ndugu na jamaa zako wafike kushiriki (hii ni kwa walio
mbali na nje ya Tanzania)
·
Kwa kuchangia pesa, madawa na vifaa vya zoezi (orodha ya vifaa na
utaratibu utapatiwa)
Viongozi, Watendaji na Wananchi
kwa ujumla waombwa kutoa ushirikiano na kushiriki kwa kadri wanavyoweza pale
zoezi hili litakapofanyika katika maeneo yao.
Kwa mawasiliano na maelezo zaidi juu ya jinsi ya kushiriki wasiliana
nasi kwa njia zifuatazo:
Mob: 0784 505045 / 0768 397241 /0713 883020 /0754 505043.
E-mail: ekimasha@jamiiforums.com
au bukobawadau@gmail.com
Imetolewa na:
Kitengo cha Uhamasishaji Jamii
Bukoba Wadau Media
0 comments:
Post a Comment