Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Nape Nnauye
akiwaongoza baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo kushuhudia maporomoko ya
maji ya Rusumo yaliyopo wilayani Ngara ambapo moja ya vyanzo vyake
vikubwa vya maji vimeanzia katika Mapori ya Akiba ya Biharamulo, Burigi
na Kimisi (BBK) wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara mwishoni mwa wiki
mkoani wa Kagera.
Wajumbe
wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakipewa maelezo kuhusu mipaka
ya Pori la Akiba ya Biharamulo kutoka ziwa Victoria katika kituo cha
Katete kutoka kwa Meneja wa Mapori ya Biharamulo, Burigi, Kimisi (BBK),
Bw. Bigilamungu Kagoma (wa kwanza kushoto) wakati Kamati hiyo
ilipotembelea mapori yaliyopo mkoani Kagera mwishoni mwa wiki
Meneja
wa Mapori ya Biharamulo, Burigi, Kimisi (BBK), Bw. Bigilamungu Kagoma
(wa kwanza kushoto) akiwaonesha Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na
Utalii katika ramani mahali ambako Pori la Akiba la Burigi lilipoanzia
wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara katika Mapori ya Akiba ya
Biharamulo, Burigi, Kimisi (BBK), yaliyopo mkoani Kagera hayo mwishoni
mwa wiki mkoani Kagera
Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Nape Nnauye
akiwazungumza na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo mara baada ya kujionea
Pori la Akiba la Burigi katika wilaya ya Karagwe ambayo ni moja ya kati
avyanzo vyake vikubwa vya maji ambavyo vimeanzia katika Mapori ya Akiba
ya Biharamulo, Burigi na Kimisi (BBK) wakati kamati hiyo ilipofanya
ziara mwishoni mwa wiki mkoani wa Kagera.Wajumbe
wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakiangalia hema ambalo askari
wanyamapori hulitumia kumpumzika wakiwa katika Mapori wakati wanapofanya
doria za kuwabaini majangili.Meneja
wa mpaka katika Tanzania na Rwanda ambaye pia ni Afisa Mwandamizi wa
Forodha, Polycarp Lashau akiwaongoza Wajumbe wa kamati ya Bunge ya
Ardhi, Maliasili na Utalii kushuhudia maporomoko ya maji ya Rusumo
yaliyopo wilayani Ngara ambapo moja ya vyanzo vyake vikubwa vya maji
vimeanzia katika Mapori ya Akiba ya Biharamulo, Burigi na Kimisi (BBK)
wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara mwishoni mwa wiki mkoani wa KageraWajumbe
wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakipewa maelezo kuhusiana na
mali mbalimbali za watuhumiwa wa ujangili zikiwemo baiskeli na pikipiki
zilizokamatwa katika kituo cha Katete kwenye Pori la Akiba ya Biharamulo
kutoka kwa Meneja wa Mapori ya Biharamulo, Burigi, Kimisi (BBK), Bw.
Bigilamungu Kagoma (wa kwanza kushoto) wakati Kamati hiyo ilipotembelea
mapori yaliyopo mkoani Kagera hayo mwishoni mwa wiki
(PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA-MNRT)
Kamati
ya Ardhi, Maliasili na Utalii ambayo ipo mkoani Kagera imeridhishwa na
utendaji kazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA)
baada ya kutembelea Mapori ya Akiba ya Biharamulo, Burigi na Kimisi
(BBK) kuangalia kazi za uhifadhi zinazofanywa ambapo wameipongeza TAWA
kwa kitendo cha kurudisha hali ya mapori hayo ikiwemo kurejea kwa
wanyamapori na uoto wa asili ambapo awali mapori hayo yalikuwa
yameharibiwa kwa kasi kutokana na makundi ya mifugo kufanya malisho
katika maeneo hayo.
Katika
ziara hiyo,iliyoanzia katika Wilaya ya Biharamulo, Wajumbe wa Kamati
hiyo waliweza kushuhudia eneo la Pori hilo lilipoanzia katika ziwa
Victoria na baadaye kushuhudia Pori la Burigi lililopo katika wilaya za
Karagwe na Biharamulo na badaye Pori la Kimisi ambalo lipo katika wilaya
mbili za Karagwe na Ngara.
Hata
hivyo,Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Nape Nnauye aliridhishwa na masuala ya
uendeshaji wa mapori hayo huku akiahidi kuyasaidia mapori hayo kwa
kuishauri serikali iweze kuwekeza miundombinu ili kukuza utalii katika
ukanda wa ziwa Victoria
‘’Tunatambua
kuwa TAWA ni changa haijaanzishwa muda mrefu lakini ndani ya kipindi
kifupi imeweza kufanya mambo mazuri katika kulinda Maliasili zetu , Sisi
kamati tumeridhisha na utendaji wake’’ alisema Mwenyekiti
Kutokana
na utendaji kazi wa Mamlaka hiyo , ‘Mwenyekiti wa Kamati hiyo iliahidi
kuwa watalishauri na pamoja na kuishawishi Serikali iweze kuongeza pesa
katika bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 ili iweze kutimiza wajibu
yake.
Kwa
upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla
aliielezea kamati hiyo kuwa TAWA ipo mbioni kubadili mfumo wake katika
mapori hayo ambapo badala ya kuendelea kufanya shughuli za uwindaji wa
kitalii pekee wamepanga kuanzisha utalii wa picha ili kufungua fursa za
kiuchumi katika ukanda huo.
Aidha,
Waziri Kigwangalla alisema kuwa kutokana na Mapori hayo kurejea katika
uasilia wake baada kuharibiwa kwa kiasi kikubwa na uvamizi wa mifugo
hali iliyopelekea hadi wanyamapori kuhama, Wizara inafanya utafiti ili
kuongeza baadhi ya wanyama katika Mapori hayo ili kuweza kuwavutia
watalii zaidi kutembelea maeneo hayo.
Aliongeza
kuwa, mapori hayo yana sifa ya pekee za kumvutia mtalii yeyote aweze
kutembelea katika maeneo hayo huku ukitaja wanyamapori wanne wakubwa
kuwa wanapatika katika mapori hayo isipokuwa faru pekee.
Awali
kamati hiyo ilipokea taarifa kutoka kwa Wenyeviti wa Kamati za ulinzi na
usalama za wilaya ambapo miongoni mwa mambo yaliyojitokeza uvamizi wa
maeneo ya mapori ya akiba kwa kuanzisha shughuli za kilimo pamoja na
kulisha mifugo ndani ya hifadhi.
Naye,
Mtendaji Mkuu wa TAWA, James Wakibara alisema moja ya mikakati ya TAWA
ni kubadilisha aina ya biashara kwa kuanza kuchanganya ambapo TAWA
itaendesha biashara ya uwindaji wa vitalu pamoja na utalii wa picha
katika mapori hayo kwa lengo la kuiongezea serikali mapato
Alisema
Serikali ipo katika mchakato wa kuboresha miundombinu kwa kuanza na
barabara ndani ya mapori hayo ili kuweza kuwavutia wawekezaji kujenga
hoteli mbalimbali ambazo watalii watazitumia kwa ajili ya kupumzika.